Kukamatwa kwa kiwanda bubu cha mafuta ya mawese mkoani Pwani, nawapongeza Zitto na Bashe kwa hatua walizochukua

Kukamatwa kwa kiwanda bubu cha mafuta ya mawese mkoani Pwani, nawapongeza Zitto na Bashe kwa hatua walizochukua

Tukio linaeleweka sana. Hebu tafakari je mtuhumiwa amepelekwa MAHAKAMANI? Je watakapofika mahakami wataongozwa na sheria IPI? Je polisi wanaoweledi wa kurtoa USHAHIDI kwenye tukio kama hilo? Usishabikie pasi kuelewa WIGO na UKOMO wa majukumu ya polisi. Vinginevyo yako POTOFU na uelekeo wa polisi kwenye kesi kama hizi, nasikitika kukwambia tunashida sana ya UELEWA kwenye sheria. Hivi huoni hiki ni KITUKO? N laiti polisi wangalikuwa wanafunguliwa kesi za madai kwa makosa ya KUBAMBIKA na MICHONGO hii nchi ingetangazwa MUFLISI.
Huyu usibishane nae ndio alivyo
 
Wakati mwingine mambo yanakuzwa bila sababu ya msingi! Ukamuaji wa mafuta ya mawese unaweza kufanyika bila kuwa na kiwanda. Kinachotakiwa ni mapipa ya chuma na jiko la mkaa au kuni na kuanza kuchemsha. Sasa ili polisi wafanikishe nia yao ovu ya kukubambikia kesi watasema hilo jiko ni kiwanda!

Shida sio ukamuaji wa mawese. Sababu hata mimi nyumbani kwangu nakamua alizeti na kupata mafuta
Shida ni kuzalisha bidhaa kwa kiwango kikubwa na kuulisha umma bila kuzingatia taratibu za uzalishaji na usambazaji unaomlinda mlaji, mzalishaji na taifa
 
Nani anayekagua maandazi yanaouzwa stendi na wamachinga au zile sambusa na mishkaki ya barabarani
Ile Kazi ya Bwana na bibi afya lakini awafanyi thus wanawauzia watz Vyakula kwenye magazeti na vyombo vya plastic vyote hivi usababisha kansa.
Wino ni sumu plastic ni sumu.
 
Polisi wamefanya kazi yao kwa sababu utaratibu wa kufanya shughuli kama hiyo upo na unapaswa ufuatwe.

Lazima akamatwe ili ahojiwe kuna uwezekano anafahamu kabisa hiki nachofanya lazima nipitie hatua hizi na hizi ila kwa ubishi wa kiafrica akaacha kufuata hizo taratibu.

Unazalisha chakula tena kwa kiwango kikubwa hakuna mamlaka yoyote inajua unachoweka Au kufanya kwenye hiyo product yako, mazingira ya uzalishaji labda sio safi na salama. Hatuwezi kuishi bila utaratibu hata kama ni masikini.

Ikitokea hayo mafuta yakawa na madhara kwa watu mtakuja hapa mseme mamlaka kazi yao ni kuifatilia chadema tu haina muda na Afya za watanzania.
 
Polisi wamefanya kazi yao kwa sababu utaratibu wa kufanya shughuli kama hiyo upo na unapaswa ufuatwe.

Unazalisha chakula tena kwa kiwango kikubwa hakuna mamlaka yoyote inajua unachoweka Au kufanya kwenye hiyo product yako. Hatuwezi kuishi bila utaratibu hata kama ni masikini.
Umesoma majibu ya Waziri mwenye dhamana?
 
Tukio linaeleweka sana. Hebu tafakari je mtuhumiwa amepelekwa MAHAKAMANI? Je watakapofika mahakami wataongozwa na sheria IPI? Je polisi wanaoweledi wa kurtoa USHAHIDI kwenye tukio kama hilo? Usishabikie pasi kuelewa WIGO na UKOMO wa majukumu ya polisi. Vinginevyo yako POTOFU na uelekeo wa polisi kwenye kesi kama hizi, nasikitika kukwambia tunashida sana ya UELEWA kwenye sheria. Hivi huoni hiki ni KITUKO? N laiti polisi wangalikuwa wanafunguliwa kesi za madai kwa makosa ya KUBAMBIKA na MICHONGO hii nchi ingetangazwa MUFLISI.

Wewe unajua wigo na ukomo wa police unaishiaga wapi😅😅😅
Nenda kawaulize TFDA TRA BRELA TBS wakueleze vizuri vile wanafanya kazi kabla ya kuwapangia POLISI unachotaka wewe.
Taratibu zipo aliyekamatwa amevunja sheria sasa sijui mnachoshabikia nini 🙄🙄
 
Shida sio ukamuaji wa mawese. Sababu hata mimi nyumbani kwangu nakamua alizeti na kupata mafuta
Shida ni kuzalisha bidhaa kwa kiwango kikubwa na kuulisha umma bila kuzingatia taratibu za uzalishaji na usambazaji unaomlinda mlaji, mzalishaji na taifa
Ndugu yangu, hizo dumu hata 20 hazifiki.

Kuna peanut butter na crisps zinauzwa nyingi tu supermarket wala hazina TBS; hatukatai makpsa ya kuzalisha mafuta bila kuzingiatia vibali; huyu wala hazalishi kibiashara; hiyo anazalisha ni subsistence.
Investigation ifanyike kwa kuona intent ya huyu mtu na asaidiwe.

