Kukaa Kijijini ni kufeli maisha

Kukaa Kijijini ni kufeli maisha

Huku kusini nilipo sasa watu wanapiga pesa za ufuta ,hapa nangoja mwezi wa 5 &6 niingie mzigoni ..

Madogo wanatembea pesa nyingi sana ,watu wanacheza na msimu tu.
True jambo ambalo huwa linaonekana watu wa vijijini wapo broke ni kukosa financial Education

Nilimsikia hata Samiah akisema hivyo kuwa Financial education ndo inawasumbua vijana wanaopiga pesa za msimu.

Na hii ukija huku mjini Unaweza kuonekana unapiga hatua kea sababu hicho kidogo unakiwekea bajeti nzuri.

Ila interm of earning money hata kijijini waweza pata pesa tu
 
Habari wana jf napenda kutanguliza huu uzi kama ulivyoandikwa hapo juu. Najua kuna baazi ya watu hawawezi kunielewa. Ila ukweli upo hivi kukaa kijijin kwa kijana unaejitafuta kimaisha ni kufeli na nasema hivi kwasbabu nazoziona mimi.

Cha kwanza.... KUZUNGUKWA NA WATU WASIOSAHIHI NA WENYE MITAZAMO HASI.
Kijijini watu wengi hawaamin kuish ndoto zao na wanaamin kila aliyefanikiwa ni mchawi, freemason,jambazi.. na kila ukijaribu kufanya kitu tofaut na mila za hapo kijijin. Wengi hawaamin unaweza kufanikiwa watakukatisha sana tamaaa

2.KUDUMAA AKILI NA KULIZIKA MAPEMA.
kijijni ukimilki pikpik tu wanaanza kukuita boss kitu ambacho kinalufanya ujionee umefanikiwa na kulizika mapema.
Pia hata mazingira hayaruhusu mtu ukue kiuchumi unakosa sehem ya kutizamia au role model tofaut na mjin

3.MZUNGUKO WA PESA NI MDOGO SANA
Kijjn ni rahis sana kuuwa pesa ukifungua biashara kutokana na mzunguko. Pesa huja mara moja tu wakat wa mavuno na kuna baazi ya biashara kama nguo baazi ya wanakijij huwa na dhana kwamba kununua nguo mpka sikukuu au safari. Na ukinunua nguo bila kuzingatia hivo vitu husema unaharibu pesa au unatumia pesa ovyo

5.KUKOSA NDOTO ZOZOTE
kijijin mtu akiamka asubuh anaenda shamba na akirud shamb anawaza aoge akae kijiweni apige stori bas siku imeisha. Na kubishana na vitu visivokuwa na msingi na kupiga umbea

Kiufupi yapo mengi yanayomzuia mtu kukua na kuwa na mtazamo chanya ila kwa machache ndo hayo

NB.ushauri wangu kama unajitafuta kimaisha usikae kijijini sana ni bora uanze na level za wilaya
ILA KUKAA VIJIJINI VIJANA WENZANGU NI KUFELI KIJIJINI HAKUNA MAENDELEO NA NDO MAANA HAKUNA AFSA BIASHARA WALA MASOKO
KIJIJINI SHUGHULI KUBWA NI KILIMO NA NDO MAANA KUNA AFSA KILIMO

kama una maoni unaweza ukashare ila mi kwa mtazamo wangu upo hivyo
upotoshaji 🐒

kwahiyo huko mjini, stress za kukosa ajira na kuota mvi, huku hujaoa, huna plot, huna mtoto hata wa kusingiziwa tu, huna mchumba, nguvu za kijinsia zinalegalega, huna hela ya kodi , umri umesonga n.k ndio kukua kiakili?🐒

wadogo zako mlosoma pamoja ulowacha waloishia darasa la 7, huku kijijini wameo, wana watoto wa kutosha, wana mijumba ya maana, wana miliki matrekta na magari, matoyo au bodaboda kama zote, wanakopsha watumishi, wana mashamba mamia ya hekta nk. huko ndio kudumaa akili?🐒

msione aibu rudini nyumbani , still you can make it🐒
 
Unakaa mjini halaf unakaa sehem ka mbagala au gongo la mboto au kigambon shida tupu kuanzia usafir mpk maisha unapanga chumba kimoja kwa tabu halaf kijijin watu wanaishi maisha mazur tu bora nn ss
 
NI vzr kupata exposure ya mazingira tofauti tofauti kila sehem ina fursa zake na inawezekana ukawa na base sehem zote ili ku alternate/ diversify resources zako.
 
