Kukaa Kijijini ni kufeli maisha

😁😁😁😁
 
Reactions: _ly
Dont conclude in that, kila mtu panamfaa mahali anapoishi kulingana na mtazamo wake (Vision)
Kuna watu ukiwaangalia mjini wanaishi maisha ya tabu sana. Usikae mjini kama huna akili ya kimaisha.

Wapo watu wanaishi mijini wala haisaidii bali wanajitengenezea umaskini tu
 
Kahama ni kijijini?Ili nichukue maamuzi saa hii
 
Sasa hao wanaokaa mjini Kwa mateso wakienda Kijijini ni innaillah wa innalillah rajuuuuuuun.
 
Vijana wanalima wanapiga pesa kijijini na wanajenga wananunua ndamA wanawaboresha ukikaa mjini bila mtaji au kazi utaishia kuvaa na kumiliki simu
Napingana nawe:

Kuishi kijijini sio ufinyu wa akili_Wapo wapambanaji wenye fursa (kijijini), mauzo/biashara zao wafanyia mjini na kurudi kijijini .
 
Kwa mtazamo wako (na wale wenye awazo kama yako), uko sahihi ila inafaa utoke nje ya box na uyaangalie maisha ya kijijini kwa kwa mtazamo chanya.
Kumbuka kwamba hivyo vyakula vyote mnavyokula hapo mjini vinatoka kijijini. Siku hizi sio sawa na enzi au zama zile ambapo hakukuwa na mawasiliano. Walio mjini wanawasiliana na walio vijijini kwa simu, email au Whatsapp na biashara inaendelea baina ya mzalishaji na mlaji ndani ya muda mfupi sana. Vijana walio vijijini kama sio wale wavivu na walevi kupindukia wanapiga hela ndefu na sio tu katika msimu wa kilimo bali kwa mwaka mzima kwa kuzingatia shughuli au kipindi. Kijijini huwezi kufanya shughuli -biashara moja tu na ukapata mafanikio. Huku vijijini kuna kila fursa isipokuwa fursa ya Utapeli-uchwara hakuna .
Fursa zilizopo ni e.g.
1. Ufugaji-kibiashara ikiwemo biashara ya mazao ya mifugo -mayai, mifugo hai, nyama, ngozi etc
2. Kilimo-biashara; Unalima kile utakachouza/kina soko la mapema au kulima kwa mkataba mazao ya muda mfupi na yasiyo asilia hapo kijijini e.g. dengu, rozela, mkunazi, Ashwagandha (Withania somnifera) .n.k
3. Biashara ya duka la rejareja na kuuza vyakula vya mifugo
4. Ufundi e.g. Utengenezaji vifaa vya chuma - grills, uchomeleaji (vijiji vingi kuna umeme)
5.Uanzishaji wa karakana ndogo kutoa huduma za kifundi e.g. Kukarabati/kurepair vifaa vya usafiri (gereji) ref. hakuna kijiji kisicho na bodaboda
6. Utoaji wa huduma ya Lishe e.g. kuweka genge la vyakula - Dagaa, nyanya, vitunguu n.k. au Kuanzisha Bucha n.k.
NB: Fursa huku Vijijini ni nyingi sana - inahitaji tu kijana ajitambue na azitambue fursa zilizopo na kupata ushauri afanye kipi na kwa malengo gani na kwa muda gani.
Vijana wengi hukimbilia mjini kwa kuhadaiwa na vibiashara vya mkononi a.k.a Umachinga, Starehe au kuajiriwa kwenye makampuni au kuajiriwa kwa watu binafsi.
 
Hakuna biashara kijijn tuache kuzunguka , soko Lao kubwa wanategemea mjin,,
Kijijn NI sehemu fulan ya kupata mtaji ukipata mtaji sehemu ya kukuza mtaji wako ni mjini Tu ,

Kijijn Fanya kilimo na ufugaj ila uwe unatokea mjin,
 
Ww kaa na akili zako hivyo hivyo kuna watu wanapiga hela mara hata kumi ya vihela unavyokimbizana nazo huko town.Kuna dogo aliuza tu mpunga wake kapiga m 50 ww una hata m 5 hapo
Hapo ukute unamtaja mtu yupo Katavi mkoa ambao wakikusanya kodi yao wote kwa mwaka ni bilioni 7 tu😂.
Wakati kwa kwa Ilala hiyo ni kodi ya biashara ya mtu mmoja
 
You Nimefanya kazi vijiji vya Tabora,Singida Aisee vijana wanalewa sana vipombe vinaitwa ambulance ni kama visungura...kifupi wamechoka,unaweza mwambia Mtu Shikamoo kumbe umemzidi miaka 9🙆
 
Hakuna biashara kijijn tuache kuzunguka , soko Lao kubwa wanategemea mjin,,
Kijijn NI sehemu fulan ya kupata mtaji ukipata mtaji sehemu ya kukuza mtaji wako ni mjini Tu ,

Kijijn Fanya kilimo na ufugaj ila uwe unatokea mjin,
Mkuu; mbona unajipinga tena mwenyewe katika comment yako? Kama unakubali kwamba soko lao kubwa lipo huko mjini shida sasa iko wapi? Hitajio la kimsingi ni Mzalishaji (Supply) na Mlaji (Demand) Kama hayo ya kimsingi yapo ni kazi ya hao vijana kuchagua akae upande gani wa hiyo mizania. Kama kijana hajajipanga na ameshindwa kuzibaini fursa zilizopo huko kijijini, hata akienda kukaa mjini ni kazi bure tuu, ataishia kuwa Teja na kama ni Ke ataishia kudanga.
Usisahau kwa hali ya kimaisha ya sasa kuna mstari mwembamba sana kati ya maisha ya kijijini na ya mjini - kama ni ugumu wa maisha upo pande zote.
 
You
Nimefanya kazi vijiji vya Tabora,Singida Aisee vijana wanalewa sana vipombe vinaitwa ambulance ni kama visungura...kifupi wamechoka,unaweza mwambia Mtu Shikamoo kumbe umemzidi miaka 9🙆
Hoja hii mbona iko kotekote? Mjini baadhi ya vijana (Ke na Me) wanavuta bangi, unga na wameenda mbali zaidi mpaka hata Me wamejiingiza kwenye Biashara ya ngono(Ushoga).
Ulevi wa pombe na madawa ya kulevya upo Mjini na vijijini kadhalika lakini kwa viwango tofauti.
 
Hakuna biashara kijijn tuache kuzunguka , soko Lao kubwa wanategemea mjin,,
Kijijn NI sehemu fulan ya kupata mtaji ukipata mtaji sehemu ya kukuza mtaji wako ni mjini Tu ,

Kijijn Fanya kilimo na ufugaj ila uwe unatokea mjin,
Fact bro
 
Basi Leo wanakijiji mtamfokea mleta mada[emoji16][emoji16][emoji16][emoji16][emoji16][emoji16][emoji16]ila na Mimi naunga mkono hoja kukaa Kijijini aiseee HAPANA....Kuna upweke sana[emoji849]
Kijijini kupo poaa sanaa, [emoji23][emoji23][emoji23]
 
Kijijini kupo poaa sanaa, [emoji23][emoji23][emoji23]
Uwii mkinikuta huko mpige simu polisi unaweza Kuta nimetekwa!Kijijini kukaa pasizidi siku Tano,utaanza kupaukaa😁
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…