Kukojoa Hadharani yawa Fashion Dar aibu na adhabu kali vihusike?

Jaji Mfawidhi

JF-Expert Member
Joined
Feb 20, 2016
Posts
17,434
Reaction score
27,177
Dar es salaam, ukipita pale Jangwani unaona bodaboda ametoa mboo yake anakojoa, hajali nani ni nani, hajali watoto wa kike wa shule ya zanaki wala jangwani.

Ukienda maeneo mengi utaona wanaume wanatoa mboo, anakojoa na akimaliza anakunguta kunguta, unajiuliza hivi haoni aibu na fedheha, sasa ni wakati Tanzania tuamke na kukemea.

Mimi kama mama huwa nasikitika, lakini kwa mabinti wadogo wanapata fedhea na msongo wa mawazo!

Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi ya Uganda (UPDF) na mtoto wa Rais wa nchi hiyo Yoweri Museveni, Jenerali Muhoozi Kainerugaba, ameonya vikali kuhusu tabia ya watu kujisaidia haja ndogo hadharani na kupendekeza adhabu kali ya kifungo kisichopungua miaka mitano jela kwa watakaotiwa hatiani.

Kupitia ukurasa wake rasmi wa mtandao wa X, Jenerali Muhoozi ametoa wito kwa vyombo vya sheria kuwakamata papo hapo wanaume wote wanaojisaidia pembezoni mwa barabara mbele ya umma na watoto, akisisitiza kuwa kitendo hicho kinachafua mazingira na kuvunja heshima ya jamii.

Kauli hiyo imeibua mjadala mzito mtandaoni na miongoni mwa wananchi, ambapo baadhi ya watu wameunga mkono msimamo huo wakitaja kuwa ni hatua ya kuimarisha nidhamu, usafi na kuwalinda watoto dhidi ya mienendo mibovu barabarani.

Hata hivyo, wakosoaji na wataalamu wa sheria wamepinga vikali adhabu hiyo ya miaka mitano jela, wakieleza kuwa ni kubwa kupita kiasi kwa kosa dogo la kero ya usafi na haipo kwenye sheria za sasa za nchi ambazo kimsingi huweka adhabu ndogo za faini au kazi za kijamii kupitia sheria ndogo za mamlaka za miji.

Wadau wa mipango miji wameeleza kuwa changamoto kuu inayochochea tabia hiyo ni uhaba mkubwa wa vyoo safi na salama vya umma katika Jiji la Kampala na pembezoni mwa barabara kuu, wakishauri serikali kuboresha miundombinu kwanza kabla ya kutoa adhabu kali.

Hadi sasa, Serikali ya Uganda na Jeshi la Polisi havijatoa tamko rasmi la kuthibitisha iwapo mapendekezo hayo ya Jenerali Muhoozi yataingizwa rasmi katika miongozo ya kiutekelezaji ya kisheria au kubaki kuwa msimamo wake binafsi.
 
Attachments

  • pmh.jpeg
    pmh.jpeg
    203.1 KB · Views: 6
hata hapa boma sokoni nssf wanakojoa kawaida bila woga mrema alipokuwa waziri wa mambo ya ndani alizuia hii kitu na aliweza
 
Ilianza safarini kuchimba dawa kando ya barabara na nyuma ya basi, ikazoeleka kwamba unaweza ukakojoa hadharani bila aibu huku watu wakikutazama. Wanaume na wanawake wakawa wanashusha mikoja mbele ya abiria wenzao bila aibu
Hili jambo la kukemea kwa nguvu zote.
 
Shame upon them, sasa wawe wanarekodiwa na kupostiwa, alafu mtu anashika umme wake uliotoka kwenye uke asubuhi na kukuzia karanga, kukuchongea chungwa, hamna usafi.

Unaona kabisa muuza karanga kautoa, kaushika , anaukunguta alafu unanunua karanga unakula , tena unanawa kwanza maana una amini karanga ni safi
 
Dar es salaam, ukipita pale Jangwani unaona bodaboda ametoa mboo yake anakojoa, hajali nani ni nani, hajali watoto wa kike wa shule ya zanaki wala jangwani.
Ukienda maeneo mengi utaona wanaume wanatoa mboo, anakojoa na akimaliza anakunguta kunguta, unajiuliza hivi haoni aibu na fedheha, sasa ni wakati Tanzania tuamke na kukemea.
Mimi kama mama huwa nasikitika, lakini kwa mabinti wadogo wanapata fedhea na msongo wa mawazo!

Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi ya Uganda (UPDF) na mtoto wa Rais wa nchi hiyo Yoweri Museveni, Jenerali Muhoozi Kainerugaba, ameonya vikali kuhusu tabia ya watu kujisaidia haja ndogo hadharani na kupendekeza adhabu kali ya kifungo kisichopungua miaka mitano jela kwa watakaotiwa hatiani.
Kupitia ukurasa wake rasmi wa mtandao wa X, Jenerali Muhoozi ametoa wito kwa vyombo vya sheria kuwakamata papo hapo wanaume wote wanaojisaidia pembezoni mwa barabara mbele ya umma na watoto, akisisitiza kuwa kitendo hicho kinachafua mazingira na kuvunja heshima ya jamii.
Kauli hiyo imeibua mjadala mzito mtandaoni na miongoni mwa wananchi, ambapo baadhi ya watu wameunga mkono msimamo huo wakitaja kuwa ni hatua ya kuimarisha nidhamu, usafi na kuwalinda watoto dhidi ya mienendo mibovu barabarani.

Hata hivyo, wakosoaji na wataalamu wa sheria wamepinga vikali adhabu hiyo ya miaka mitano jela, wakieleza kuwa ni kubwa kupita kiasi kwa kosa dogo la kero ya usafi na haipo kwenye sheria za sasa za nchi ambazo kimsingi huweka adhabu ndogo za faini au kazi za kijamii kupitia sheria ndogo za mamlaka za miji.
Wadau wa mipango miji wameeleza kuwa changamoto kuu inayochochea tabia hiyo ni uhaba mkubwa wa vyoo safi na salama vya umma katika Jiji la Kampala na pembezoni mwa barabara kuu, wakishauri serikali kuboresha miundombinu kwanza kabla ya kutoa adhabu kali.
Hadi sasa, Serikali ya Uganda na Jeshi la Polisi havijatoa tamko rasmi la kuthibitisha iwapo mapendekezo hayo ya Jenerali Muhoozi yataingizwa rasmi katika miongozo ya kiutekelezaji ya kisheria au kubaki kuwa msimamo wake binafsi.View attachment 3665262
Jaji mfawizi Leo ndo nimejua Kama weweni mama .!
 
Ilianza safarini kuchimba dawa kando ya barabara na nyuma ya basi, ikazoeleka kwamba unaweza ukakojoa hadharani bila aibu huku watu wakikutazama. Wanaume na wanawake wakawa wanashusha mikoja mbele ya abiria wenzao bila aibu
Ni aibu sana, hili taifa linahita Mungu wa Israel kulikomboa.
 
Hili jambo la kukemea kwa nguvu zote.
tena ni aibu kabisa, mtu kasafiri na binti yake mkubwa anashusha kojo mbele ya kadamnasi, abiria wengi huogopa kujificha vichakani kwa hofu ya wanyama wakali na majambazi kwa hiyo wote hukojoa hapohapo karibu na basi, mbaya zaidi wengine wanashusha haja kubwa wakiwa wamejifunika kanga kubigubi, wakiinuka tu unaona kimba
 
Hujatembea ww...njoo mwanza uone watu wanavyoanika dakari zao mchana kweupe tena tena wakizielekeza kweny barabara ambazo kuna wingi wa watu wakiwemo watt wadogo....aibu utaona wewe
 
Shame upon them, sasa wawe wanarekodiwa na kupostiwa, alafu mtu anashika umme wake uliotoka kwenye uke asubuhi na kukuzia karanga, kukuchongea chungwa, hamna usafi.

Unaona kabisa muuza karanga kautoa, kaushika , anaukunguta alafu unanunua karanga unakula , tena unanawa kwanza maana una amini karanga ni safi
Umewasahau wauza soda, chupa anaishikia pale shingoni kabisa karibu na mdomo wa chupa.
 
Hao vichwa maji ni wa kutandikwa bakora nyingi za shingoni au wakamatwe kwa nguvu bila kufunga flies za sarawili zao na kupelekwa rumande.Sheria za afya katika serikali zipo na wanajua.Wanyukwe faini au miezi sitasita mung'anda au vyote kwa pamoja ili kenge wengine wakiona wataacha ujingaujinga.Hata kama hawajui kama ni kosa siyo utetezi kwao.Wanakojoakoja hovyo tu kama ngedere.
 
Vyoo vya kulipia vijengwe maeneo hayo wanaoenda kutoa mboo na kukojoa.
Kuna mtu hata hyo 300 ya kukojowa hana,,
Serikali ijenge vyoo vya public na viwe na watu wa usafi..

Hivi kujisaidia pia ulipe?.
Inchi ngumu sn hii
 
Back
Top Bottom