Kukamatwa kwa kiwanda bubu cha mafuta ya mawese mkoani Pwani, nawapongeza Zitto na Bashe kwa hatua walizochukua

Kukamatwa kwa kiwanda bubu cha mafuta ya mawese mkoani Pwani, nawapongeza Zitto na Bashe kwa hatua walizochukua

Jamani, hivi ni kweli tunatetea uhaqlifu? Hivi hiyo bidhaa ikiwadhuru wananchi mtamlaumu nani. Hivi kweli tumefikia mahali pa kuchagua sheria zipi zifuatwe na zipi zipuuzwe. Tutakuwa tunajenga taifa la namna gani? Ni afadhali mtu awe mkweli kuliko huyu aliekyuwa anatengeneza mafuta akiuza kutumia nembo za viwanda vingine. Huyo Zitto sasa hivi amekuwa irrelevant ndiyo maana anarukia vitu ambavyo yeye kama kiongozi wa kitaifa asingetakiwa. Anajikweza tu, but he is done.
Sio kutetea uhalifu,
Kwa kifupi, Sera ya viwanda ingekuja na malengo yanayohesabika na kufikika.
Mfano in three years tufungue viwanda 100,000 vya mafuta (mawese, Karanga, alizeti n.k) vyenye uwezo wa kuprocess tani 1000 each. Then incentives process nzima, kuanzia Kwa mkulima mpaka mwisho, after 5yrs ndo Kodi zao zirudi

Kwa hesabu hiyo suala la soko la mkulima, bei Kwa mlaji, ajira Kwa vijana yangekuwa solved Kwa mpigo.

Then ukimaliza mafuta unakuja kwenye sukari, unga wa ngano, unga wa ugali, ulezi, juices, maziwa n.k

In ten years unakuta unaviwanda visivopungua 2M vinavotoa ajira rasmi Kwa atleast 5M people.

Then suala la ajira na bei Kwa mlaji au mkulima inakuwa umelimaliza
 
ila bashe akitoa viboriti na vibanzi vidogo vidogo vya siasa chafu chafu, kwa kweli atakuwa kiongozi mzuri ndani ya li-chama chakavu la CCM!
Mama alifanya chaguo sahihi kunfanya huyu Bwana Waziri kamili.
 
Kumiliki kiwanda bila ya kibali/leseni ni kosa kisheria. Lakini pia kuzalisha bidhaa kiwandani na kuuza pasipo kukagaguliwa na TANZANIA FOOD AND DRUGS AUTHORITY nayo ni kosa kisheria na bidhaa hizo zaweza kuwa ni hatari kwa matumizi ya mwana wa Adamu.

Kwa mantiki hiyo huna sababu ya msingi ya kulilaumu jeshi la polisi. Kwani limetekeleza wajib wake. Bali kumpongeza mwana matukio Zitto na waziri wa kilimo ni jambo jema.

Ningekuona una maana endapo tu ungelisifu jeshi la polisi kwa kumwibua mhusika huo na akapata kusaidiwa na waziri wa kilimo.
TFDA sasa ni TMDA. Issues zote za food zinafanywa na TBS. Huyo mjasiriamali angesaidiwa, ujasiriamali sio kitoto.
 
Kumiliki kiwanda bila ya kibali/leseni ni kosa kisheria. Lakini pia kuzalisha bidhaa kiwandani na kuuza pasipo kukagaguliwa na TANZANIA FOOD AND DRUGS AUTHORITY nayo ni kosa kisheria na bidhaa hizo zaweza kuwa ni hatari kwa matumizi ya mwana wa Adamu.

Kwa mantiki hiyo huna sababu ya msingi ya kulilaumu jeshi la polisi. Kwani limetekeleza wajib wake. Bali kumpongeza mwana matukio Zitto na waziri wa kilimo ni jambo jema.

Ningekuona una maana endapo tu ungelisifu jeshi la polisi kwa kumwibua mhusika huo na akapata kusaidiwa na waziri wa kilimo.
Sasa kuna huyu mama hawa hapa mtaani ana kiwanda bubu cha kuchakata maandazi,na hajakaguliwa na tfda,sijui nimnokolee?
 
