Kukinukisha ni uhaini, ila wanaoiba mali za umma waone aibu!

Kukinukisha ni uhaini, ila wanaoiba mali za umma waone aibu!

Expensive life

JF-Expert Member
Joined
May 2, 2020
Posts
4,095
Reaction score
13,016
Nchi yangu nini hiki, aliyesema tutakunukisha ni muhaini, ila wanaoiba mali za umma kila uchwao waone aibu.

Hawa wezi wa mali za umma ndio wahaini sasa, ukiachana na baadhi ya maeneo mijini, zunguka vijijini uone hali ilivyo, ulinganishe na rasilimali za nchi hii. Ni huzuni.

Kama jiji la Dar es salaam tu wanateseka na maji vipi huko vijijini? Nimepata bahati kuzunguka mikoa kadhaa hali ni mbaya. Barabara, shule, hospital, maji na kadhalika ni huzuni.

Ukisika mtu kaiba mabilioni ya fedha alafu anaambiwa aone aibu bila kuwajibishwa, alafu kuna mwingine kasema tutakunukisha yupo gerezani unabaki kushangaa.
 
Ilitakiwa ukimkuta mtu amevaa vazi la kijani unagonga mawe mengi sana.
 
Kama kuna mtu yoyote unajua ameiba mali za umma, nenda kamshtaki mahakamani
 
Back
Top Bottom