Kukamatwa kwa Mtanzania Kiongozi wa Waasi nchini Msumbiji: Kwanini hakuripotiwi na Vyombo vyetu?

Kukamatwa kwa Mtanzania Kiongozi wa Waasi nchini Msumbiji: Kwanini hakuripotiwi na Vyombo vyetu?

Mwenzao ana kesi hapa nchini, akina kibatala wanajitahidi kumnasua, halafu habari za maendeleo zimekuwa nyingi, nafasi katika vyombo vya habari zimejaa
Serikali imesema watalii waje tu Tanzania hakuna uhalifu wa aina yoyote
 
Habarini za Asubuhi Watanzania wenzangu, BBC wameripoti kupatikanika kwa kiongozi wa waasi ambaye ni raia wa Tanzania. Vikosi vya jeshi la Msumbiji vinasema kuwa vimemkamata kiongozi wa kijihadi, raia wa Tanzania, katika wilaya ya Nangade kaskazini mwa jimbo la Cabo Delgado...
Duh.
 
Bila picha ni uzushi! BBC siyo wa kuaminiwa kivile!
ALI wapo wangapi duniani? KIPI kinathibitisha ni mtanzania??
Hii ni tetesi tu
 
Waandishi wetu wa habari simpaka watumiwe usafiri hata wa daladala ndio waende sehemu ya tukio?
Kumbuka yaliyotokea Mwanza wiki ya jana
Kwani Msumbiji hakuna waandishi wa habari wanaoendana nao?
 
Bila picha ni uzushi! BBC siyo wa kuaminiwa kivile!
ALI wapo wangapi duniani? KIPI kinathibitisha ni mtanzania??
Hii ni tetesi tu
Waliosema Ali ni mtanzania sio BBC bali ni jeshi la MSUMBIJI, serikali yetu inabidi ifuatilie kama kweli ni Mtanzania kweli. Kama ni mtanzania kweli anatoka mkoa gani, familia gani ma ukoo gani? TERRORISM is not Tourism as Tanzanian police knows.
 
Hawakupaswa kutangaza, huo ni uharibifu wa masuala ya kiintellijinsia, hapo ni kama wamewapa alert wenzake na Ali, kuwa kimeumana Ali yupo mikononi mwa vyombo, atakavyoteswa atawataja woteee!

Ndiyo maana nasema huo ni uzushi Tu!
 
Back
Top Bottom