Yaani niliiangalia jana, nikamuomba Mungu, atuepushe na hili genge la mapolisi wasio jua taratibu.
Nika waza mbali zaidi kwamba huyu mjasirilia mali alikataa kuwapa rushwa.

Nyie si ndio mlikuwa mnailalamikia serikali iliyopita kwa kutozingatia sheria na taratibu? Sasa kwanini mnatete uhalifu? Huyu ametengeneza kiwanda bubu na ni kinyume na sheria anatakiwa kufikishwa mahakamani!

Lazima tukubaliane kabisa kwa sasa tusitumie sheria bali busara maana kuna mwingine ataanza kutengeneza konyagi,kutengeneza Mo energy halafu tujiulize nao tutatumia sheria au busara?

Tusitafute kick za kisiasa lazima tujue nini kinasababisha watu wanafungua viwanda bubu? Lazima tujue wanakwama wapi? Maana inawezekana lengo ni kukwepa kodi tuu na huu ni uhalifu kama uhalifu mwingine! Kama shida ni kupata leseni,kodi kubwa,eneo la kufanyia kazi?

Hii style ya kutumia busara sio suluhu
 
Polisi wanapokosa shughuli hubuni njia za ajabu na matatizo yasiyowahusu. Wanatakiwa waelewe ukomo wa majukumu yao, au ndio ile MICHONGO?
Mojawapo wa kazi ya Jeshi la Polisi ni kuzuia utendekaji wa makosa ya jinai. Kuendesha kiwanda bila usajili huku kikizalisha bidhaa za kula bila ukaguzi wowote ni uhalifu katika Sheria zetu. Hivyo polisi walikuwa sawa kumkamata. Hoja ya msingi ni tuwe na utaratibu wa kuwajengea uwezo wawekezaji wadogo na wa kati katika masuala ya masoko na sheria.
 
Nakushukuru sana mleta taarifa, Pia nampongeza huyo Bwana Halifa Issa kwa ubunifu.
Kibaha mawese ni mengi sana yanaishia kuliwa na ngedere,naomba serikali imwezeshe huyo bwana ili watu wapate sehemu ya kuuza bidhaa hii na pia wengine wapate ajira. Polisi walitakiwa wawatafute watu wanaohusika na mambo ya TBS au TFDA kama waliona atahatarisha afya za watu,badala ya wao kwenda kukamata kama wanavyokamata bangi na gongo.

Hili lisipokemewa kuna siku tutawakuta wanapita madukani wenyewe kukamata bidhaa feki madukani.
kwa mtizamo wangu si kazi yao .
Pia majirani wa huyo ndugu wajitathimini,wamesukumwa na wivu,wakidhani wamemuharibia
kumbe wamempaisha. Fitina na majungu hazilipi ndugu zangu. Kesho mtu akiwa anakanda chapati kwa wingi na kuuza naye atarepotiwa,hivi tunataka watu wafanye kazi gani?
 
Mojawapo wa kazi ya Jeshi la Polisi ni kuzuia utendekaji wa makosa ya jinai. Kuendesha kiwanda bila usajili huku kikizalisha bidhaa za kula bila ukaguzi wowote ni uhalifu katika Sheria zetu. Hivyo polisi walikuwa sawa kumkamata. Hoja ya msingi ni tuwe na utaratibu wa kuwajengea uwezo wawekezaji wadogo na wa kati katika masuala ya masoko na sheria.
Hivi nini maana ya kiwanda?
hayo madumu na mawese ndo kiwanda hicho? mbona sioni mashine?
Leo hii kuna wamama wengi wanatengeneza batiki,kumi,n.k nyumbani kwao
je nao wakamatwe? nenda kigoma uone watu wanavyokamua mafuta ya mawese nyumbani
sasa huyu mkigoma kuja kuyakamua kibaha imekuwa nongwa?

Utakuta wakati anafuatwa huyo mjasilia mali wamepitwa watu kijiweni rundo,
Hivi huko huko kibaha, sehemu zote wanaouza matofari ya kutengenezwa na mashine nao wana usajiri?
Kama tumeamua kujitegemea,lazima tujitathimini. Kama kuna sheria za kuzuia mtu kujiongeza kwa
kutumia raslimali zinazomzunguka,hizo ndo za kupelekwa bungeni kwa hati ya dharura ili zirekebishwe.
 
