Black Sniper
JF-Expert Member
- Dec 10, 2013
- 32,406
- 55,148
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
hahahahaumenikumbusha long time!niliacha kula mikate kwa ajili ya hii bakery!nilikuwa mdogo by then kaka yangu ndo alikuwa ananipa story jinsi wanavyokanda huo unga hapo kwa wasomali
Zama hizo ilikuwa ikisikika kuwa watu wazima wa haja walikuwa wakikanda unga wa ngano wa kutengenezea mikate kwa kutumia miguu ! Nimekuwa nikijiuliza hivi haya mambo yalikuwa ya kweli au ni stori za vijiweni. Naambiwa wanaume walikuwa wanalowa jasho chapa chapa, ila sasa wangefanyaje na vitendea kazi havikuwepo. Hivi hali ikoje siku hizi?
Msiishie kwenye mikate tu,hata kwa scale ndogo ya mapishi mambo ya kukuna nazi mama ntilie ana kitoto kichafuchafu na anakisafisha huku akiendelea na upishi mara kwapa au kunani kumemuwasha anajikuna, lazima upate tu ile ladha tamu ya ziada na umsifie kwa kujua kukarangiza ! .kingine wale watayarishi wa mvinyo kiasili kule ulaya huzitia zabibu katika mabeseni makubwa na huita rafiki zao basi hupiga stori wakinywa mvinyo huku wakiwa kwenye beseni zile wakiziponda zabibu kwa miguu yao!
picchu mbona hao watu wako uchi mama weeeee hiyo wine inafukiza mikojo tu lol
Aghhhhh jamani....alafu kiboflo mbona ndo hatuwezi kukikosa? Ah wadudu wote wanakufa kwenye matanuri banaa. ..
Boflo na urojo wa kokoni kwa kombo shosti sina la kukwambia......urojo ule sijaona mfano wake mtamu balaa
Mtumeee usitake kuntapisha saa hizi......vyakula vya kununua vina mashaka yaani tu ujilie ila usiombe uende mazingira yanayopikwa unaweza usile tena cha kununua.....
Bora watu tufanye mazoezi ya kufunga kwa muda mrefu ili iwezekanapo tule nyumbani tu! Labda mtu ukisafiri!
Cha kununua ndio kizuri,ukimaliza kula huoshi vyombo.
Nalog off
Dhaaa wine tena na ninavyoipenda.umenifanya niwaze mpk najionea huruma ila siwezi wacha kuinywaa.ntavumilia tu hvyo hvyo
Mie pia niliwahi kubahatika kusogea karibu na sehemu wanayooshea vyombo kwenye eneo la biashara ya mama ntilie. Duh, haisemekani, ila waswahili tunasema mbaya kuona, maana chakula kizuri ni kile ulichopika nyumbani kwako, huko nje tule tu, tusiwaze upande wa pili.ndio maana hutakiwi kuuliza uliza ama kuchunguza. we kula nenda kaharishie mbele na usirudi tena pale
siku moja nilizidiwa na njaa na nilipotafuta pa kuipunguzia kwa vyakula vya kawaida nikakosa kabisa maamuzi yakawa nikatulie walau na chips
nilipofika nikajisogeza karibu na anapooshea na kupikia nilichokiona nilisinyaa utumbo na nikashiba ghafla. hayo maji ya kuoshea sahani afadhali yale unayopishana nayo tandale kwa tumbo
Zama hizo ilikuwa ikisikika kuwa watu wazima wa haja walikuwa wakikanda unga wa ngano wa kutengenezea mikate kwa kutumia miguu ! Nimekuwa nikijiuliza hivi haya mambo yalikuwa ya kweli au ni stori za vijiweni. Naambiwa wanaume walikuwa wanalowa jasho chapa chapa, ila sasa wangefanyaje na vitendea kazi havikuwepo. Hivi hali ikoje siku hizi?