Kukamatwa Juzi kwa Kato Rasta Muuaji wa Afande Muna Kawe ni jibu tosha kuwa huwezi Kuikimbia popote pale Jamhuri kama ikikutaka

Kukamatwa Juzi kwa Kato Rasta Muuaji wa Afande Muna Kawe ni jibu tosha kuwa huwezi Kuikimbia popote pale Jamhuri kama ikikutaka

Kuna Mwamba nae kanipa Elimu kama hii yako Mkuu. Unataka kuniambia asingetumia Simu kamwe asingedakwa?

Ina maana Polisi wana Mtambo wa Kusoma Mnara ulioko na kisha wakaja Kukudaka kama Kuku Uvunguni mwa Kitanda?

Naomba kujua hasa Polisi hufanya nini ili Kumkamata Mhalifu aliyekimbia kwani hata Mimi sikutegemea huyu Dogo Kato Rasta kuwa angekamatwa wakati nilisikia kuwa alikuwa akitaka Kutorokea nchini Msumbiji.
Kama ana move na simu basi mifumo iliyopo TCRA/ kampuni za simu inasoma exactly simu yake inapokea mawimbi kutoka mnara gani wa simu. Hivyo taarifa hio inatumiwa na polisi (Cyber Crime Unit) kuwasiliana kwa radio na polisi wa eneo hilo kwa ajili ya kumfuatilia muhusika. Hata yule kijana aliywua Rombo akakamatwa Jema Ngorongoro kule ni makosa haya haya muhalifu anayofanya. Kutumia vifaa vya teknolojia.

Kwa nchi zilizoendelea, detection ya movement ya muhalifu inafanyika hata kwa kuangalia manunuzi yake anayofanya (mf credit card, ATM anayotumia/aliyotumia mara ya mwisho), ticket za bus (zipo electronically), camera za barabarani (street camera), CCTV za maeneo maarufu kama alipita hapo n.k. Itoshe kusema tu huyo Rasta alikosa uelewa mdogo sana wa mambo otherwise asingeweza kushikwa maana TZ bado coordination ya hizi aspect ni mbaya.
 
PT hawa hawa walioshindwa kuwakamata washambuliaji wa Lissu?
Hawa hawa ninaowajua mimi?
Intel mbovu za PT, Tiss, na Jw mpaka majasus ya Rwanda yanaingia nchini yanateka na kuondoka na watu 5 wa familia moja?
Huyo jamaa simu ndio iliomponza ukiwa na msala km ule usitumie simu kabisa utakamatwa asubuhi na mapema

Sent from my SM-A013G using JamiiForums mobile app
 
Angefanikiwa kuvuka border chance ya kumkamata ingekua ndogo kama ni muhuni kweli.
Usijifaraji kumbuka kisa Cha walio muuwa mzungu Walter mpinga ujangiri mmoja alivuka mpaka kakamatwa Burundi.
Kumbuka tukio la majuzi vijana wadogo wa kiha waliuwa wenzao kwa sumu wakakimbilia Burundi waka karibia kukamatwa huko huko kwa ushirikiano wa majeshi ya polisi ndipo wakarudi nchini wakakamatwa.
Labda uende misitu ya Congo.
 
Aliua Kawe Dar es Salaam tarehe 25 Oktoba, 2023 na Kakamatwa rasmi Juzi tarehe 29 Desemba, 2023 huko Mkoani Ruvuma.

Na ili kuonyesha kuwa Intelijensia ya Jeshi la Polisi nchini ni Kali ni kwamba ndani ya Miezi hii Miwili Muuaji Rakesh Kato Mayele ( alias ) Rasta Kato au Rasta Mayele ( Dereva Bajaji Kawe ) alikuwa akiwakimbia / akiwakwepa Polisi kwa Kuhamahama Mikoa ambapo aliishi Mikoa karibia Mitano kabila ya Mbio zake kuishia rasmi Mkoani Ruvuma ( Songea ) ambako ndiko Alikodakiwa / Alikokamatwa.

Namaliza tu kwa kusema kuwa kwa Teknolojia Kubwa iliyoko Tanzania kwa sasa na Intelijensia Mahiri ya Jeshi la Polisi, JWTZ na TISS ukiona umefanya Tukio lolote lile baya cha kufanya haraka sana ambacho nakushauri ni Wewe Kujiua tu ila usijidanganye kuwa hutopatikana kamwe kwa Kigezo cha Kutegemea Waganga wa Kienyeji kama ambavyo alikuwa akifanya huyu Kijana Muuaji Kato aliyemuua Afisa wa JWTZ Kanali Deogratius Muna ( Mtani wangu wa Kinyiramba ) kutokea Mkoa wa Singida.

Hongera sana PT kwa Kumkamata.

