Pre GE2025 Kukimbia kwa Dkt. Nchimbi haikuwa sababu ya vyama vingine kususia mdahalo

Pre GE2025 Kukimbia kwa Dkt. Nchimbi haikuwa sababu ya vyama vingine kususia mdahalo

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)

safuher

JF-Expert Member
Joined
Feb 11, 2019
Posts
11,837
Reaction score
17,412
TUFANYE KWAMBA WOTE WALIKUBALI WATASHIRIKI MDAHALO HUU.

SWALI

Je kulikuwa na makubaliano yoyote kwamba kama hatoshiriki Dr nchimbi basi waliobaki wote wasishiriki ?

mjadala huu haukuwekwa maalumu kwa ajili ya Dr nchimbi,bali ni wananchi na makatibu wa vyama.

kitendo cha makatibu wakuu wengine kususia na kutishiriki eti kwa sababu fulani hajashiriki hiyo maana yake mdahalo huu ulikuwa na mrengo maalumu yaani ULIANDALIWA KWA AJILI YA MTU MMOJA.

kama mdahalo ulikuwa kwa ajili ya makatibu wote na wananchi waliohudhuria basi kwa nini kutokufika kwa mmoja huyo na wengine wagomee?

PIA SOMA
- Kuelekea 2025 - Mdahalo wa Makatibu Wakuu wa Vyama vya Siasa: Nchimbi kaingia mitini, wengine wagoma kushiriki!
 
Maskini nawaonea huruma star tv kwa cost walizotumia afu watu wanaingia mitini...
 
Chadema wamezingua sana, wao walipaswa waoneshe mfano wa kutokimbia maana nchimbi asingekuwa na majibu
 
Mdahalo bila chama kinachounda serikali unakuwa ni kama kikao cha masimango tu kwa marehemu. Wako sahihi kugomea.

Ova
Yalifanyika wapi makubaliano kwamba asipokuja yeye na mdahalo usifanyike ?
 
Chadema wamezingua sana, wao walipaswa waoneshe mfano wa kutokimbia maana nchimbi asingekuwa na majibu
Sahihi kabisa.

Kosa moja halihalalishi kosa jingine.

Kama Dr nchimbi kafanya kosa la kutohudhuria basi na wao ndio wafanye jambo linaloleta athari ya kutifanyika mjadala ?

Wamekosa uungwana mpaka bwana Odemba analia.
 
Chukua 10,000 alafu toa buku then nambie umebakiza kiasi gan.

Je ni msimbazi tena??

Basi umeelewa sasa. Hawa FISIEM kichwan hamna kitu kazi kutumia Pori-see tu ambao requirement ya recruitment yao wengi ni darasa la 7
 
Yalifanyika wapi makubaliano kwamba asipokuja yeye na mdahalo usifanyike ?
Rudia kusoma hayo maoni yangu, au mshirikishe uliyenaye hapo, halafu uone kama hili swali lako linanihusu mimi au Odemba.

Ova
 
Rudia kusoma hayo maoni yangu, au mshirikishe uliyenaye hapo, halafu uone kama hili swali lako linanihusu mimi au Odemba.

Ova
Swali hili ni kwa wote wanaosapoti kitendo cha wagombea wengine kukataa kushiriki kwa kisingizio cha kwamba wa CCM hakuwepo.
 
Swali hili ni kwa wote wanaosapoti kitendo cha wagombea wengine kukataa kushiriki kwa kisingizio cha kwamba wa CCM hakuwepo.
Karudie kusoma maoni yangu, itakusaidia sana kunielewa. Maana naona unazidi kupotea njia.

Ova
 
Karudie kusoma maoni yangu, itakusaidia sana kunielewa. Maana naona unazidi kupotea njia.

Ova
Nimeyaelewa maoni yako ambayo umeyatoa,na mimi nimetoa maoni yangu kuhusu maoni yako.

Suala la kwamba swali langu halikuhusu wewe sio tatizo kwani hata wewe umeniquote na wala haukuwa na majibu yanayonihusu mimi.
 
TUFANYE KWAMBA WOTE WALIKUBALI WATASHIRIKI MDAHALO HUU.

SWALI

Je kulikuwa na makubaliano yoyote kwamba kama hatoshiriki Dr nchimbi basi waliobaki wote wasishiriki ?

mjadala huu haukuwekwa maalumu kwa ajili ya Dr nchimbi,bali ni wananchi na makatibu wa vyama.

kitendo cha makatibu wakuu wengine kususia na kutishiriki eti kwa sababu fulani hajashiriki hiyo maana yake mdahalo huu ulikuwa na mrengo maalumu yaani ULIANDALIWA KWA AJILI YA MTU MMOJA.

kama mdahalo ulikuwa kwa ajili ya makatibu wote na wananchi waliohudhuria basi kwa nini kutokufika kwa mmoja huyo na wengine wagomee ?
Shadow SGs ni watoto wadogo mno kujadiliana na mtu mzima kama SG wa CCM ndio maana hayo yote yametokea 🐒
 
Mambo mengi yangemtaka yeye
Hayo machache ambayo yangewataka vyama vingine kwa nini waondoke wakati kuna machache yangewataka wao ?

Sio sahihi kususia huduma ndogo eti kwa sababu kuna huduma kubwa hauzipati.

Tumia hizo huduma ndogo huku ukizidai hizo kubwa.
 
Nimeyaelewa maoni yako ambayo umeyatoa,na mimi nimetoa maoni yangu kuhusu maoni yako.

Suala la kwamba swali langu halikuhusu wewe sio tatizo kwani hata wewe umeniquote na wala haukuwa na majibu yanayonihusu mimi.
Hukuelewa maoni yangu, mimi nimeeleza kuhusu situation, wewe unaniunganisha na maandalizi ya mdahalo.

Ova
 
Back
Top Bottom