Kukamatwa kwa kiwanda bubu cha mafuta ya mawese mkoani Pwani, nawapongeza Zitto na Bashe kwa hatua walizochukua

Kukamatwa kwa kiwanda bubu cha mafuta ya mawese mkoani Pwani, nawapongeza Zitto na Bashe kwa hatua walizochukua

Kumiliki kiwanda bila ya kibali/leseni ni kosa kisheria. Lakini pia kuzalisha bidhaa kiwandani na kuuza pasipo kukagaguliwa na TANZANIA FOOD AND DRUGS AUTHORITY nayo ni kosa kisheria na bidhaa hizo zaweza kuwa ni hatari kwa matumizi ya mwana wa Adamu.

Kwa mantiki hiyo huna sababu ya msingi ya kulilaumu jeshi la polisi. Kwani limetekeleza wajib wake. Bali kumpongeza mwana matukio Zitto na waziri wa kilimo ni jambo jema.

Ningekuona una maana endapo tu ungelisifu jeshi la polisi kwa kumwibua mhusika huo na akapata kusaidiwa na waziri wa kilimo.

Nani anayekagua maandazi yanaouzwa stendi na wamachinga au zile sambusa na mishkaki ya barabarani
 
Kumiliki kiwanda bila ya kibali/leseni ni kosa kisheria. Lakini pia kuzalisha bidhaa kiwandani na kuuza pasipo kukagaguliwa na TANZANIA FOOD AND DRUGS AUTHORITY nayo ni kosa kisheria na bidhaa hizo zaweza kuwa ni hatari kwa matumizi ya mwana wa Adamu.

Kwa mantiki hiyo huna sababu ya msingi ya kulilaumu jeshi la polisi. Kwani limetekeleza wajib wake. Bali kumpongeza mwana matukio Zitto na waziri wa kilimo ni jambo jema.

Ningekuona una maana endapo tu ungelisifu jeshi la polisi kwa kumwibua mhusika huo na akapata kusaidiwa na waziri wa kilimo.
Hivi yale Mafuta ya UPAKO au ya Mwamposa huwa wanayakamata? Wasogee waone!! Na bado jamaa akirudi kwao Kigoma usijekuta afwande akavuliwa vitufe😂🤣😜
 
Yote

Yote uliyoyaandika ninakubaliana nawe isipokua aya ya kulisifu jeshi la polisi,tabia hii sijui itaisha lini hapa nchini why police wakimbilie press kabla ya kufanya uchunguzi kwanza na kujidhihirisha kwanza kosa lililofanyika na kumpeleka mahakamani kwanza?elewa alikua suspect!sio haki kwa polisi to parade someone bila y ushahidi wa kutosha.
Kwa aina hii ya kosa haichukuwi hata nusu saa kwa upande wa polisi kubaini kama mtuhumiwa ana kosa au la. Ni maswali mawili tu majibu yake yanatoa jibu sahihi

1. Unayo lessen ya biashara yako?
2. Unacho Kibali cha TFDA?

Mimi pia sipendelei polisi kutaka umaarufu kupitia media. Utulivu wa uharifu utatoa taswila ya kuwa polisi wanafanya kazi yao. Na siyo kila kitu kimbilia kwenye media ili kupata umaarufu
 
Katika majukumu ingalikuwa vema polisi wakawashirikisha wenye mamlaka na weledi wa kukagua ubora wa chakula na kudhibiti uzalishaji wa bidhaa. Kwa kuwa wao hawakutaka kushirikisha hizo mamlaka husika ndipo linapokuja suala la NIA na DHAMIRA ya Polisi katika huo UKAMATAJI haukuwa sahihi na umejaa MASHAKA. Je wanao WELEDI? Je ni MCHONGO?
Ni vyema tukapeana uelewa kidogo ili kujenga hadhi ya jukwaa hili.

Polisi kukamata mmiliki wa kiwanda hicho sambamba na bidhaa anazozalisha ambazo ni vielezo hawakufanya hata chembe ya kosa.

Kinachofuatia baada ya ukamataji huo ni kuwashirikisha mamlaka husika ambao ni TFDA na mamlaka ya lesseni. Ikibidi na mkemia mkuu wa serikali.
 
Je kuna sehemu yeyote ambayo yule mtoa taarifa wa kipolisi alisema amezihusisha mamlaka husika? Mzee hapa ni MCHONGO ndio uliotalamaki kama wangemalizana BAHARINI hii mambo usingeiona. Namsifu sana yule jamaa. ALINYUTI kama hajui na jamaa WAKAUVABA na MOTO umewawakia. Ndio maana wenye DHAMANA wameamua AACHIWE.
 
