Kukatwa Misaada toka USAID kilio ni kikubwa!

Kukatwa Misaada toka USAID kilio ni kikubwa!

Kwanini tusubiri Hisani ya Wamerakani ?!!!! Kwanini tusianze kwa kuwahoji wanaokusanya Kodi zetu huenda wanakusanya nyingi au hawazitumii ipasavyo...

Hapa ndiyo tunajua kama tuna viongozi wasomi au vilaza acheni tuanze kuitegemea...hizo degree zao za uchumi hapa ndipo sehemu muhimu pa kufanyia kazi, mtegemea cha ndugu hufa masikini waswahili walisema
Wanapeana kwa kujuana, tujikumbushe usemi wa ndugu naization
 
1. Kukatwa kwa Msaada wa takribani Trillioni 1 TZS kwenye sekta ya Afya/Elimu kwa mwaka. Hilo litaumiza kila mtu, tusifurahie kindezi.

2. Sekta nyingine kama TRA (income tax), Health insurance, general insurance, mabenki (mikopo ya wafanyakazi), domestic airlines, kampuni za Magari zote zinakwenda kulia)).
CCM wanasema "Mama amezuia vifo vya wazazi" kumbe ni pesa ya USAID, ukiwa muongo buana unaishi kwa mashaka sana sana maisha yako yote
 
1. Kukatwa kwa Msaada wa takribani Trillioni 1 TZS kwenye sekta ya Afya/Elimu kwa mwaka. Hilo litaumiza kila mtu, tusifurahie kindezi.

2. Sekta nyingine kama TRA (income tax), Health insurance, general insurance, mabenki (mikopo ya wafanyakazi), domestic airlines, kampuni za Magari zote zinakwenda kulia)).
Wakati huo huo Serikali inatumia takriban Tshs 500B kwa mwaka kwa ajili ya kununulia magari, inatumia takriban Tshs 300B kwa matumizi ya kawaida ya ofisi za Umma na inatumia zaidi ya 300B kwa safafi za ndani na nje ya nchi. Vipi bwana kaka kama utashauri matumizi haya yapunguzwe ili tujibane pamoja na mambo mengine kufidia hali hii? Huoni kama tunafundishwa kujitegemea na katika hili tunaweza? Acha mimi niwe ndezi, kwa kweli nimefurahi sana kwa misaada hii kukatwa. Na ikatwe zaidi ili tusimame kwa miguu yetu wenyewe. Tunaweza.
 
Trump anafanya vyema, hii itasaidia sana kuwafanya waAfrika wengi(hususani Watu weusi) kuanza kuwa na akili nzuri ya kuweza kujitegemea wao wenyewe.
Hata Watawala waliopo watakuwa na Heshima na nidhamu ya hali ya juu kabisa katika Matumizi ya Fedha za Kodi za Wananchi.
Siyo siri hata kidogo,Watawala karibia wote kabisa wa nchi za Afrika hawana kabisa nidhamu nzuri ya hali ya juu katika Matumizi ya Fedha za Kodi za Wananchi waliopo katika nchi zao. Watawala wengi sana ni Wezi, Mafisadi, Wafujaji Sana wa Fedha za Kodi, n.k.
Tazama msafara huu wa Kiongozi huyu wa nchi fulani hapa Afrika kisha jiulize:- Je, ni gharama kubwa kiasi gani ilitumika kwenye msafara huu wa anasa? Je, kuna ULAZIMA wowote ule wa kuwa na misafafara kama hii kwenye nchi hiyo ambayo Bajeti yake ya kila Mwaka hutegemea Misaada kutoka Marekani na washirika wake? Je, Wananchi wa kawaida waliopo katika nchi hiyo wanaweza kupata faida gani hasa kutokana na misafafara yenye misururu mirefu ya magari kama huu?

Tafakari, Chukua Hatua!
Msafara una gari karibia 150 na hakuna hata gari moja chini ya milioni 200, bado karibia zoote ni zile ambazo zinatembea km 5 kwa lita 1.

Mambo haya ya kipuuzi inabidi yaishe, kuna sehemu hakuna umeme, maji, huduma ya afya tabu, darasamoja watoto 100 na bado shule nzima walimu wa5 tu.
 
