Kukatika kwa nywele

Kukatika kwa nywele

Mahondaw

JF-Expert Member
Joined
Apr 9, 2013
Posts
67,252
Reaction score
168,563
Jamani Jamani naomba mnishauri nifanyeje mwenzenu ni wiki mbili tu zimepita tangu niritachi nywele zangu kwa dawa ya radiant.

Nilifululiza kusuka kama miezi mitatu hivi Sa majuzi nilipofumua nikasema ngoja niritachi kwanza kichwa kipumue nikae kama wiki mbili nibane na kuchana mitindo mingine haaa mpaka dakika hii nywele zimekatika vya hatari.

Zilikua ndefu sana jamani nimesuka miaka nenda rudi leo ukiziona hapa mbele ndo ndefuuuu kuanzia katikati ya kichwa mpaka nyuma kote huko utafikiri mtu alieanza kutonea miezi miwili jamani kha! Nashindwa cha kuzifanya nikiwazaakili ni kama imestack kidogo.

kichwani Nimevaa kofia na vitambaa mpaka pozi limeniishia kwani kuna nguo nyingine vitambaa na kofia zinagoma kabisa mazingira mengine kofia vitambaa sio haviendani na kunyoa naona dah!
 
kama kinga hazijapungua sijui tena tatizo litakuwa nini
 
Kwani ulikuwa unatumia dawa hiyo Mara nyingi na pia unapenda kuziwekea conditioner

Na ushauli wangu ndani ya mwezi mmoja jitaidi kukaa na mtindo wiki 2 na hizo 2 zinazo baki fanyia stimin na kaa bila kusuka ukingoja wiki 2 zipite.

Nywele ni matunzo ndugu yangu unaweza kuona unanywele nyingi zikikosa afya utalia mwenyewe
 
Umeshapima ngoma

Mara kibao tu..mbona
Halafu ukimwi haukati nywele bana ukimwi nywele zenyewe bila kuweka dawa zinakua lainiii za kuteleza fulani. you remind me our jirani imelda died 2010 of HIV / AIDS OMG rest in peace jirani!
 
nywele ni asili
mwingine hana matunzo na nywele but zko vizuri na hazkatika na mwingine ndo ivo znakatiks sana tuuu,so poleee ndugu jitahidi kuwekea stiming na pia ukisuka usikae nazo sanaa coz nayo mi sababu ya kukatika kwa nywele
 
Pole sana inawezekana ulipokuwa ukizisuka ulikuwa hufanyi treatment kwa hiyo zikawa dhaifu au aliyekuweka dawa alikuweka vibaya nywele zikakatika au msuko mmojawapo uliosuka umekukata nywele...maoni yangu kwako hapo ni either kuzilinganisha uendelee kusuka hadi zikue pia castor black oil itakusaidia utafute na treatment nzuri ya nywele. Pole sana
 
Jamani Jamani naomba mnishauri nifanyeje mwenzenu ni wiki mbili tu zimepita tangu niritachi nywele zangu kwa dawa ya radiant.
Nilifululiza kusuka kama miezi mitatu hivi Sa majuzi nilipofumua nikasema ngoja niritachi kwanza kichwa kipumue nikae kama wiki mbili nibane na kuchana mitindo mingine haaa mpaka dakika hii nywele zimekatika vya hatari.
Zilikua ndefu sana jamani nimesuka miaka nenda rudi leo ukiziona hapa mbele ndo ndefuuuu kuanzia katikati ya kichwa mpaka nyuma kote huko utafikiri mtu alieanza kutonea miezi miwili jamani kha! Nashindwa cha kuzifanya nikiwazaakili ni kama imestack kidogo. kichwani Nimevaa kofia na vitambaa mpaka pozi limeniishia kwani kuna nguo nyingine vitambaa na kofia zinagoma kabisa mazingira mengine kofia vitambaa sio haviendani na kunyoa naona dah!
Steaming ni kitu muim sana katika utunzaj wa nywele
Radiant ndo dawa unatotumia siku zote ama ulibadilisha??
 
