Frustration
JF-Expert Member
- Jan 30, 2018
- 3,134
- 4,124
Habarini za Asubuhi Watanzania wenzangu, BBC wameripoti kupatikanika kwa kiongozi wa waasi ambaye ni raia wa Tanzania.
Vikosi vya jeshi la Msumbiji vinasema kuwa vimemkamata kiongozi wa kijihadi, raia wa Tanzania, katika wilaya ya Nangade kaskazini mwa jimbo la Cabo Delgado.
Kiongozi huyo mwenye umri wa miaka 39, anayejulikana kama Ali, alikamatwa pamoja na wanamgambo wengine wa Kiislamu sita wenye uhusiano na kundi la Islamic State, maafisa wa kijeshi wameeleza.
Amesema alikuwa mmoja wa viongozi wa wanamgambo ambao kazi yao ilikuwa kuajiri wapiganaji na kutekeleza mashambulizi ya moja kwa moja.
Kukamatwa kwake kunakuja huku kukiwa na hali mbaya ya usalama katika wilaya hiyo, na mfululizo wa mashambulizi ya wanajihadi katika siku za hivi karibuni.