Kufahamu mkasa huo, soma: Updates za kifo cha Afande Luteni Kanali Muna aliyeuawa Kawe kwa kuchomwa kisu na dereva bajaji Kato
Naona unawasanifu hao Tiss
 
2013 kwetu tulipata kibarua wa shamba, yule bwana kumbe huko kwao aliua jamaa mwenzie wakiwa kibanda umiza huko Tabora,
Yule bwana alikua mtiifu wa kazi za shamba na kuchunga mifugo yetu,

Alikaa pale kijijini had 2016 akaoa na kuanzisha familia yake, 2019 kuna jamaa mnunua mazao kumbe ni wa huko kijijini kwao na anamfahamu, alivyofika kumuona alihamaki, kakuta mwenzake ana mke na mtoto na nyumba yake, kiufupi ana maisha yake,
Yule jamaa ndo akatusimulia pale home, nakumbuka mzee akamuambia yule mgeni asiseme kwa watu, huwezi amini baada ya muda ndugu wa yule kibarua walikuja kule kijijini, navyoongea maisha yake yako pale kijijini ana fuga ng'ombe na mbuzi, kurudi kwao hataki tena, ila ndugu zake ndo wanamtembelea.
Serikali haishindwi kumtafuta yeyote aliyefanya mauaji ikiamua kamwe, kama utaendelea kubisha basi bisha at your own risk, nimemaliza.

Sent from my CPH2387 using JamiiForums mobile app
 
Usijifaraji kumbuka kisa Cha walio muuwa mzungu Walter mpunga ujangiri mmoja alivuka mpaka kakamatwa Burundi.
Kumbuka tukio la majuzi vijana wadogo wa kiha waliuwa wwnzao kwa sumu wakakimbilia Burundi Waka karibia kukamatwa huko huko kwa ushirikiano wa majeshi ya polisi ndipo wakarudi nchini wakakamatwa.
Labda uende misitu ya Congo.
Na misitu ya Congo tigers hawatakuacha salama.
 
Askari wa bongo vikosi vyote wana skillz za kutosha ila huzitumia tu pale kunapokua na masrahi yao ya kimaokoto au kihisia au masrahi ya serkali ovu ya ccm.
Hawafanyi kazi kutumikia raia hawa chawa wa kijani na manjano.
Kweli tupu maneno yako.

Kinachoumiza zaidi hawa 'mabaka" ambao walikuwa wanapendwa na kuaminiwa na wananchi, nao wamejitumbukiza kwenye shimo la UCHAWA.....wamekuwa wa hovyo haswa.
 
Usijifaraji kumbuka kisa Cha walio muuwa mzungu Walter mpunga ujangiri mmoja alivuka mpaka kakamatwa Burundi.
Kumbuka tukio la majuzi vijana wadogo wa kiha waliuwa wwnzao kwa sumu wakakimbilia Burundi Waka karibia kukamatwa huko huko kwa ushirikiano wa majeshi ya polisi ndipo wakarudi nchini wakakamatwa.
Labda uende misitu ya Congo.
Dah noma, Cha msingi ni kutofanya uhalifu basi.
 
Wewe ndio usingemaliza hata siku Mbili.

Ukishakuwa mhalifu wa kiwango cha muuaji au gaidi simu au chombo chochote cha mawasiliano ni mwiko kutumia.

Usipojiweka jela kwa hiyari yako mwenyewe kwa kujizuia kuwasiliana watakukamata ili wakuweke jela kinguvu.
Kufanya hivyo hakuondoi possibility ya kukamatwa kuna delay tu.

Magaidi hawatumii simu lakini bado wanakamatwa.
 
Tunatakiwa tufahamu kuwa duniani kote mhalifu anayetafutwa (hata mimi na wewe ikitokea ,Mungu aepushe ) hukumbwa na vitu viwili vikuu ambavyo ni :

1) Hofu (Fear): ni hali ya wasiwasi inayompata mtu au mnyama mbele ya mwingine au kingine kisichompendeza au kuhatarisha usalama wake.

2) Woga (Paranoia/ Anxiety) (Naomba nirekebishwe): ni tabia ya kupatwa na hofu kupita kiasi inayokuwa ndani ya binadamu juu ya kitu au vitu fulanifulani.

Hivyo vitu viwili hupelekea kufanya makosa ya kimkakati ambayo vyombo vya dola huvitumia kama faida kwao! Ukiwa na hivyo vitu ni lazima narudia tena ni lazima utafanya makosa.

Moja ya mafunzo ya kijasusi na machache kwa vyombo vya dola ni kukuondolea hivyo vitu vikuu viwili na kukupa vitu vipya! Baada ya kuondolewa hivi vitu huwa wanaweza kuhimili hali zote! Mimi na wewe hatuwezi!

Mfano 1: mwangalie Kikwete na marehemu Magufuli reaction zao kuhusu jambo lolote, utagundua mmoja amekasirika mwingine anatabasamu.

Unaweza kuona huyu aliyekasirika ni jasiri kumbe ni kinyume chake! Mwingine ana hisia mwingine anaigiza hisia!