Jamani Jamani naomba mnishauri nifanyeje mwenzenu ni wiki mbili tu zimepita tangu niritachi nywele zangu kwa dawa ya radiant.
Nilifululiza kusuka kama miezi mitatu hivi Sa majuzi nilipofumua nikasema ngoja niritachi kwanza kichwa kipumue nikae kama wiki mbili nibane na kuchana mitindo mingine haaa mpaka dakika hii nywele zimekatika vya hatari.
Zilikua ndefu sana jamani nimesuka miaka nenda rudi leo ukiziona hapa mbele ndo ndefuuuu kuanzia katikati ya kichwa mpaka nyuma kote huko utafikiri mtu alieanza kutonea miezi miwili jamani kha! Nashindwa cha kuzifanya nikiwazaakili ni kama imestack kidogo. kichwani Nimevaa kofia na vitambaa mpaka pozi limeniishia kwani kuna nguo nyingine vitambaa na kofia zinagoma kabisa mazingira mengine kofia vitambaa sio haviendani na kunyoa naona dah!

Tension alopecia, tumia Tress
 
Tumia black castor oil ya jamaica ni nzuri sana....halafu usipende kusuka mfululizo bila kuzitreat nywele zako(kuziosha,kueka steaming etc)...Pia ue unasuka protective styles ambazo hazikati nywele zako kwa haraka....
 
Kama unachaganya dawa ndo shida inapoanzia. Kuna kipindi nilichaganya dawa nywele zilikatiika, hzo ndo nikaanza kuweka mega,pia usipende kuweka weka steaming zinaharibu nywele
 
Kuwa unapenda kusuka kwa mtu mmoja, kubadili wasusi wengine wana mikono mibaya

Suka muda mrefu kabla ya kiretouch mf: mimi naretouch mara2 kwa mwaka

Kila ukifumua fanya steaming
 
Kama unachaganya dawa ndo shida inapoanzia. Kuna kipindi nilichaganya dawa nywele zilikatiika, hzo ndo nikaanza kuweka mega,pia usipende kuweka weka steaming zinaharibu nywele
Mbona tunachanganyikiwa humu ndan coz wengne wanadiscourage steaming wengine mnaincourage, tunaomba na sababu jaman
 
Tumia jamaican black Castrol itasaidia zikue ila unahitaji kuzifanyia steaming protein steaming eg mayonnaise na moisture base steaming kama perfect, cholesterol ya dark and lovely kila unapofumua hizi steaming unazipishanisha ukieka kwanza protein inayofuata eka moisture

pia kuwa makin na style unazosuka nyingine zinafanya nywele kufungana hivo kukatika and labda ulieka dawa isio faa jaribu mega au olive oil za box ni nzur.
 
Ukisuka muda mrefu na hasa kama unasukasuka nywele za kuongezea (Rasta, weavings...) unakua umezibebesha nywele mzigo.

Pia pale mahali uzi wa kushonea unapopita au rasta zilipoanzia huwa dhaifu kwa sababu nywele hukazwa au ndio panapobeba ile nywele.

Hushauriwi kuweka dawa mara tu baada ya kufumua.
Ukifumua chana nywele zako vizuri. ZIOSHE, FANYA STEAMING inayoendana na aina ya nywele yako.

Paka mafuta mazito KILA SIKU kwenye ngozi chini ili ngozi isiwe kavu kwa muda wa wiki nzima tangu kufumua na kuziosha.

Hii inafanya nywele zirudi kwenye hali yake na ziwe imara.
Baada ya wiki sasa unaweza kurudia kutia dawa.
Utapata matokeo mazuri.

PIA KUMBUKA KWENYE KUWEKA DAWA, NYWELE ZISIZO NA DAWA TU NDIO ZINATAKIWA KUWEKWA DAWA.
Ila wengi huwa sio waelewa.
 
Back
Top Bottom