Kufuata taratibu na sheria ndio msingi wa afya na usalama wa mlaji

Huyu mtanzania aliyeweza hadi kuwa na kiwanda bila kufuata utaratibu alikua na nia gani? ! Je ni kweli hajui kwamba ni makosa? Ubora wa bidhaa anayozalisha kibiashara ukoje?

Kusema kwamba police wamemuonea sio sawa, binafsi nawapongeza kwa kufanya kazi yao.

Kuendelea kushabikia uvunjifu wa sheria ati sababu alichofanya mtu kina manufaa tutakuja shangaa tunalishwa sumu na kuja kufa au kupata maradhi
Wakati mwingine mambo yanakuzwa bila sababu ya msingi! Ukamuaji wa mafuta ya mawese unaweza kufanyika bila kuwa na kiwanda. Kinachotakiwa ni mapipa ya chuma na jiko la mkaa au kuni na kuanza kuchemsha. Sasa ili polisi wafanikishe nia yao ovu ya kukubambikia kesi watasema hilo jiko ni kiwanda!
 
Kwa hili la mafuta ya kula, kuna haja ya ku-balance the two, kuvunja sheria kwa kuwa na backyard factory na motive ya mwenye kiwanda cha mafuta.

Honestly, kwa level ya RPC mpaka anaenda kwenye media ku-break news wamekamata mtu mwenye kiwanda cha kuchakata mafuta ya mawese, nadhani kuna chembe ya kupungukiwa na weledi wa vijana waliomkamata mpaka mtoa taarifa (RPC).

Watu wengi hawana ajira rasmi na mtu kafikiri kajibana mpaka kupata mtambo na kaanza kuzalisha kwa kuongeza thamani toka raw palm fruits mpaka mafuta. Hii ni effort kubwa na ingekuwa sifa kama RPC angekuwa wa kwanza kuwaita SIDO, TBS wamsaidie kufanya kwa kuzingatia taratibu za ubora ili anachozalisha kisije kuwa na athari kwenye afya za walaji.

Kazi kubwa kuwa Polisi ni kudhibiti uhalifu; na moja ya kazi ya kipepelezi ni kutafiti nia ovu (evil motive); sasa kwa huyu jamaa anazalisha mafuta ya kula, je kulikuwa na evil motive kweli? Sidhani.

TBS, SIDO, TIRDO wamkaa sana ofisini, busara ni kuhamasisha initiatives za uzalishaji wa kuongeza thamani ya raw materials na ni vema pia kuwafuata kule waliko kuliko kusubiria wahusika wawafuate ninyi maofisini.

Bila shaka baada ya hapa, jamaa huyu (mjasiliamali) atalindwa na kupewa ushirikiano. Kiuhalisia, many not all, many gov officials are so slow in ensuring quick change is realized and timely service delivery.

Katika hili, tutegemee bank za uwekezaji kama TIB and TADB wajitokeze kwa kuwa na package ya equipment financing loan and business skill development training kit kwa mtu kama huyu ili azalishe mafuta mengi zaidi kwa modern tech, auze kwa wananchi na kurejesha mkopo.
 
Hawa wata set precedence! Vyakula na dawa sio kitu cha kufanyia mchezo au majaribio.

Wanaoshabikia wala hawatumii hayo mawese, wao wanafurahia kuona sheria zilizowekwa hazifuatwi na mtu mwingine lakini wao wanazifuata😅😅😅
 
Jana iliibuka story mitandaoni ya Jeshi la Polisi kumkamata Mtanzania Halali akikamua Mafuta bila kuwa na "usajili" yaani vibali, Mafuta ya mawese. Kama kawaida Jeshi letu (ambalo kwa mujibu wa Waziri wake, wengi wao ni failures) hawakumuumiza kichwa Wala kutumia busara, wakaitisha Press na kumsulubu mwekezaji mzawa aliyekua anatafuta ada za watoto wake kwa njia Halali.

Mungu akitaka kukupa kitu sometimes anakupitisha Kwenye majaribio magumu sana, Police bila kujua kuwa kwa kuitisha Press walikua wanamsaidia kumpiga chura Teke. Leo ndugu Zitto alipost Twitter akimuonba Waziri wa Kilimo Husein Bashe kumsaidia mwekezaji mzawa huyu kujua hatua stahiki za kuboresha kazi yake na hatimae Bashe ameripoti kuwa ameshachukua hatua.

