Kukata kodi ya jengo kwenye LUKU, watakaokuwa walipaji wakuu ni wapangaji na si wamiliki tena

Uwezo wa viongozi wetu wa kufikiri una walakini. Wananchi masikini wanakwenda kubebeshwa mzigo wa malipo ya kodi ya majengo tena. Nasema hivi kwa kuwa nyumba nyingi wapangaji ndiyo wanaonunua umeme na wala si wamiliki.

Sasa kitendo cha kukata kodi ya pango la jengo kutoka kwenye umeme ni kuwaumiza wananchi masikini wa nchi hii huku wamiliki wa majengo hayo wakiendelea kuchukua kodi zao kama kawaida.

Bajeti mbaya kuwahi kutokea tangu Uhuru.
Kwani mpangaji anashindwa nini kukata hiyo kodi ya jengo kwenye pesa anayomlipa mwenye nyumba?
Kama umekubaliana na mwenye nyumba sh 200,000 kwa mwezi, na hali ukijua ya kwamba utamlipia kodi ya jengo ya sh 1,000 kwa mwezi, mbona ni rahisi tu kukubaliana kwenye mkataba kuwa utakuwa unalipa 199,000 kwa mwenye nyumba.
 
Hadi nyumba za matope na nyasi, mabanda ya kuku,ngombe, zenye kuku zitalipiwa Kodi ya majengo. Jengo moja lenye luku 5 ,Kodi ya majengo ni mara Tano. Hii plan ninashauri ianzie Tanzania visiwani.

Visiwani asilimia kubwa ya watu wana nyumba zao binafsi sijawahi ishi nyumba ya kupanga kwa miaka yote niloishi hata kaka ni kwenda kwa ndugu kwa Zanzibar cjwah lala nyumba ya kupanga mpaka nilpoanza chuo nikaishi hostel kwaio haitaathiri watu mana kwa hao ambao wanapanga haichkui miaka mitano mtu anaishi nyumban kwake inshort ipunguzwe hiyo ni kubwa mana kuna nyumba zina meter zaidi ya moja
 
Uwezo wa viongozi wetu wa kufikiri una walakini. Wananchi masikini wanakwenda kubebeshwa mzigo wa malipo ya kodi ya majengo tena. Nasema hivi kwa kuwa nyumba nyingi wapangaji ndiyo wanaonunua umeme na wala si wamiliki.

Sasa kitendo cha kukata kodi ya pango la jengo kutoka kwenye umeme ni kuwaumiza wananchi masikini wa nchi hii huku wamiliki wa majengo hayo wakiendelea kuchukua kodi zao kama kawaida.

Bajeti mbaya kuwahi kutokea tangu Uhuru.
Unakuwaje na Luku halafu usiwe na nyumba au kwako ambako ukiaga kazini unasema unaenda nyumbani kwako- mzee mita ya luku ndiyo nyumba
 
Ni nyumba ya kiwango gani inapaswa kulipa kodi? Maana kutokana na mradi wa REA hadi mabanda ya nyasi na mbao yana umeme!
 
Uwezo wa viongozi wetu wa kufikiri una walakini. Wananchi masikini wanakwenda kubebeshwa mzigo wa malipo ya kodi ya majengo tena. Nasema hivi kwa kuwa nyumba nyingi wapangaji ndiyo wanaonunua umeme na wala si wamiliki.

Sasa kitendo cha kukata kodi ya pango la jengo kutoka kwenye umeme ni kuwaumiza wananchi masikini wa nchi hii huku wamiliki wa majengo hayo wakiendelea kuchukua kodi zao kama kawaida.

Bajeti mbaya kuwahi kutokea tangu Uhuru.
Mbona Motor Vehicle tunalipa hata sisi wawasha vibatari na hatujalalamika?
 
Ni 1000 kila mwezi. Kwa maana nyingine kwa mwaka ni 12000 tofauti na 10000 ya awali kwa hizi nyumba zetu za kawaida. In summary ni kwamba kodi ya majengo imepanda kwa 2000 zaidi.
Sawa tu,bila Kodi hakuna maendeleo, umeme vipi sisikiie mkiuzungumzia, pia wamekosea kushusha bei ya kuunganishiwa umeme??au,,, maana watu mnapinga kila kitu
 
Uwezo wa viongozi wetu wa kufikiri una walakini. Wananchi masikini wanakwenda kubebeshwa mzigo wa malipo ya kodi ya majengo tena. Nasema hivi kwa kuwa nyumba nyingi wapangaji ndiyo wanaonunua umeme na wala si wamiliki.

Sasa kitendo cha kukata kodi ya pango la jengo kutoka kwenye umeme ni kuwaumiza wananchi masikini wa nchi hii huku wamiliki wa majengo hayo wakiendelea kuchukua kodi zao kama kawaida.

Bajeti mbaya kuwahi kutokea tangu Uhuru.
Mbona Kodi ya motor vehicle kukatwa kwenye mafuta ujaizungumzia miaka yote?? Kodi ya jengo anaelipa mwenye nyumba, we katika uho mkataba wako kata iyo bukubuku ya jengo dada
 
Kwani mpangaji anashindwa nini kukata hiyo kodi ya jengo kwenye pesa anayomlipa mwenye nyumba?
Kama umekubaliana na mwenye nyumba sh 200,000 kwa mwezi, na hali ukijua ya kwamba utamlipia kodi ya jengo ya sh 1,000 kwa mwezi, mbona ni rahisi tu kukubaliana kwenye mkataba kuwa utakuwa unalipa 199,000 kwa mwenye nyumba.
Mijitu Ni mizuzu kaka, yaani hii nchi Ina Majinga mengi sana
 
Ni jambo jipya. Na makubaliano yanapaswa kuwa revisited.

Na hii maana yake ni kuwa, makubaliano na mikataba ya upangaji ipitiwe upya kwa kuzingatia hili.

Mimi binafsi nina nyumba na nimeweka wapangaji. Wakihoji na kuona kuwa ni mzigo kwao, basi niko tayari kuwapunguzia kodi kwa kiwango cha kodi ya jengo langu.

It's simple like that.
Hivi inakuaje kwa wale ambao wana zaidi ya mita moja ya luku kwenye jengo moja?
 
Unakuwaje na Luku halafu usiwe na nyumba au kwako ambako ukiaga kazini unasema unaenda nyumbani kwako- mzee mita ya luku ndiyo nyumba
Mkuu kuna watu wanakaa nyumba za serikali na zina LUKU, inamaana mtumia luku ndo atalipa hiyo kodi au?
 
Anza kudai punguzo la buku kila mwezi toka kwa baba mwenye nyumba. Kwa Mwaka elfu 12,000. Au ukitaka acha kununua luku liwe jukumu la mwenye nyumba.

Binafsi nimefurahia urahisi wa kulipa kila mwezi elfu moja. Watu wa halmashauri kila siku walikuwaa wananiletea barua za ukumbusho kulipa lakini muda wa kwenda kupanga foleni TRA nilikuwa sina
Nyumba zisizo na umeme vp
 
Ukitaka kumdhurumu mtu wewe mwambie lipa kidogokidogo
 
Back
Top Bottom