Kukamilika kwa bwawa la Mwl Nyerere kwapeleka kilio kwa mafisadi, Kwenye ukame huu wangewapiga watanzania mabilioni ya pesa

Maswa Yetu

Senior Member
Joined
Mar 18, 2023
Posts
155
Reaction score
217
Watanzania wazalendo kwa nchi yao wanajiuliza kwa jinsi jua lilivyokali mwaka huu hivi ingekuwaje mgao wa umeme kama Hayati Magufuli asingejenga bwawa la umeme la mwl Nyerere?.
Ni majenereta mangapi yangeingizwa? Zingezaliwa Richmond ngapi?
Mwaka huu mvua ni chache nchi nzima na jua linatandika kwelikweli kiasi kwamba wakulima wamekosa mazao yao kwa kukauka shambani, lakini bado mafisadi yanaona aibu kutangaza mgao wa umeme kwa sababu wanaogopa watawaambia nini Watanzania kwa sababu wanajua bwawa lao la umeme walilojengewa na Rais wa wanyonge limekamilika na linauwezo wa kutoa megawati 2115.
Mafisadi kwa vikao vyao yanajiuliza sasa tutakula wapi? Na yanapofikia hiyo hatua humlaani Hayati Magufuli kwa kuanzisha ujenzi wa bwawa hilo na yakimaliza yanamlaani pia Rais Samia kwa kukubali kumalizia miradi yote iliyoachwa na Magufuli ikiwemo hilo bwawa la umeme.
Matarajio ya mafisadi ilikuwa ni kwamba pale tu Magufuli alipofariki na ujenzi wa bwawa ungeishia hapo.
 
Mbona umeme wenyewe wanasema wanaukata kwa siku tano kuanzia trh,sita. Hili bwawa linafanya kazi gani?
 
Mafisadi hawashindwi na kitu.

Kwa sasa Wanaona aibu kuleta figisu sababu waarabu bado wapo rufiji wanamalizia kazi ya ujenzi wa bwawa. Bado hawajakabidhi rasmi kwa tanesco.


Waarabu wakishaondoka mafisadi wataanza sarakasi zao Bwawa watalikorokochoa hilo ili lisizalishe umeme. Waanze kuleta kampuni zao za gesi za ujanja ujanja waanze kupiga capacity charges.

Maji watayafungulia yamwagike yote yaishe bwawa lishindwe kuzalisha umeme ama wataweka vilipukizi vya chini kwa chini bwawa lijae matope chini kwa chini
 
Mama kazia hapo hapo,unacheka huku unawafinya...
 
Watanzania tuko macho, tutanyooka na Samia
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…