Hata wakati Tido anaongea jana usiku, ukiangalia uso wake kwa makini unaona kabisa alikua anajisikia aibu kwa anayoyasema...hivi Tido,heshima yote uliyojijengea ukiwa TBC, ndo unaishusha kwa kasi hivi?? Unajua ni vijana wangapi umewa-inspire wawe watangazaji kutokana na influence yako ya zamani?? Unadhani hapo TBC utakaa milele?? Unanisikitisha sana siku hizi, ulivyotoka BBC kwa jinsi tulivyokuheshimu, mojawapo ya maoni ya wadau ilikua ni pamoja na kukupa udaktari wa heshima katika fani ya habari, lakini kwa haya yanayoendelea chini yako, sijui unawaandalia future ya aina gani Evans na ndugu zake hapo TBC,kumbuka miaka inaenda....