Kukojoa kwenye chupa yenye mfuniko, halafu kila saa inafungwa mfuniko, kuna athari yoyote?

Duniani kuna maajabu/vituko sana. Kushuka kitandani mtu anashindwa!!!!??
Mnaoshangaa kukojoa kwenye chupa ninyi ni mambo safi, mnaona jambo la ajabu mtu kukojoa kwenye chupa AU hamshikwi na haja ndogo mara kwa mara, ukibanwa na mkojo kila wakati lazima utaona kero kwenda chooni, itakupelekea utafute kopo.
 
Nnapokomenti hapa mi nina dumu la 5 litres mimi mpaka mchana nakojolea hapa.Naona uvivu kwenda nje.Nimezoeshwa na mama yangu kule Usangi milimani mana usiku baridi.Na napata starehe sana kukojoa kwa dumu.MADA.hakuna madhara yoyote alimradi uwe unamwaga kila asubuhi na kuosha kwa maji sabuni.
 
Kuna sehemu kutoka nje usiku utakutana na vitu vya ajabu sana nje so MTU anaamua kuwa na chupa pembeni. Sio ushamba unaepuka mambo mengi ya usiku asee usiku huwa kuna vitu vingi vya ajabu km hujawahi kutana navyo huwezi jua ila ndo hivo.
 
Khaa! nimesoma coment zote ajabu sijaona aliyempa jibu mtoa mada zaidi ya kubishana tuu sio uungwana kabisa.
 
Kuna siku nimesafiri kwenye bus la ABC kwenda Iringa, mtu mmoja alipandia gari Chalinze, akaomba chupa za maji kwa watu kadhaa akakaa siti ya nyuma kabisa, kufika Mikumi mbugani akatupa chupa nje watu wa patrol wakalifukuzia basi wakatusimamisha wakasema kuna chupa ilirushwa hidhadhini kinyume na sheria na ilikuwa imetokea dirisha la nyuma kabisa na ilikuwa na mikojo, walipokwend huko ilikotokea chupa wakamkuta jamaa ana chupa zingine mbili zimejaa mikojo alikuwa anasubiri kuzitupa nje, wakashuka naye
 
Eti ni desturi na kuokoa muda hahahahahahaha Jf kuna vituko!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…