Hebu ngoja niweke hivi; uhuru wa maoni ni pamoja na uhuru wa maoni ya kijinga. Uhuru wa maoni si lazima yawe maoni tunayoyataka sisi au tunayojisikia ni ya kutufurahisha. Uhuru wa maoni haupo ati kwa sababu lugha ni ya kistaarabu kwa hiyo ikitumika lugha isiyo ya kistaarabu basi kuna polisi (Tido) na wenzake ambao wanaamua kusema "hatutatiki kukusikiliza". Endapo mtu anasema kitu ambacho kinavuka uhuru huo yule anayesemwa anatakiwa kwenda mahakamani. TBC siyo msimamizi wa maoni hayo.
Lakini jingine ni kuwa madongo yaliyorushwa na JK na wenzake Jangwani dhidi ya wapinzani yalikuwa ni ya kistaarabu? Au ni ustaaarabu kuelekea CCM na siyo kwingine?
Lakini kubwa zaidi ni kuwa Watanznaia ni watu wazima na wana uwezo wa kusikiliza, kuamua na kukataa hoja za kijinga au kipuuzi. Hawahitaji serikali ikae kama nanny kuamua kusema "hili watanzania hawastahili kulisikia". Hakuna chochote ambacho kimetamkwa jangwani ambacho hakijawahi kluandikwa au kuzungumzwa na vyombo vya habari.
Jamani, kama demokrasia imewashinda wajaribu udikteta!