Mfamaji
JF-Expert Member
- Nov 6, 2007
- 6,630
- 1,945
Wadau wa jukwaa hili salaam zenu wote,
Leo ni nane nane na wengine tumetembelea au tuna mpango wa kutembelea maonyesho mbali mbali ya wakulima. Kwenye banda moja mfanyabiashara/mkulima huyu ananidokeza changamoto alizokumbana nazo hususani kutoka benki.
Alianzisha kilimo cha green house na akapewa mkopo ambao umegawanyika mara 2. Moja ni wa kununua green house zenyewe na pili ni mtaji wa kuendesha yaani kununua pembejeo nk. Mkataba ukasainiwa. Baada ya kufunga green house ndio apewe sehemu ya pili ya mkopo huo.
Ajabu mpaka sasa mwaka na nusu hajapaptiwa huku kila uchao interest zinaingizwa. Amechanyikiwa na mbaya zaidi wanamtishia kufuta mkopo na kudai hela zao.Benk hiyo haijampa sababu ya kutotoa sehemu ya mkopo uliyobaki licha ya kudai maelezo lakini hajafua dafu. Wale vijana wa benki wanachungulia hapo kila siku.
Hii ndio bongo bana. Niliwahi kusikia jinsi benk zinavyopanga kuuza mradi wako toka siku unavyoomba mkopo sikuamini. Sasa huu hapa ni ushuhda mubashara. Jamani kamaa kuna aliyepitia tanuru hili amshari huyu ndugu.
Nawasilisha.