Kukithiri Kwa vitendo vya rushwa mradi wa bwawa la mwalimu Nyerere (Julius Nyerere hydro power project)

Kukithiri Kwa vitendo vya rushwa mradi wa bwawa la mwalimu Nyerere (Julius Nyerere hydro power project)

Joined
Dec 20, 2016
Posts
96
Reaction score
115
Habari zenu Wana jukwaa la JamiiForums

Kwanza napenda kuipongeza serikali kusimamia utekerezaji wa ujenzi wa bwawa hili kubwa nchini la kufua umeme na kutoa fursa za ajira Kwa vijana wengi wa kitanzania

Lakini mradi unapoelekea kumalizika kumetokea tatizo kubwa sana la urasimu upande kupata ajira kutokana na vishoka kufanikiwa kuwakamata ma hr wa mradi hususani ma hr wanaokaa nje ya mradi kwenye vijiji vya mloka pwani na kisaki morogoro

Kawaida contractor mchina chibi ya kampuni ya sino hydro corporation na jv Arab na elsewedy electricity kutoka Misri

Wakihitaji wafanyakazi wenye ujuzi na ambao hawana ujuzi huwatumia Hawa ma hr kuwapata watu hao ambao wamekita Kambi Nje ya ofisi hizo

Lakini Kwa tamaa ya ma hr nafasi hizi hawapei walengwa na vishoka hutumika kuuza nafasi hizi kuanzia tsh 200000 Hadi tsh 400000

Na kwenda kufanya test kama unafani welder carpenter steel fixer na nyinginezo tsh 150000
Kwa mfano wakihitaji watu 30 nafasi 25 zitauzwa na nafasi 5 ndo zitafata taratibu iliyowekwa na wasoteaji wa kazi

Utata mwingine upo upande wa kupata majibu baada ya test mwarabu atakwambia umepita na utaitwa Kwa ajili ya ajira, Lakini pindi unaporudi kusubiri kuitwa ndo forever na ukienda ofisi ya hr utaambiwa Kwa jeuri umefeli

Tunaomba serikali kupitia wizara ya ajira na vijana na wizara ya ujenzi na taasisi nyingine kuchukua hatua Kali

Kwa sababu vijana wengi wapo wanalanda vijiji vya mloka na kisaki lakini kupata ajira ni ngumu mno na WAnaopata ajira ni wale waliotoa rushwa

Vijana tunapenda kufanya kazi shida hatuna Hela za kununua kazi
 
Nchi imefunguka Rushwa, Madawa ya kulevya, Meno ya Tembo kama kawaida oya KIMNANA 🐘🐘🐘🐘🐘🐘🐘
 
Back
Top Bottom