Pfizer
JF-Expert Member
- Mar 25, 2021
- 819
- 1,093
KUKAMILIKA kwa mradi wa ujenzi wa meli nne kubwa za mizigo katika Bandari ya Karema ni fursa kwa wananchi wa mikoa inayopitiwa na Ziwa Tanganyika ya Rukwa, Katavi, Kigoma na kuongeza kipato cha kaya na Taifa.
Ujenzi wa meli hizo ulianza Aprili 2025 na ukitarajiwa kukamilika Julai 2026. Mpaka sasa mradi huo umefikia zaidi ya asilimia 95 huku meli zote zikiwa majini kwa hatua mbalimbali za uhakiki wa mwisho kuanza kutoa huduma.
Oktoba 2023, Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania (TPA) ilipokea maombi kutoka Kampuni ya Gold Voyage Logistics Limited, kampuni tanzu ya Zijin Mining Group Co. Ltd kutoka China ikiomba kukodishwa eneo katika Bandari ya Karema ili kujenga meli hizo.
Hayo yamesemwa na Msimamizi Msaidizi wa Bandari ya Karema, Anthony Poyo na wakati wa tukio la kuingizwa majini kwa mara ya kwanza meli ya nne ambapo kukamilika michakato wa vibali ukikamilika zitatoa huduma nchi za DR Congo, Zambia, Burundi na Tanzania mnufaika mkuu kutokana na kuwa na bahari.
Poyo amesema kukamilika kwa meli hizo kutaimarisha biashara kati ya Tanzania na nchi jirani kama Congo, Burundi na Zambia.
Amebainisha manufaa ya meli hizo kwamba unatarajia kuwa na kichocheo cha usafirishaji wa madini kama ya lithium, shaba na dhahabu kutoka eneo la Manono nchini DRC yanayochimbwa na kampuni hiyo ambapo kupitia Manono, Bandari ya Kalemie hadi Bandari ya Kigoma, Dar es Salaam na Tanga zitatumika kabla ya kusafirisha Kwenda nje ya nchi.
Aidha, Poyo amesema kupitia meli hizo, wakulima nao watanufaika kwa mazao ya kilimo pamoja na ajira kwa Watanzania hususan mabaharia ambapo kila meli moja inahitaji si chini ya mabaharia 15.
Pia, Shughuli za usafirishaji, upakiaji wa mizigo, huduma bandarini pamoja na biashara ndogondogo zitakazozunguka bandari hiyo zitapiga hatua.
"Ujenzi wa meli hizi kumetokana na Serikali kufungua fursa ya uwekezaji. Umeleta fursa kwa vijana, mlango wa kiuchumi kwa taifa letu na wananchi mmojammoja,” amesema Poyo.
"Hivi sasa tuna reli ya SGR, wamiliki wa wa malori watanufaika kwa kuchukua mizigo katika bandari hii. Tumehudumia zaidi ya tani 10,000 za mizigo katika bandari hii, hivyo kuja kwa meli hizi kutaongeza zenye uwezo wa kubeba tani 8,000 kwa wakati mmoja unaona jinsi tutakavyopiga hatua kubwa," amesema Poyo.
Kwa upande wa wakulima na wafanyabiashara, Poyo aamesema utarahisisha usafirishaji wa mazao kwenda katika masoko makubwa ya kikanda na kimataifa, kuongeza thamani ya mazao, kupanua masoko na kuongeza kipato cha wananchi wa mkoa wa Katavi na maeneo jirani kama ya Kigoma na Rukwa.
Mei 12, 2025, Naibu Waziri wa Uchukuzi, David Kihenzile alifanya ziara Karema kujionea ujenzi wa meli hizo zitakavyoinufaisha zaidi Tanzania kwani usafirishaji wa shehena ya mizigo kutoka Bandari ya Kigoma unategemea kutumia miundombinu ya reli zilizopo za MGR na SGR hadi Bandari ya Dar es Salaam na Tanga.
Kwa upande wake, Meneja Rasilimali Watu kutoka Kampuni ya Ankola Shipyard Co. Ltd ambao ndiyo waliounda meli hizo, Mohammed Mohamed Chande amesema mradi huo ulianza April mwaka jana na ulitarajia kukamilika Julai mwaka huu.
"Mradi umekuja kufungua njia na mlango wa kiuchumi Ziwa Tanganyika. Tunashukuru kwa ushirikiano ambao tuliupata kutoka serikalini na TPA hadi kutuwezesha kumaliza kwa wakati,” amesema.
Amesema fursa za ajira kwa vijana zimepatikana tangu mradi ulipoanza kwani wengi wamepata ujuzi na kuwa na manufaa kwa taifa," amesema Chande.
Kuhusu changamoto, Chande amesema wakati wa utekelezaji walikumbana na mabadiliko ya hali ya hewa ambayo waliweza kukabiliana nayo.
Baadhi ya wananchi wamepongeza hatua hiyo ya kukamilika kwa ujenzi wa meli hizo kwani shughuli zao za kilimo, uvuvi na mifugo huenda ikapata masoko ya ndani na nje kwani usafirisaji utakuwepo.