Tunatakiwa tufahamu kuwa duniani kote
mhalifu anayetafutwa (hata mimi na wewe ikitokea ,Mungu aepushe ) hukumbwa na vitu
viwili vikuu ambavyo ni :
1) Hofu (Fear): ni hali ya
wasiwasi inayompata mtu au mnyama mbele ya mwingine au kingine kisichompendeza au
kuhatarisha usalama wake.
2) Woga (Paranoia/ Anxiety) (Naomba nirekebishwe): ni tabia ya kupatwa na
hofu kupita kiasi inayokuwa
ndani ya binadamu juu ya
kitu au vitu fulanifulani.
Hivyo vitu viwili hupelekea kufanya makosa ya
kimkakati ambayo vyombo vya dola huvitumia kama
faida kwao! Ukiwa na hivyo vitu ni
lazima narudia tena ni lazima utafanya makosa.
Moja ya mafunzo ya
kijasusi na
machache kwa vyombo vya
dola ni kukuondolea hivyo vitu vikuu viwili na kukupa vitu vipya! Baada ya kuondolewa hivi vitu huwa wanaweza
kuhimili hali zote! Mimi na wewe hatuwezi!
Mfano 1: mwangalie
Kikwete na marehemu
Magufuli reaction zao kuhusu jambo lolote, utagundua mmoja
amekasirika mwingine
anatabasamu.
Unaweza kuona huyu aliyekasirika ni jasiri kumbe ni kinyume chake! Mwingine ana hisia mwingine
anaigiza hisia!
Mfano 2: Mwangalie
Putin na
Kim wa Korea Kaskazini, namaanisha kampe
taarifa Kim kuwa wanajeshi wako
1000 wamekufa halafu nenda kwa Putin kampe hiyo taarifa!
Nb: 1) Hisia hupelekea kufanya makosa!
Nb 2) Mhalifu siku zote huwa mwoga!
Nb 3) Dola halina hisia ila watu wake wana hisia!
Ni mtazamo wangu!
"The escape man is still human, he is still afraid, Fear becomes paranoia, paranoia ultimately psychosis. I bring this up because in one hundred and forty years, the fundamental mind of the escape man has not changed "- FBI Special Agent Alexander Mahone (Prison Break)