Dar es salaam, ukipita pale Jangwani unaona bodaboda ametoa mboo yake anakojoa, hajali nani ni nani, hajali watoto wa kike wa shule ya zanaki wala jangwani.
Ukienda maeneo mengi utaona wanaume wanatoa mboo, anakojoa na akimaliza anakunguta kunguta, unajiuliza hivi haoni aibu na fedheha, sasa ni wakati Tanzania tuamke na kukemea.
Mimi kama mama huwa nasikitika, lakini kwa mabinti wadogo wanapata fedhea na msongo wa mawazo!
Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi ya Uganda (UPDF) na mtoto wa Rais wa nchi hiyo Yoweri Museveni, Jenerali Muhoozi Kainerugaba, ameonya vikali kuhusu tabia ya watu kujisaidia haja ndogo hadharani na kupendekeza adhabu kali ya kifungo kisichopungua miaka mitano jela kwa watakaotiwa hatiani.
Kupitia ukurasa wake rasmi wa mtandao wa X, Jenerali Muhoozi ametoa wito kwa vyombo vya sheria kuwakamata papo hapo wanaume wote wanaojisaidia pembezoni mwa barabara mbele ya umma na watoto, akisisitiza kuwa kitendo hicho kinachafua mazingira na kuvunja heshima ya jamii.
Kauli hiyo imeibua mjadala mzito mtandaoni na miongoni mwa wananchi, ambapo baadhi ya watu wameunga mkono msimamo huo wakitaja kuwa ni hatua ya kuimarisha nidhamu, usafi na kuwalinda watoto dhidi ya mienendo mibovu barabarani.
Hata hivyo, wakosoaji na wataalamu wa sheria wamepinga vikali adhabu hiyo ya miaka mitano jela, wakieleza kuwa ni kubwa kupita kiasi kwa kosa dogo la kero ya usafi na haipo kwenye sheria za sasa za nchi ambazo kimsingi huweka adhabu ndogo za faini au kazi za kijamii kupitia sheria ndogo za mamlaka za miji.
Wadau wa mipango miji wameeleza kuwa changamoto kuu inayochochea tabia hiyo ni uhaba mkubwa wa vyoo safi na salama vya umma katika Jiji la Kampala na pembezoni mwa barabara kuu, wakishauri serikali kuboresha miundombinu kwanza kabla ya kutoa adhabu kali.
Hadi sasa, Serikali ya Uganda na Jeshi la Polisi havijatoa tamko rasmi la kuthibitisha iwapo mapendekezo hayo ya Jenerali Muhoozi yataingizwa rasmi katika miongozo ya kiutekelezaji ya kisheria au kubaki kuwa msimamo wake binafsi.
View attachment 3665262