Habari wana jf napenda kutanguliza huu uzi kama ulivyoandikwa hapo juu. Najua kuna baazi ya watu hawawezi kunielewa. Ila ukweli upo hivi kukaa kijijin kwa kijana unaejitafuta kimaisha ni kufeli na nasema hivi kwasbabu nazoziona mimi.

1. KUZUNGUKWA NA WATU WASIOSAHIHI NA WENYE MITAZAMO HASI.
Kijijini watu wengi hawaamin kuish ndoto zao na wanaamin kila aliyefanikiwa ni mchawi, freemason,jambazi.. na kila ukijaribu kufanya kitu tofaut na mila za hapo kijijin. Wengi hawaamin unaweza kufanikiwa watakukatisha sana tamaaa

2. KUDUMAA AKILI NA KULIZIKA MAPEMA.
Kijijni ukimilki pikpik tu wanaanza kukuita boss kitu ambacho kinalufanya ujionee umefanikiwa na kulizika mapema.
Pia hata mazingira hayaruhusu mtu ukue kiuchumi unakosa sehem ya kutizamia au role model tofaut na mjin

3. MZUNGUKO WA PESA NI MDOGO SANA
Kijijni ni rahis sana kuuwa pesa ukifungua biashara kutokana na mzunguko. Pesa huja mara moja tu wakat wa mavuno na kuna baazi ya biashara kama nguo baazi ya wanakijij huwa na dhana kwamba kununua nguo mpka sikukuu au safari. Na ukinunua nguo bila kuzingatia hivo vitu husema unaharibu pesa au unatumia pesa ovyo

4. KUKOSA NDOTO ZOZOTE
Kijijini mtu akiamka asubuh anaenda shamba na akirud shamb anawaza aoge akae kijiweni apige stori bas siku imeisha. Na kubishana na vitu visivokuwa na msingi na kupiga umbea

Kiufupi yapo mengi yanayomzuia mtu kukua na kuwa na mtazamo chanya ila kwa machache ndo hayo

NB. Ushauri wangu kama unajitafuta kimaisha usikae kijijini sana ni bora uanze na level za wilaya
ILA KUKAA VIJIJINI VIJANA WENZANGU NI KUFELI KIJIJINI HAKUNA MAENDELEO NA NDO MAANA HAKUNA AFSA BIASHARA WALA MASOKO

KIJIJINI SHUGHULI KUBWA NI KILIMO NA NDO MAANA KUNA AFSA KILIMO

Kama una maoni unaweza ukashare ila mi kwa mtazamo wangu upo hivyo
Kwa taarifa yako labda uzungumzie mtu binafsi mwenye mgando wa mawazo, lakini kijijini watu wanapiga hela na Wana mafanikio kuliko wewe uliyeandika Uzi huu... Nenda kule Kijiji Cha Mang'ola wilayani Karatu uone kua ulicho andika ni upuuzi, simaanishi kua yote uliyo sema ni upuuzi ila kumaanisha kua kukaa kijijini ni kushindwa maisha hiyo ndo upuuzi, shamba Lina pesa kuliko kitu chochote hapa nchini ukiachana na kulitumia shamba kama kupata madini ambayo kimsingi mzungu ndo anachota, lakini ktk maisha yetu, Kijiji kinaweza kukutoa zaidi ya hizi blaablaa za mjini

Imagine mjini unapopasifia, watu wamejaa vijiweni na hawana kila kitu, mifumo ya upataji pesa imegeuka kua ni ujanja ujanja tu kwa karibu 85%ya waTanzania waishio mjini, lakini kwa walio Vijijini wako wazi ktk upataji pesa kwao, labda tu mtu akose vyanzo, mjini kumejaa vijana mateja, wavuta bangi, waropokaji wa matusi hovyo vijiweni, mchana kutwa wanaongelea Simba na Yanga na wanarudi nyumbani hawana pesa Wala akili yoyote ya nini wafanye kujikwamua kimaisha, kiufupi kijijini ndiko kwenye neema.
 
Ndiyo maana mkifa maiti zenu zikiletwa huku vijijini kuzikwa, hua tunakataa kuchimba kaburi mpaka ndugu zenu watulipe maana mnadharau sana baadhi yenu.

