Serikali ilipotumia nguvu kupambana na huu ugaidi kule kibiti,kama kawaida wanasiasa wa upinzani walilitumia tukio lile kama agenda ya kutafutia kick za kisiasa.
Tulifikia mahali Polisi wanavamiwa vituoni mchana kweupe.
Askari wanavamiwa kwenye vizuizi mchana kweupe na kuuwawa kama kuku.
Tukafikia mahali kuwa mwenyekiti wa serikali ya kijiji huko kibiti ni kosa na unauwawa.
Serikali ilipolivalia njuga hili kundi na kufanikiwa kulidhibiti ndio likatimkia huko Mozambique[emoji1174].
Tanzania [emoji1241] kila kitu tunapiga domo, kila kitu ni ujuaji.
Kwa hili tukio kuna la kujifunza hapo kwa jamii yetu.
Na sijui kwa nini Media za Tanzania [emoji1241] zinakuwa na umbeya badala ya kutuletea habari.
Wao wanakaa kudandia lift kwenye magari ya wakubwa kwenda kuwajenga kisiasa kwa kupewa vibahasha vya khaki.
Kisha taarifa za habari zinajaa siasa tupu.
Makonngamano, Warsha, Uzinduzi, Uteuzi na kisha Migogoro ya wakulima na wafugaji.
Hatuoni media kwa mfano ikimtafuta waziri wa Nishati na kumuweka Interview atuambie sababu ya kuzuka ghafla kwa tatizo la umeme nchini?
Lini na nini hatma yake?
Na vitu vingine kama hivyo vyenye kuigusa jamii.
MEDIA Tanzania [emoji1241] ni kanjanja tupu 75%.
Huko online media nako TCRA imepakalia kimya huku kukiwa na madudu tupu.
Wao TCRA wanamuona Polepole tu.