Jana iliibuka story mitandaoni ya Jeshi la Polisi kumkamata Mtanzania Halali akikamua Mafuta bila kuwa na "usajili" yaani vibali, Mafuta ya mawese. Kama kawaida Jeshi letu (ambalo kwa mujibu wa Waziri wake, wengi wao ni failures) hawakumuumiza kichwa Wala kutumia busara, wakaitisha Press na kumsulubu mwekezaji mzawa aliyekua anatafuta ada za watoto wake kwa njia Halali.
Mungu akitaka kukupa kitu sometimes anakupitisha Kwenye majaribio magumu sana, Police bila kujua kuwa kwa kuitisha Press walikua wanamsaidia kumpiga chura Teke. Leo ndugu
Zitto alipost Twitter akimuonba Waziri wa Kilimo Husein Bashe kumsaidia mwekezaji mzawa huyu kujua hatua stahiki za kuboresha kazi yake na hatimae Bashe ameripoti kuwa ameshachukua hatua.
Jambo hili linastahili pongezi sana maana ni Watanzania wengi sana wanaumizwa na Hawa Watawala wadogo wanaojiita miungu Watu wakiongozwa na Jeshi la Polisi, Watendaji, na maafisa wengine wa SERIKALI.
---
Ujumbe wa Zitto Kabwe
Wananchi wanatafuta njia zao za kujipatia kipato. Bwana Halifa Issa anapaswa kusaidiwa kuonyeshwa njia za vibali na sio kukamatwa. Waziri wa Kilimo ndugu
@HusseinBashe na Waziri wa Mambo ya Ndani Bwana Masauni kemeeni mambo haya. Huyu anafanya value addition. Support him
Majibu ya Waziri wa Kilimo, Hussein Bashe
Nashukuru kwa Taarifa hii nimewasiliana na Mh DC wa kibaha nimemuomba amtafute huyu mwananchi na kumsaidia kupitia SIDO na wizara ya kilimo tuna promote “Value addition” through backyard processing hana tofauti na wale wa alizeti wanaouza Barabarani ni Jukumu letu kuwasaidia
View attachment 2086623
View attachment 2086625