Kumiliki kiwanda bila ya kibali/leseni ni kosa kisheria. Lakini pia kuzalisha bidhaa kiwandani na kuuza pasipo kukagaguliwa na TANZANIA FOOD AND DRUGS AUTHORITY nayo ni kosa kisheria na bidhaa hizo zaweza kuwa ni hatari kwa matumizi ya mwana wa Adamu.

Kwa mantiki hiyo huna sababu ya msingi ya kulilaumu jeshi la polisi. Kwani limetekeleza wajib wake. Bali kumpongeza mwana matukio Zitto na waziri wa kilimo ni jambo jema.

Ningekuona una maana endapo tu ungelisifu jeshi la polisi kwa kumwibua mhusika huo na akapata kusaidiwa na waziri wa kilimo.
Mawazo ya kidwanzi sana haya, na ya watu wenye roho mbaya. Ukienda Kigoma kule Uvinza ndani ndani hivyo viwanda vidogo vya kusindika mawese ni vingi sana, kama ambavyo Kuna viwanda vidogo dogo vingi tuu vya kukamua alizeti. Hao polisi walitakuwa kumuelekeza ofisi husika apate vibali na aendelee na uzalishaji. Kumbuka bado hali ya upatikanaji wa mafuta nchini ni tete na bei iko juu, sasa badala ya kumuunga mkono kwa kumuelekeza eti polisi wanakimnikia kumkata na kumtoa kwenye media.
 
Hii tabia ya serikali na vyombo vya dola kuzuia, kudhibiti na kukamata wananchi wanaofanya ubunifu kwa kuongeza thamani au kutengeneza bidhaa inatakiwa ibadilishwe kwa kuwa na mtazamo chanya.
Uzuiaji, udhibiti na ukamataji huu ni uendelezaji wa fikra za kimasikini na rushwa.
Ili taifa liendelee hii tabia lazima ikome.
Pongezi kwa Waheshimiwa Waziri na Zito.
Sahihi kabisa.
 
Kufuata taratibu na sheria ndio msingi wa afya na usalama wa mlaji

Huyu mtanzania aliyeweza hadi kuwa na kiwanda bila kufuata utaratibu alikua na nia gani? ! Je ni kweli hajui kwamba ni makosa? Ubora wa bidhaa anayozalisha kibiashara ukoje?

Kusema kwamba police wamemuonea sio sawa, binafsi nawapongeza kwa kufanya kazi yao.

Kuendelea kushabikia uvunjifu wa sheria ati sababu alichofanya mtu kina manufaa tutakuja shangaa tunalishwa sumu na kuja kufa au kupata maradhi
Wewe unajua huo mchakato wa kufuata ili kufungua kakiwanda?? Viwanda vidogo vya mawese kule Kigoma ni vingi sana huko vijijini, nani anavikagua na kujua ubora wa mafuta? Kuna watu kibao wanakamua mafuta ya alizeti nani anakagua ubora? Kuna mashine kibao za kusaga unga na kukoboa Mchele nani anakagua ubora?? Haya Kuna mamalishe kila kona hapa nchini nani huwakagua kuona ubora wa chakula wanachopika?? Haya hawa polisi wamesomea Food science kujua ubora wa hayo mafuta yansyokamuliwa??
 
Jeshi la Polisi Mkoa wa Pwani limefanya msako mkali na kufanikiwa kumkamata mtu mmoja aitwaye Halifa Issa (42) mkazi wa Kongowe Wilayani Kibaha kwa kosa la kumiliki na kuendesha kiwanda bubu cha kuchakata mafuta ya mawese bila ya kuwa na kibali kinyume na sheria.
Wao ni kama robot, wanachojua ni 'kufanya msako mkali' na 'kukamata' tuu!

Jeshi letu (ambalo kwa mujibu wa Waziri wake, wengi wao ni failures)
Siyo wengi wao, ni woote!
 
Yaani niliiangalia jana, nikamuomba Mungu, atuepushe na hili genge la mapolisi wasio jua taratibu.
Nika waza mbali zaidi kwamba huyu mjasirilia mali alikataa kuwapa rushwa.
Ha ha ha!
Wankyo mbn huwa madhubuti sana hapo aliingizwa na nani mkenge
 
Back
Top Bottom