Jambo hili linastahili pongezi sana maana ni Watanzania wengi sana wanaumizwa na Hawa Watawala wadogo wanaojiita miungu Watu wakiongozwa na Jeshi la Polisi, Watendaji, na maafisa wengine wa SERIKALI.

---

Ujumbe wa Zitto Kabwe

Wananchi wanatafuta njia zao za kujipatia kipato. Bwana Halifa Issa anapaswa kusaidiwa kuonyeshwa njia za vibali na sio kukamatwa. Waziri wa Kilimo ndugu @HusseinBashe na Waziri wa Mambo ya Ndani Bwana Masauni kemeeni mambo haya. Huyu anafanya value addition. Support him

Majibu ya Waziri wa Kilimo, Hussein Bashe

Nashukuru kwa Taarifa hii nimewasiliana na Mh DC wa kibaha nimemuomba amtafute huyu mwananchi na kumsaidia kupitia SIDO na wizara ya kilimo tuna promote “Value addition” through backyard processing hana tofauti na wale wa alizeti wanaouza Barabarani ni Jukumu letu kuwasaidia

View attachment 2086623
View attachment 2086625
Heko zitto na bashe mumefanya jambo zuri kwa uchumi wa wananchi. Huyu nina hakika akisaidiwa ataweza kuongeza ajira kwa kua na kiwanda mkakati cha kuigwa.
 
Katika majukumu ingalikuwa vema polisi wakawashirikisha wenye mamlaka na weledi wa kukagua ubora wa chakula na kudhibiti uzalishaji wa bidhaa. Kwa kuwa wao hawakutaka kushirikisha hizo mamlaka husika ndipo linapokuja suala la NIA na DHAMIRA ya Polisi katika huo UKAMATAJI haukuwa sahihi na umejaa MASHAKA. Je wanao WELEDI? Je ni MCHONGO?

Unayajua majukumu ya police katika matukio kama haya? Unajua kwanini vibali vya uendeshaji wa shughuli mbalimbali hubandikwa kwenye eneo la wazi la office?
Huo weledi unaoungolea wewe ni upi labda!?
Au unataka kutulazimisha kwamba mwenye kiwanda ameonewa??

Kuna wakati tuweke ushabiki usiokua na maslahi kwetu kando turudi kusimamia ukweli! Na ukweli ni kwamba huwezi fungua kiwanda ukatengeneza bidhaa na kuzisambaza kwa wananchi zitumike bila kufuata taratibu

Au Mnataka waachwe halafu kesho tuanze kurusha lawama hawakuwajibika!?
 
Siyo kazi ya Polisi hiyo!

Unafikiri maofisa wa TBS TFDA TRA huwa hawafanyi kazi na maofisa wa POLISI!?
Au wamekiuka utaratibu uliowawekea wewe?

Btw kwenye maswala kama haya hata wewe mwananchi kama mdau muhimu sana unazo taratibu zinazokuwezesha kureport wavunjifu wa sheria kama hawa kwa vyombo husika kwa usalama wetu sote
 
Unayajua majukumu ya police katika matukio kama haya? Unajua kwanini vibali vya uendeshaji wa shughuli mbalimbali hubandikwa kwenye eneo la wazi la office?
Huo weledi unaoungolea wewe ni upi labda!?
Au unataka kutulazimisha kwamba mwenye kiwanda ameonewa??

Kuna wakati tuweke ushabiki usiokua na maslahi kwetu kando turudi kusimamia ukweli! Na ukweli ni kwamba huwezi fungua kiwanda ukatengeneza bidhaa na kuzisambaza kwa wananchi zitumike bila kufuata taratibu

Au Mnataka waachwe halafu kesho tuanze kurusha lawama hawakuwajibika!?
Tukio linaeleweka sana. Hebu tafakari je mtuhumiwa amepelekwa MAHAKAMANI? Je watakapofika mahakami wataongozwa na sheria IPI? Je polisi wanaoweledi wa kurtoa USHAHIDI kwenye tukio kama hilo? Usishabikie pasi kuelewa WIGO na UKOMO wa majukumu ya polisi. Vinginevyo yako POTOFU na uelekeo wa polisi kwenye kesi kama hizi, nasikitika kukwambia tunashida sana ya UELEWA kwenye sheria. Hivi huoni hiki ni KITUKO? N laiti polisi wangalikuwa wanafunguliwa kesi za madai kwa makosa ya KUBAMBIKA na MICHONGO hii nchi ingetangazwa MUFLISI.
 
Back
Top Bottom