Mfano 2: Mwangalie Putin na Kim wa Korea Kaskazini, namaanisha kampe taarifa Kim kuwa wanajeshi wako 1000 wamekufa halafu nenda kwa Putin kampe hiyo taarifa!

Nb: 1) Hisia hupelekea kufanya makosa!

Nb 2) Mhalifu siku zote huwa mwoga!

Nb 3) Dola halina hisia ila watu wake wana hisia!

Ni mtazamo wangu!

"The escape man is still human, he is still afraid, Fear becomes paranoia, paranoia ultimately psychosis. I bring this up because in one hundred and forty years, the fundamental mind of the escape man has not changed "- FBI Special Agent Alexander Mahone (Prison Break)
Kumbe kuna tofauti kabisa kati ya hofu na woga?

Basi huwa naamini haya maneno yana maana sawa "hofu, woga, wasiwasi na mashaka".

Sent from my CPH2387 using JamiiForums mobile app
 
Ujinga ni kujifanya unajificha halafu unazima simu na kuwasha au kutupa Line ya simu na kununua mpya afu kuendelea kutumia simu Ile Ile.
Tupa simu tupa line uone kama utadakwa kirahisi. Ingekuwa mm ningekuwa Mogadishu muda huu
Utavukia wapi sasa
 
Kama ana move na simu basi mifumo iliyopo TCRA inasoma exactly simu yake inapokea mawimbi kutoka mnara gani wa simu. Hivyo taarifa hio inatumiwa na polisi (Cyber Crime Unit) kuwasiliana kwa radio na polisi wa eneo hilo kwa ajili ya kumfuatilia muhusika. Hata yule kijana aliywua Rombo akakamatwa Jema Ngorongoro kule ni makosa haya haya muhalifu anayofanya. Kutumia vifaa vya teknolojia.

Kwa nchi zilizoendelea, detection ya movement ya muhalifu inafanyika hata kwa kuangalia manunuzi yake anayofanya (mf credit card, ATM anayotumia/aliyotumia mara ya mwisho), ticket za bus (zipo electronically), camera za barabarani (street camera), CCTV za maeneo maarufu kama alipita hapo n.k. Itoshe kusema tu huyo Rasta alikosa uelewa mdogo sana wa mambo otherwise asingeweza kushikwa maana TZ bado coordination ya hizi aspect ni mbaya.
Kuna yule muuwaji kutoka South Africa na mchumba wake Dr nani sijui walidakwa hotelini Arusha wakila maraha juzi kati hapa mwaka ulioisha jana. Ogopa teknolojia; baanda ya Mungu Mwenyezi; technology is next!
 
Tunatakiwa tufahamu kuwa duniani kote mhalifu anayetafutwa (hata mimi na wewe ikitokea ,Mungu aepushe ) hukumbwa na vitu viwili vikuu ambavyo ni :

1) Hofu (Fear): ni hali ya wasiwasi inayompata mtu au mnyama mbele ya mwingine au kingine kisichompendeza au kuhatarisha usalama wake.

2) Woga (Paranoia/ Anxiety) (Naomba nirekebishwe): ni tabia ya kupatwa na hofu kupita kiasi inayokuwa ndani ya binadamu juu ya kitu au vitu fulanifulani.

Hivyo vitu viwili hupelekea kufanya makosa ya kimkakati ambayo vyombo vya dola huvitumia kama faida kwao! Ukiwa na hivyo vitu ni lazima narudia tena ni lazima utafanya makosa.

Moja ya mafunzo ya kijasusi na machache kwa vyombo vya dola ni kukuondolea hivyo vitu vikuu viwili na kukupa vitu vipya! Baada ya kuondolewa hivi vitu huwa wanaweza kuhimili hali zote! Mimi na wewe hatuwezi!

Mfano 1: mwangalie Kikwete na marehemu Magufuli reaction zao kuhusu jambo lolote, utagundua mmoja amekasirika mwingine anatabasamu.

Unaweza kuona huyu aliyekasirika ni jasiri kumbe ni kinyume chake! Mwingine ana hisia mwingine anaigiza hisia!

Mfano 2: Mwangalie Putin na Kim wa Korea Kaskazini, namaanisha kampe taarifa Kim kuwa wanajeshi wako 1000 wamekufa halafu nenda kwa Putin kampe hiyo taarifa!

Nb: 1) Hisia hupelekea kufanya makosa!

Nb 2) Mhalifu siku zote huwa mwoga!

Nb 3) Dola halina hisia ila watu wake wana hisia!

Ni mtazamo wangu!

"The escape man is still human, he is still afraid, Fear becomes paranoia, paranoia ultimately psychosis. I bring this up because in one hundred and forty years, the fundamental mind of the escape man has not changed "- FBI Special Agent Alexander Mahone (Prison Break)
Season 2 Episode 1
 
Back
Top Bottom