Bashe kafanya jambo la maana sana
 
Mwambie asome majibu ya Waziri mwenye dhamana, sasa kama mtu anapingana na Waziri wake sisi tufanyeje
 
Shida sio ukamuaji wa mawese. Sababu hata mimi nyumbani kwangu nakamua alizeti na kupata mafuta
Shida ni kuzalisha bidhaa kwa kiwango kikubwa na kuulisha umma bila kuzingatia taratibu za uzalishaji na usambazaji unaomlinda mlaji, mzalishaji na taifa
Kwani wewe huuzi hayo mafuta? Kutoka Shinyanga, Singida, Dodoma hadi Morogoro mafuta ya alizeti yanauzwa barabarani yakiwa ndani ya chupa za maji, vigaloni na vidumu, je ukamuaji wake unasimamiwa na mamlaka ipi ya serikali?
 
Wanaoshabikia wala hawatumii hayo mawese, wao wanafurahia kuona sheria zilizowekwa hazifuatwi na mtu mwingine lakini wao wanazifuata[emoji28][emoji28][emoji28]
Je yale mafuta ya alizeti yanayouzwa huko mastand yamekaguliwa na tbs pamoja na TFDA au mnaongea tuu,hayo mavyakula yanayouzwa huko stand huwa yamekaguliwa na hizo taasisi mnazozisemea ?
 
Jana iliibuka story mitandaoni ya Jeshi la Polisi kumkamata Mtanzania Halali akikamua Mafuta bila kuwa na "usajili" yaani vibali, Mafuta ya mawese. Kama kawaida Jeshi letu (ambalo kwa mujibu wa Waziri wake, wengi wao ni failures) hawakumuumiza kichwa Wala kutumia busara, wakaitisha Press na kumsulubu mwekezaji mzawa aliyekua anatafuta ada za watoto wake kwa njia Halali.

Mungu akitaka kukupa kitu sometimes anakupitisha Kwenye majaribio magumu sana, Police bila kujua kuwa kwa kuitisha Press walikua wanamsaidia kumpiga chura Teke. Leo ndugu Zitto alipost Twitter akimuonba Waziri wa Kilimo Husein Bashe kumsaidia mwekezaji mzawa huyu kujua hatua stahiki za kuboresha kazi yake na hatimae Bashe ameripoti kuwa ameshachukua hatua.

Jambo hili linastahili pongezi sana maana ni Watanzania wengi sana wanaumizwa na Hawa Watawala wadogo wanaojiita miungu Watu wakiongozwa na Jeshi la Polisi, Watendaji, na maafisa wengine wa SERIKALI.

---

Ujumbe wa Zitto Kabwe

Wananchi wanatafuta njia zao za kujipatia kipato. Bwana Halifa Issa anapaswa kusaidiwa kuonyeshwa njia za vibali na sio kukamatwa. Waziri wa Kilimo ndugu @HusseinBashe na Waziri wa Mambo ya Ndani Bwana Masauni kemeeni mambo haya. Huyu anafanya value addition. Support him

Majibu ya Waziri wa Kilimo, Hussein Bashe

Nashukuru kwa Taarifa hii nimewasiliana na Mh DC wa kibaha nimemuomba amtafute huyu mwananchi na kumsaidia kupitia SIDO na wizara ya kilimo tuna promote “Value addition” through backyard processing hana tofauti na wale wa alizeti wanaouza Barabarani ni Jukumu letu kuwasaidia

View attachment 2086623
View attachment 2086625
Kuna baahi ya mambo Nchi hii yanatoa hasira badala wasifu ubunufu wake na weledi alionao eti wanawnda.kumukamata cha msingi hawa vijana wasaidiwe
 
Kwani wewe huuzi hayo mafuta? Kutoka Shinyanga, Singida, Dodoma hadi Morogoro mafuta ya alizeti yanauzwa barabarani yakiwa ndani ya chupa za maji, vigaloni na vidumu, je ukamuaji wake unasimamiwa na mamlaka ipi ya serikali?

Je yale mafuta ya alizeti yanayouzwa huko mastand yamekaguliwa na tbs pamoja na TFDA au mnaongea tuu,hayo mavyakula yanayouzwa huko stand huwa yamekaguliwa na hizo taasisi mnazozisemea ?

Ndio mimi siuzi, na najua nitakapotaka kuuza lazima niruhusu mamlaka husika kunisimamia nisije ua watu.

Chochote kinachofanyika nje ya taratibu ni kosa na hakuna haja ya kutetea makosa

Kama serikali inavyokamata Gongo inayoitwa konyagi, iendelee kukamata hata mafuta, nyama, samaki vinavyouziwa walaji bila kuthibitika ubora wake

Hatuwezi kusema kama kuna kosa linafanyika pale basi na hapa tufanye makosa. Huo utakua upumbavu wa kiwango cha juu sana kwetu
 
Duh kumbe nabishana na kitufe cha Mpapure

Nenda kale mawese uache kubishana....
Yaani mtu mzima unayejua kusoma na kuandika kabisa unashabikia kula bidhaa zosizopimwa wala kujulikana viwango vyake vya ubora!?
Huzuni sana kwakweli🙄
 
Back
Top Bottom