Tanzania wakipokea pesa ya USAID huwa inaingizwa kwenye channel nyingi nyingi huko wizara ya Afya, nakumbuka sana wakati tunafanya Mradi wa Global Fund ( HIV//AIDS and TB), pesa nyingi ilikua imnajengewa mazingira ya kuliwa na watendaji wa serikali huku serikali na yenyewe ikiwa na % kwenye hizi issues. Kwa sasa hali itakua mbaya sana sana
 
1. Kukatwa kwa Msaada wa takribani Trillioni 1 TZS kwenye sekta ya Afya/Elimu kwa mwaka. Hilo litaumiza kila mtu, tusifurahie kindezi.

2. Sekta nyingine kama TRA (income tax), Health insurance, general insurance, mabenki (mikopo ya wafanyakazi), domestic airlines, kampuni za Magari zote zinakwenda kulia)).
 
Attachments

  • 5955854-cb3f65d5329085bfef676bf87f8c5800.mp4
    2.4 MB
Kama kawaida natarajia haya yafuatayo:

Kupanda kwa bei za bundle,
Kuongezeka bei ya luku na hela ya mwezi wa jengo ,
Kupanda kwa bei ya mafuta na nauli ,
Hawachomoki humo mkuu.

Lakini kusema mwaka huu hatununui v8 hawawazii hilo kuna mbunge mmoja alisema kila laini ikatwe Tsh 500 ili kila mtanzania apate bima ya afya ila nchi yangu.

TANZANIA HATUJAWAHI KUWA NA TATIZO LA HELA TUNA TATIZO LA USIMAMIZI MBOVU NA WIZI WA FEDHA ZA UMMA BASI.

Watu kila siku wanatajwa na CAG wanakula hela lakini ndio kwanza wengine wapo mpaka leo tena viongozi wanadunda yaani hela inayoliwa ni nyingi kuliko inayoenda kwenye miradi.
Aisee umeona mbali Sana Kwa kifupi tutarajie Kodi kuongezeka maradufu
 
1. Kukatwa kwa Msaada wa takribani Trillioni 1 TZS kwenye sekta ya Afya/Elimu kwa mwaka. Hilo litaumiza kila mtu, tusifurahie kindezi.

2. Sekta nyingine kama TRA (income tax), Health insurance, general insurance, mabenki (mikopo ya wafanyakazi), domestic airlines, kampuni za Magari zote zinakwenda kulia)).
Kila mtu lazima alie mpaka muuza mboga, wenye hotels, hata waliokuwa wanagongea jero
 
1. Kukatwa kwa Msaada wa takribani Trillioni 1 TZS kwenye sekta ya Afya/Elimu kwa mwaka. Hilo litaumiza kila mtu, tusifurahie kindezi.

2. Sekta nyingine kama TRA (income tax), Health insurance, general insurance, mabenki (mikopo ya wafanyakazi), domestic airlines, kampuni za Magari zote zinakwenda kulia)).
Acha tulie tujifunze kuacha uchawa tufanye kazi za kweli na zinazoonekana na sii zile za kupambwa kwa midomo ya chawa.
 
Wakati JPM anasema watanzania tufanye kazi kwa bidii, hatuna mjomba wa kutusaidia kuna baadhi ya raia na viongozi hawakuielewa hii kauli nadhani sasa wataielewa.
 
Kuna mtu mmoja wa CCM aka chama twawala alituaminisha sisi watanganyika ni matajiri tutembee kifua mbele - hao mabeberu hawana lolote.

Kwa hiyo mtoa mada ondoa shaka na hao wazungu - pesa ipo ndani ya Serikali twawala ya CCM tena ya kutosha - hakuna mtanganyika atakosa kidonge cha kurefusha maisha.
 
IMG_20250208_164152_054.jpg

Hizo condom zilizoandikwa GOT nazo zitaanza kuadimika Mtaani, maana zilikuwa ni za msaada kutoka UsAid

Baadhi ya watumishi waliokuwa wanapiga kimoja cha faster faster chooni/kwenye magari nao wajiandae 🙌
 
Back
Top Bottom