Kukojoa kwenye chupa yenye mfuniko, halafu kila saa inafungwa mfuniko, kuna athari yoyote?

Kukojoa kwenye chupa yenye mfuniko, halafu kila saa inafungwa mfuniko, kuna athari yoyote?

Duniani kuna maajabu/vituko sana. Kushuka kitandani mtu anashindwa!!!!??
Mnaoshangaa kukojoa kwenye chupa ninyi ni mambo safi, mnaona jambo la ajabu mtu kukojoa kwenye chupa AU hamshikwi na haja ndogo mara kwa mara, ukibanwa na mkojo kila wakati lazima utaona kero kwenda chooni, itakupelekea utafute kopo.
 
Nnapokomenti hapa mi nina dumu la 5 litres mimi mpaka mchana nakojolea hapa.Naona uvivu kwenda nje.Nimezoeshwa na mama yangu kule Usangi milimani mana usiku baridi.Na napata starehe sana kukojoa kwa dumu.MADA.hakuna madhara yoyote alimradi uwe unamwaga kila asubuhi na kuosha kwa maji sabuni.
 
Kuna sehemu kutoka nje usiku utakutana na vitu vya ajabu sana nje so MTU anaamua kuwa na chupa pembeni. Sio ushamba unaepuka mambo mengi ya usiku asee usiku huwa kuna vitu vingi vya ajabu km hujawahi kutana navyo huwezi jua ila ndo hivo.
 
Khaa! nimesoma coment zote ajabu sijaona aliyempa jibu mtoa mada zaidi ya kubishana tuu sio uungwana kabisa.
 
Nyakati za usiku, wengine ni uvivu kuinuka kwenda chooni kujisaidia haja ndogo, baadala yake wanatumia kopo, ndoo au chupa kujisaidia haja ndogo.
Swali langu lipo kwenye hawa wanaotumia chupa yenye mfuniko, yaani akishamaliza kukojoa, anaifunga kwa mfuniko.
Maswali:
(1) Lile joto kali linalokuwa kwenye chupa linalosababishwa na kufunga chupa kwa mfuniko kwa muda mrefu halina athari kwenye uume?
(2) Ukitumia chupa au kopo kwa muda mrefu, kwenye kopo au chupa kunabaki vitu kama magadi, yale magadi ni nini?
Asanteni.
Kuna siku nimesafiri kwenye bus la ABC kwenda Iringa, mtu mmoja alipandia gari Chalinze, akaomba chupa za maji kwa watu kadhaa akakaa siti ya nyuma kabisa, kufika Mikumi mbugani akatupa chupa nje watu wa patrol wakalifukuzia basi wakatusimamisha wakasema kuna chupa ilirushwa hidhadhini kinyume na sheria na ilikuwa imetokea dirisha la nyuma kabisa na ilikuwa na mikojo, walipokwend huko ilikotokea chupa wakamkuta jamaa ana chupa zingine mbili zimejaa mikojo alikuwa anasubiri kuzitupa nje, wakashuka naye
 
Ni ajabu kwa sababu wewe hujawahi kukojoa kwenye kopo.
Siyo dalili ya woga, ni uvivu na uchovu.
Kukojoa kwenye makopo ni desturi iliyokuwepo, iliyopo na itakayokuwepo, ipo kwa sababu za kiusalama na kuokoa muda.
Usomi isiwe tiketi ya kifungo cha kutofanya mambo mengine.
Eti ni desturi na kuokoa muda hahahahahahaha Jf kuna vituko!
 
Back
Top Bottom