Logikos
JF-Expert Member
- Feb 26, 2014
- 15,460
- 24,233
Kwanini tusubiri Hisani ya Wamerakani ?!!!! Kwanini tusianze kwa kuwahoji wanaokusanya Kodi zetu huenda wanakusanya nyingi au hawazitumii ipasavyo...
www.jamiiforums.com
www.jamiiforums.com
Iwapo tunapunguza Utoaji Huduma (kubinafsisha); kwanini Kodi hazipungui? Je, tunaongeza kumbana Mwananchi ili kutoa (huduma) gani?
Kodi ni muhimu sana ili kufadhili shughuli za serikali, huduma kwa umma kama vile barabara na mashule, Usalama wa Jamii, Afya na Mengineyo. Sasa kama hata hayo kuanzia Elimu (Mikopo na Shule Binafsi); Afya tuna BIMA ya Afya na kulipia Private; Kuhakikisha wafanyakazi wanalipwa ujira stahiki...
Ustawi wa Jamii; A Penny Saved is a Penny Earned; Serikali inaweza Kumpunguzia Mzigo wa Matumizi Mwananchi hivyo Kumwongezea Kipato cha Kutumia
Maadui wetu hawajawahi Kubadilika Umasikini, Ujinga na Maradhi..., Vilevile Mahitahi Muhimu ya Binadamu hayabadilika (Chakula Malazi na Mavazi); Karne ya sasa ambayo sio kila mtu anaweza kuchukua Jembe na kwenda kulima mihogo na kupata kitoweo Pesa inahitajika. Hii ndio itakupatia mahitaji...