Elections 2010 Kukatishwa Kwa Matangazo Jangwani: Tido Mhando Alonga

Kwahili nadhani kuna tatizo la watu wengi kutokuwa objective. Ni kweli kwamba kuna mahakama, lakini je hao wanaoona kwamba wamekashifiwa au TBC inaamini wamekashifiwa mnadhani wakienda mahakani TBC itakuwa salama au nayo itatakiwa kulipa faini kwa sababu wao ndio wamerusha kashfa hizo? Kwa ujumla TBC haiwezi kurusha matangazo wanayoamini kuwa ni kashfa eti km mtu huyo anadhani amekashifiwa aende mahakani wakati wanauwezo wa kuzuia hali hiyo isitokee. Lazima tukumbuka kuwa TBC nao wanawajibika kwenye matangazo wanayoyarusha sio mtu aliyetukanwa au kudhalilishwa tu.
Pia dhana ya kumpiga mwandishi wa habari, huu ni upuuzi wa hali ya juu. Kwa bahati mbaya CHADEMA nao wanataka kuuvaa mkenge huu. Ni rekodi mbaya saana kwao na lazima viongozi wa CHADEMA wajitokeze wazuie hali hii. SIASA sio uhuni.
 
Aanfal,
TBC haiwezi kuwa "sued" kwa kashfa kwa kutangaza live matamshi yanayoonekana kuwa "kashfa" dhidi ya mtu fulani. Tuseme leo Marando amesema Kikwete alihusika katika mikataba iliyopelekea watu kuzikwa wakiwa hai Bulyankulu, na sasa Kikwete amesema atalipa fidia. Kama allegations hizi si kweli mwenye dhamana ya kushtakiwa ni Marando na wala si TBC. TBC walihusika tu kutangaza mkutano wa CHADEMA, ambao ulikuwa news worthy, lakini hawawezi kuhusika kushtakiwa kwa content za mkutano huo.
 

Huyu Tido historia itamfananisha na aliyewahi kuwa waziri wa ulinzi wa Marekani kipindi Marekani ilipovamia Iraq. Waziri huyo aliyekuwa anaitwa Rumsfeld, alikuwa na kiburi sana. Alikuwa anamsikiliza G. Bush peke yake, hata bunge nchini mwake halikuwa aliheshimiki kwake. Wananchi wakaanza kupiga kelele juu yake. Nguvu ya umma ilipozidi kuwa kali, G. Bush aliamua kumuondoa. Alikuwa waziri wa ulinzi wa marekani ambaye alikuwa na nguvu sana kuliko hata wengine lakini sauti ya Umma ilimuondoa.

Sasa na Tido naye akae mguu sawa, maana siku hazifanani. This time watanzania hawadanganyiki na propaganda za technical issues. Be careful husijetolewa ngeu na watanzania waliochokana na tabia yako ya kujipendekeza.
 
Asubuhi hii nasikiliza vichwa vya habari vya magazeti na kuna gazeti ambalo limeandika kuwa hotuba zilitawaliwa na jazba na matusi ndo maana matangazo yalikatwa.Katika mjadala huu kuna maelezo ya kuwa matangazo yalikatwa baada ya Marando kuwataja kwa majina wakubwa,which is which??
 

labda waliposema slaa kapata mke. Lakini hili na mengine hayamhusu tido. Wapinzani wametukanwa sana na hawajazima tv zao ili wana wa nchi wasiyasikie matusi hayo
 
Hata wakati Tido anaongea jana usiku, ukiangalia uso wake kwa makini unaona kabisa alikua anajisikia aibu kwa anayoyasema...hivi Tido,heshima yote uliyojijengea ukiwa TBC, ndo unaishusha kwa kasi hivi?? Unajua ni vijana wangapi umewa-inspire wawe watangazaji kutokana na influence yako ya zamani?? Unadhani hapo TBC utakaa milele?? Unanisikitisha sana siku hizi, ulivyotoka BBC kwa jinsi tulivyokuheshimu, mojawapo ya maoni ya wadau ilikua ni pamoja na kukupa udaktari wa heshima katika fani ya habari, lakini kwa haya yanayoendelea chini yako, sijui unawaandalia future ya aina gani Evans na ndugu zake hapo TBC,kumbuka miaka inaenda....
 
Mungu wangu! What a shame!
Niwape moyo wapenda mabadiliko ya kweli kuwa haya ni mapito tu ambayo ukombozi wowote lazima upitie.
Hizi ni dalili kuwa mapambano ya ukombozi yameshaanza kuguza mizizi ya udhalimu na sasa wadhalimu wanahaha.
 
=========
Anfaal
Mimi nitakubaliana nawe siku nikiona TBC inakata matangazo ya CCM kwa sababu Makamba katukana, Kikwete kakejeli na Hiza kakufuru kama ilivyo kawaida yao. Kinyume na hapo, hii hekima unayotupa, inakata upande mmoja na haiingii akilini mwetu. Wote tumeona hotuba za hao watu, na wala TBC haikudiriki kukatisha matangazo, achilia mbali kutotuonyesha JK akianguka jukwaani. Na hii ni tabia hata ya magazeti ya serikali Habari leo na Daily news.
 
Hapo ndio watanzania watawafundisha TBC kufanya kazi kwa kufuata maadili. Waulize tabia ya fire kwenda kwenye tukio la moto bila maji imeishia wapi siku hizi


Loo...hiyo Avatar yako inanikumbusha vita ya wenyewe kwa wenyewe kenya baada ya uchaguzi
 
TBC NYAMBAF!!!!!
TIDO WATCH OUT!!!:mad2:
 
Kiongozi wa chadema alipoanguka ndipo wakakata matangazo?
 
Wote hapa tunaelewa kuwa CCM na serikali yake wanatafuta sababu kuifanya kampeni ya Chadema iwe ngumu na kuwapunguzia kasi, jambo lolote litakalotokea kama zile hotuba za akina Marando watalitumia kama sababu.

Pamoja na hayo, inakuwaje haya madongo yanarushwa na watu ambao juzi tu walikuwa CCM? wote tunakumbuka jinsi Marando alivyosaidiwa na CCM kupata ubunge wa East Africa kinyume na matakwa ya vyama vya upinzani. Akina Shibuda et al. ambao hadi siku chache zlizopita walikuwa wakimsifia Kikwete na hivi wamekimbilia upinzania kutafutia tiketi ya kugombea Ubunge, sina uhakika kama 'kufumba na kufumbua' wamepona ule ugonjwa wa unafiki unaoendelea ndani ya CCM?

Mie naona DEMOKRASIA imevamiwa na sio mara ya kwanza watanzania kudanganywa na manbii wa uongo wanaotumwa na CCM kuua upinzani???!!!!
 
sasa hayo matusi yako wapi hapoo, yaani TIDO amebadilika sana tena sana , sio TIDO yule wa BBC
 
Ha ha ha ama kweli CHADEMA ni wageni wa siasa za CCM ,yaani matangazo yamekatwa kidogo mnapiga makelele ,sizani kama mtaiweza mizengwe na mikakati ya Chama Tawala ? Mambo ndio kwanza ata CCM awajafungulia majibwa yao !!:lol:
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…