Kukabwa usiku na kushindwa kupumua vizuri usiku ukiwa umelala

Kukabwa usiku na kushindwa kupumua vizuri usiku ukiwa umelala

shimwe

JF-Expert Member
Joined
Jul 20, 2013
Posts
213
Reaction score
82
Mara nyingi inanitokea sana usiku nikiwa kwenye usingizi najitahidi kuita sauti haitoki hata kidogo nikijitahidi kujigeuza upande mwingine nashindwa nikijitahidi kuamka kwa nguvu zote nashindwa mpaka hiyo initoke na mimi nafanya kazi moja tu ya kubana pua mdomo kwa sekunde kadhaa ndoo napata nafuu.

Kwa anayejua tatizo kama hili linasababishwa nini asisite kunishauri, wengine wanasema ni jini ni kweli?
 
Nimeogopa mkuu, pole wewe ni me au ke?
Cc: MziziMkavu
 
Last edited by a moderator:
mimi ni dume la simba ndg yangu mzizi mkavu
 
Kabla ya kulala weka mfupa wa nguruwe chini ya godoro.
 
kula kitimoto kwa afya yako kisha chukua mfupa au kama vipi unatengeneza kabisa cheni unafungia mfupa au jino unavaa kwisha.la sivyo wakati wa kulala sali
 
Wapo wanaosema hilo ni jini. Nasema hayo ni mapepo tu. Yawe majini au majinamizi yote ni mapepo tu. Ndg yangu, iko kiboko ya hayo yoote. Kwanza jaribu kiila utakachoambiwa humu jf na pale utakapoona vimeshindikana hii yangu haitashindwa.
Lipo jina moja tu, jina lipitalo majina yoote. Hilo jina, mwenye hilo jina amepewa mamlaka yote, mbinguni juu na duniani pia. Huyo mwenye hilo jina aliepewa hayo mamlaka yote, hakufanya uchoyo. Ametupa na sisi yaani ametupa hayo mamlaka, ili sisi tukikutana na mateso kama yako tulitumie hilo jina kwa mamlaka aliotupa litusaidie.
Mfano, ukilipwa mafao yako, hawakupi fedha taslimu. Wanakupa karatasi iitwayo cheki. Imeandikwa kiasi na idara iliyokupa hiyo cheki. Ukienda Benki tu, unaitoa kule unangojea kidogo tu. Mtunza fedha wa benki anakupa mamilioni yako una sepa.
Sasa, huyo mwenye hilo jina ametupa sisi wanadamu watakao muamini kuwa anao huo uwezo, ametupa hilo jina tulitumie.
Linaitwa Jina la YESU KRISTO WA NAZARETI. Weye, ukilitaja jina hilo, hata kwa kuwaza tu; HAKUNA nasema HAKUNA pepo atakaye simama. Hutoweka ghafla.
Kabla hujalala sema hivi; YESU WA NAZARETI UNILINDE. Anza leo uone. Tafuta biblia uusome mstari huu; Luka 10 : 19
ni PM kupata simu yangu. Niite saa yeyote nitakuombea hata kwa mbali wala hutaona taabu hiyo tena.
 
Mkuu pole sana. Kweli hilo ni jini(nightmare)jinamizi Nikiweka hapa picha yake unaweza kufa kwa kihoro. Soln: 1. Fanya maombi ya kukemea hiyo hali kwa nguvu zote(kwa jina la Yesu) na uendelee kusimama kwenye maombi, ukilegalega tu lazima litarudi tena kwa hasira zote si utakuwa ulisharijeruhi!!! 2:Option: Kama ukishindwa kusimama kwenye maombi ukitaka kulala weka kisu kidogo chini ya mto lazima likimbie. 3:Option: Tafuta mfupa wa Noah uwe unaweka chini ya mto. Nb: Option no:2 na 3 hutumika kwa muda tu, kama siku tano mfululizo.
 
Haya majini wakati mwingine mnayasingizia sana. Makosa ya kuundaa mwili kwa ajili ya kulala mnawasingizia mapepo!!, mtu unakula chakula kizitoooo usiku halafu hapo hapo ndani ya dakika 20 umesharukia kitandani unadhani mwili utaacha kumisbehave???!!!!
 
kula kitimoto kwa afya yako kisha chukua mfupa au kama vipi unatengeneza kabisa cheni unafungia mfupa au jino unavaa kwisha.la sivyo wakati wa kulala sali

kiti nakula sana mpaka.mafuta yake najipakaa mwili mzima.
 
mara nyingi inanitokea sana usiku nikiwa kwenye usingizi najitahidi kuita sauti haitoki hata kidogo nikijitahidi kujigeuza upande mwingine nashindwa nikijitahidi kuamka kwa nguvu zote nashindwa mpaka hiyo initoke na mimi nafanya kazi moja tu ya kubana pua mdomo kwa sekunde kadhaa ndoo napata nafuu kwa anayejua tatizo kama hili linasababishwa nini asisite kunishauri, wengine wanasema ni jini ni kweli???

Hali hii hata mimi hunitokea mara kadhaa,inakera sana aisee wakati mwingine mpaka pumzi unakosa ukija zinduka kwa nguvu unajisikia kuchoka sana
 
Niliwahi kuwa na hilo tatizo kwenye miaka ya 2006 hadi 2008. Nikamshirikisha kiongozi wangu WA kiroho, maana kama Ni maombi na sala kabla ya kulala nilikuwa nafanya sana. Na hiyo hali ilikuwa ikinitokea hata nikilala mchana. Nilivyozungumza nae, akaniambia; hiyo wakati mwingine husababishwa na kutolala vizuri. Yawezekana Ni uchovu au tu mwili wenyewe unakuwa haujalala katika hali stahiki. Hasa uti WA mgongo Unapokuwa hauja pumzishwa vizuri, unapostuka mwili hukosa mawasiliano kwa muda. Jifunze kulala kifudi fudi, au chali katika godoro bora. Unaweza uka google 'sleeping paralysis' ukasoma zaidi juu ya tatizo lako.

Sent from my BlackBerry 9810 using JamiiForums
 
Tusijekuwa tunashauri mtu kulala na mifupa wakati ana tatizo la moyo! Natahadharisha tu jamani!
 
Kula chakula chepesi nyakati za usiku,lala kwa wakati na jifunze kulala kifudifudi.Hamna cha mapepo wala majini.Hizi habari za kuaminishwa kuhusu mapepo zimewafunga watu wengi sana fikra
 
Yaah inatokea hasa unapolala chali nahisi kutakua kuna sababu ya kibiologia behind.
 
Back
Top Bottom