Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Nimekaa jiji moja hapa nchini miaka 16, ni kazi za ofisini tu zilizoniokoa kimaisha, sasa niko kijijin 100% mpaka nalaum mbona nilichelewa kwenda huko. Ninafanya vizuri zaidi na bado kazi ofisini huko mjini nafanya vema tu. Mjini sio pa kukimbilia kama huna shughuli maridhawa, utaishia kuishi kwa stress tuBora umesema ukweli,nikiwahi kukaa Kwa mda mjiwmema kigamboni aisee Kuna watu wanaishi Kwa kuunga unha sana nyumba mbovu Ile mbaya ila ukimwambia aende kijijin hataki but ukoangalia life yake hata mie wa kijijin hanifikii hata nusu ya mali nilizonazo
Mkuu umesahau na mkoa wangu pia Manyara, macharlee wakiivisha vitunguu ni shida hizo Jogoo wanakunywa Kama majiYou
Nimefanya kazi vijiji vya Tabora,Singida Aisee vijana wanalewa sana vipombe vinaitwa ambulance ni kama visungura...kifupi wamechoka,unaweza mwambia Mtu Shikamoo kumbe umemzidi miaka 9🙆
Ww kaa na akili zako hivyo hivyo kuna watu wanapiga hela mara hata kumi ya vihela unavyokimbizana nazo huko town.Kuna dogo aliuza tu mpunga wake kapiga m 50 ww una hata m 5 ha
Sio kweli, ukikaa kwa malengo unatoboa, mimi naisho dar ila ilotokea kipindi flano nilaenda masasi nikavutiwa na kilimo cha korosho nikanunua hekari 10 zenye mikorosho tayari, kula msimu napata si chini ya 18m. Nashangaa vijana wa kusini wamejazana mbagala na wanaishia kwa shida wakati wana mashamba huko kwaoHabari wana jf napenda kutanguliza huu uzi kama ulivyoandikwa hapo juu. Najua kuna baazi ya watu hawawezi kunielewa. Ila ukweli upo hivi kukaa kijijin kwa kijana unaejitafuta kimaisha ni kufeli na nasema hivi kwasbabu nazoziona mimi.
1. KUZUNGUKWA NA WATU WASIOSAHIHI NA WENYE MITAZAMO HASI
Kijijini watu wengi hawaamin kuish ndoto zao na wanaamin kila aliyefanikiwa ni mchawi, freemason,jambazi.. na kila ukijaribu kufanya kitu tofaut na mila za hapo kijijin. Wengi hawaamin unaweza kufanikiwa watakukatisha sana tamaaa
2. KUDUMAA AKILI NA KULIZIKA MAPEMA
Kijijni ukimilki pikpik tu wanaanza kukuita boss kitu ambacho kinalufanya ujionee umefanikiwa na kulizika mapema. Pia hata mazingira hayaruhusu mtu ukue kiuchumi unakosa sehem ya kutizamia au role model tofaut na mjin
3. MZUNGUKO WA PESA NI MDOGO SANA
Kijijni ni rahis sana kuuwa pesa ukifungua biashara kutokana na mzunguko. Pesa huja mara moja tu wakat wa mavuno na kuna baazi ya biashara kama nguo baazi ya wanakijij huwa na dhana kwamba kununua nguo mpka sikukuu au safari. Na ukinunua nguo bila kuzingatia hivo vitu husema unaharibu pesa au unatumia pesa ovyo.
4. KUKOSA NDOTO ZOZOTE
Kijijini mtu akiamka asubuh anaenda shamba na akirud shamb anawaza aoge akae kijiweni apige stori bas siku imeisha. Na kubishana na vitu visivokuwa na msingi na kupiga umbea.
Kiufupi yapo mengi yanayomzuia mtu kukua na kuwa na mtazamo chanya ila kwa machache ndo hayo
NB. Ushauri wangu kama unajitafuta kimaisha usikae kijijini sana ni bora uanze na level za wilaya
ILA KUKAA VIJIJINI VIJANA WENZANGU NI KUFELI KIJIJINI HAKUNA MAENDELEO NA NDO MAANA HAKUNA AFSA BIASHARA WALA MASOKO
KIJIJINI SHUGHULI KUBWA NI KILIMO NA NDO MAANA KUNA AFSA KILIMO
Kama una maoni unaweza ukashare ila mi kwa mtazamo wangu upo hivyo