Kukanda unga ngano wa mikate kwa miguu

Kukanda unga ngano wa mikate kwa miguu

1409214413289.jpg1409214440699.jpg
 
umenikumbusha long time!niliacha kula mikate kwa ajili ya hii bakery!nilikuwa mdogo by then kaka yangu ndo alikuwa ananipa story jinsi wanavyokanda huo unga hapo kwa wasomali
hahahaha
 
Zama hizo ilikuwa ikisikika kuwa watu wazima wa haja walikuwa wakikanda unga wa ngano wa kutengenezea mikate kwa kutumia miguu ! Nimekuwa nikijiuliza hivi haya mambo yalikuwa ya kweli au ni stori za vijiweni. Naambiwa wanaume walikuwa wanalowa jasho chapa chapa, ila sasa wangefanyaje na vitendea kazi havikuwepo. Hivi hali ikoje siku hizi?

Kweli ehh! Sasa nimegundua kwa nini mikate ya zamani ilikuwa mitamu kuliko ya sasa hivi. Ni sawa na mboga iliyopikwa kwenye chungu, huwa ni tamu sana kulinganisha na mboga iliyopikwa kwenye masufuria yenu ya kisasa.
 
Msiishie kwenye mikate tu,hata kwa scale ndogo ya mapishi mambo ya kukuna nazi mama ntilie ana kitoto kichafuchafu na anakisafisha huku akiendelea na upishi mara kwapa au kunani kumemuwasha anajikuna, lazima upate tu ile ladha tamu ya ziada na umsifie kwa kujua kukarangiza ! .kingine wale watayarishi wa mvinyo kiasili kule ulaya huzitia zabibu katika mabeseni makubwa na huita rafiki zao basi hupiga stori wakinywa mvinyo huku wakiwa kwenye beseni zile wakiziponda zabibu kwa miguu yao!

Na ndio maana katika mahoteli makubwa wanawake sio wapishi,kazi zao ni usafi na kukaribisha wageni!
 
Aghhhhh jamani....alafu kiboflo mbona ndo hatuwezi kukikosa? Ah wadudu wote wanakufa kwenye matanuri banaa. ..
 
Mtumeee usitake kuntapisha saa hizi......vyakula vya kununua vina mashaka yaani tu ujilie ila usiombe uende mazingira yanayopikwa unaweza usile tena cha kununua.....

Cha kununua ndio kizuri,ukimaliza kula huoshi vyombo.
Nalog off
 
Bora watu tufanye mazoezi ya kufunga kwa muda mrefu ili iwezekanapo tule nyumbani tu! Labda mtu ukisafiri!
 
Dhaaa wine tena na ninavyoipenda.umenifanya niwaze mpk najionea huruma ila siwezi wacha kuinywaa.ntavumilia tu hvyo hvyo

Ilikuwa enzi hizo lakini siku hizi kuna mashine zinazokamua.
 
ndio maana hutakiwi kuuliza uliza ama kuchunguza. we kula nenda kaharishie mbele na usirudi tena pale
siku moja nilizidiwa na njaa na nilipotafuta pa kuipunguzia kwa vyakula vya kawaida nikakosa kabisa maamuzi yakawa nikatulie walau na chips
nilipofika nikajisogeza karibu na anapooshea na kupikia nilichokiona nilisinyaa utumbo na nikashiba ghafla. hayo maji ya kuoshea sahani afadhali yale unayopishana nayo tandale kwa tumbo
Mie pia niliwahi kubahatika kusogea karibu na sehemu wanayooshea vyombo kwenye eneo la biashara ya mama ntilie. Duh, haisemekani, ila waswahili tunasema mbaya kuona, maana chakula kizuri ni kile ulichopika nyumbani kwako, huko nje tule tu, tusiwaze upande wa pili.
 
Zama hizo ilikuwa ikisikika kuwa watu wazima wa haja walikuwa wakikanda unga wa ngano wa kutengenezea mikate kwa kutumia miguu ! Nimekuwa nikijiuliza hivi haya mambo yalikuwa ya kweli au ni stori za vijiweni. Naambiwa wanaume walikuwa wanalowa jasho chapa chapa, ila sasa wangefanyaje na vitendea kazi havikuwepo. Hivi hali ikoje siku hizi?

Kwa hiyo tulikuwa tunakula jasho yelewiiiiiiiiiiiiiiiiiii
 
Back
Top Bottom