Yaani umeamua kutuanzishia uzi kutusimanga kisa vipesa kidogo tu vya udalali ulivyoshika hapo mjini.
 
😁😁😁 hakika inafikirisha sana
 
Nnachofahamu tatizo kubwa la vijijini ni kutokuwa na shughuli zakufanya mtu aingize pesa mwaka mzima, lakini wapo wanaojiongeza na kufanya vizuri, mfano mtu analima mazao yakuvuna kila baada ya miezi mi3 bado anafuga mfano nguruwe anauhakika wa kuzalisha na kuuza mifugo kila baada ya miezi mi4, kwaiyo kiujumla inategemea mtu binafsi, lakini kwa ambae hana mtaji bora awe mazngira ya kuingiza hela kila siku kwenye mishemishe halafu akipata mtaji ambao hata akiingiza hela shamban ataweza kuish vzuri tu anavyosubiri mavuno, mwisho wa siku maisha ni popote ndiomaana kuna watu wa hali zote mijini na vijijini.
 
Vijana wanalima wanapiga pesa kijijini na wanajenga wananunua ndamA wanawaboresha ukikaa mjini bila mtaji au kazi utaishia kuvaa na kumiliki simu
Vipi wale ambao hawawezi kalima?
 
Nnachofahamu tatizo kubwa la vijijini ni kutokuwa na shughuli zakufanya mtu aingize pesa mwaka mzima, lakini wapo wanaojiongeza na kufanya vizuri, mfano mtu analima mazao yakuvuna kila baada ya miezi mi3 bado anafuga mfano nguruwe anauhakika wa kuzalisha na kuuza mifugo kila baada ya miezi mi4, kwaiyo kiujumla inategemea mtu binafsi, lakini kwa ambae hana mtaji bora awe mazngira ya kuingiza hela kila siku kwenye mishemishe halafu akipata mtaji ambao hata akiingiza hela shamban ataweza kuish vzuri tu anavyosubiri mavuno, mwisho wa siku maisha ni popote ndiomaana kuna watu wa hali zote mijini na vijijini.
Vipi wale ambao hawawezi kulima?
 
Sasa milion 50 ndio kapiga pesa hapo?

Mjini itabaki kuwa mjin tu na ndio maana ma viwanda , ma kampuni na kila aina ya huduma bora zipo town

Milion 50 mpaka auze mpunga wakati mjin mafogo wanazipiga kila leo

Na ndio maana akina manji, bakhresa na kina Mo wengi wapo mjin
Kwa nchi masikini kama hii million 50 nyingi sana kwa watu walio wengi
 
Hakuna biashara kijijn tuache kuzunguka , soko Lao kubwa wanategemea mjin,,
Kijijn NI sehemu fulan ya kupata mtaji ukipata mtaji sehemu ya kukuza mtaji wako ni mjini Tu ,

Kijijn Fanya kilimo na ufugaj ila uwe unatokea mjin,
Sahihi
 
Unasema kweli mkuu. Mimi tangu nimalize chuo nimekaa kijijini miaka mitano, kukaa huku ni kupoteza muda na nguvu. Japo kwa miaka hii nimepata kamtaji lazima mwaka huu nitimkie town. Kijijin watu wanalogana na kukwamishana sana. Pia wanalizika mapema sana, kijana ananunua ngombe mbili au tano anaanza kutamba amefanikiwa, hzo ngombe tano zimemchukua miaka minne na zaidi kuzinunua.
Nikweli pia watu wanalima sana, hapa nilipo kuna jamaa wanne vijana wanalima mpunga hawakosi gunia mia kila mwaka, niwachache hao na wanamashamba mengi, kulima ekari kumi kuna hitaji gharama kubwa kuanzia kukodi, kulima mpaka kuvuna. Watu wengi hawana mashamba. Kingine watu kijijin wanajadiliana sana. Mi naona bora kukaa mjini halaf tafuta mashamba kijijin lima, muda wa kilimo piga kilomo kijijin kaa mjini.
Sahihi
 
Jarib kukaa unazan kuna kilimo siku hizi bila mtaji kila kitu kinahitaji pesa bro
Unawashauri wote waje mjini. Tupe mbinu sasa kwamba baada ya watu kutoka vijijini, utatoa wapi vibarua wa kukulimia ama kufanya kazi shambani
 
Back
Top Bottom