Kukopa benki na changamoto zake

Kukopa benki na changamoto zake

Mfamaji

JF-Expert Member
Joined
Nov 6, 2007
Posts
6,630
Reaction score
1,945
Wadau wa jukwaa hili salaam zenu wote,

Leo ni nane nane na wengine tumetembelea au tuna mpango wa kutembelea maonyesho mbali mbali ya wakulima. Kwenye banda moja mfanyabiashara/mkulima huyu ananidokeza changamoto alizokumbana nazo hususani kutoka benki.

Alianzisha kilimo cha green house na akapewa mkopo ambao umegawanyika mara 2. Moja ni wa kununua green house zenyewe na pili ni mtaji wa kuendesha yaani kununua pembejeo nk. Mkataba ukasainiwa. Baada ya kufunga green house ndio apewe sehemu ya pili ya mkopo huo.

Ajabu mpaka sasa mwaka na nusu hajapaptiwa huku kila uchao interest zinaingizwa. Amechanyikiwa na mbaya zaidi wanamtishia kufuta mkopo na kudai hela zao.Benk hiyo haijampa sababu ya kutotoa sehemu ya mkopo uliyobaki licha ya kudai maelezo lakini hajafua dafu. Wale vijana wa benki wanachungulia hapo kila siku.

Hii ndio bongo bana. Niliwahi kusikia jinsi benk zinavyopanga kuuza mradi wako toka siku unavyoomba mkopo sikuamini. Sasa huu hapa ni ushuhda mubashara. Jamani kamaa kuna aliyepitia tanuru hili amshari huyu ndugu.

Nawasilisha.
 
Ungetusaidia ni Bank [emoji542] gani mkuu, ili tujue pa kuanzia kwanza

Mimi ni third party kwa hiyo kusema ni ipi nitakuwa nimekiuka. Japo wengi mtashngaa lakini ni kweli tupu.
 
Sasa kama unaficha ficha utakua hujatusaidia kitu na wala watu hawatokupa ushauri nini cha kufanya watakupuuza,kwanini ufiche wakati umefikwa na tatizo? Hujiamini hata kwa ID fake unayotumia? Au huo mkopo wa aina hiyo ulikopeshwa peke yako kwenye hiyo bank kwaiyo ukiwataja tu watakujua kua ni wewe

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kusema na ukweli bank zetu sio rafiki kihivyo yani kwanza hizou collateral sio za nchi hii kama kijana unataka kulima na hauna mtaji unaambiwa uilete hati ya nyumba unaitolea wapi sasa

Argue don't shout
 
Kijana Benki za kiislam ndio solution kwa dunia ya sasa Islamic Banking system, hakuna riba za kitwahut
 
Hii thredi ingekua ni ya mabo ya kijinga ya kule mmu au chit and chat, ingekuwa pg ya 40 ivi sasa.

Anyway, tz ni ngumu sana kufanikiwa bila magumashi.
SA kupata leseni ya biashara ni hardly 30 min, ila tz ni zaidi ya miezi 4.
Mkuu acha kuudanganya umma mimi leseni ya biashara nilipata ndani ya siku moja tu muhimu ni kuhakikisha unafahamu taratibu za biashara husika unayotaka kuanzisha

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mimi ni third party kwa hiyo kusema ni ipi nitakuwa nimekiuka. Japo wengi mtashngaa lakini ni kweli tupu.
Hebu achag mambo ya kitoto na wewe........wewe unawafixha kwasababu gani?! Wao si wamekiuka utaratibu......kwa misingi hiyo hiyo na wewe ukiuke utaratibu maana hata sioni haja ya kuwaficha mapakashume hao......hebu wataje hapa halafu tuone watakufanya nini?!

SONY Xperia Z5 Premium
 
Mkuu acha kuudanganya umma mimi leseni ya biashara nilipata ndani ya siku moja tu muhimu ni kuhakikisha unafahamu taratibu za biashara husika unayotaka kuanzisha

Sent using Jamii Forums mobile app
Una uhakika aliyekupatia hiyo leseni hakuwa ndigu au jamaa yako.....?! Maana usitake kutetea mambo ambayo wengine tumeshayashuhudia

SONY Xperia Z5 Premium
 
Nampa pole sana mdau aliyepata hayo masaibu maana hata mkopo utaulipaje sasa wakati biashara haijasimama. Kwa mawazo yangu ni kwamba unapokopa kuanzishaia biashara hakikisha tayari una asilimia fulani ya pesa ambayo umeipata kwa savings zako. Mkopo wa asilimia mia wa wewe bila kuchangia chochote huwa unaleta shida baadaye..
 
Mkuu acha kuudanganya umma mimi leseni ya biashara nilipata ndani ya siku moja tu muhimu ni kuhakikisha unafahamu taratibu za biashara husika unayotaka kuanzisha

Sent using Jamii Forums mobile app
Baadhi ya sehemu hapa tz kupata tin # ni matatizo.
Hapo ndo suala LA leseni linapokuwa kazi, unakuta mkoa una kituo kimoja tu cha kutolea tin
 
Back
Top Bottom