Kukosa mishahara sekta binafsi: Ni muda wa Social Security Funds kutoa hata 30% ili watu wajikimu

Kukosa mishahara sekta binafsi: Ni muda wa Social Security Funds kutoa hata 30% ili watu wajikimu

mbutamaseko

JF-Expert Member
Joined
Nov 20, 2018
Posts
743
Reaction score
1,071
Kulingana na yanayotokea kwa watu kukosa mishahara mfano shule binafsi kama tusiime, st Anne Marie na zingine nyingi ilhali watumishi hao wanachangia vizuri tu nssf. Serikali aioni haja ya kuruhusu watu wachukue sehemu ya asilimia 30 tu ya mafao yao ili kujilinda kipindi hiki cha janga la covid19. Lengo kuu la mifuko hii in kuihifadhi jamii.

Na ni dhahiri kwa hali ilivyo wanahitaji hifadhi nyakati hizi kwani waajiriwa hawana fedha na waajiri hawana fedha za kuwalipa ni vyema wapewe walizokuwa wanatunza nssf ili nazo ziwatunze na ndio malengo. Au kama kuna watu wamezitafuna basi wanachama waambiwe. Kama kweli hii ni serikali ya wanyonge lazima italifanyia kazi suala hili tofauti na hapo itakuwa ni kuigiza tu kujali wanyonge.

Na fedha zitoke ndani ya wiki au sikutatu kulingana na hali ya dhalura iliyopo.

WABUNGE MKO WAPI? HIZI NDIO ZILIKUWA HOJA ZA DHARURA KUJADILIWA BUNGENI SIO UPINZANI KUWAZA KUPINGA TU KILA KITU NA WA CHAMA TAWALA KUSIFIA MPAKA UJINGA.

Fanyieni kazi haya
 
Halafu ukistaafu umeshazeeka na kuchoka utakubali malipo ya uzeeni pungufu 30%?
 
Sheria inasemaje? Ni wazo mzuri lakini ungeanza kwa kuwaomba wabunge wapeleke muswada bungeni wenye mapendekezo Haya,maana sheria ya mafao haitambui hili swala

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hata wao watawala wanatamani sana kufanya hivyo ila hizo hela zipo sasa mkuu?
 
Hawa wabunge wa CCM na serikali yao ya kishetani na kibinafsi unadhani itawasikiliza. This is dona kantri
 
Hawa wabunge wa ccm na serikali yao ya kishetani na kibinafsi unadhani itawasikiliza.....this is dona kantri
Itawabidi tu wasikie bila kujali wako vp . nao pia wanaitegemea jamii ili waishi. sasa bila kuilinda tena kwa fedha zao wenyewe!!! Hawatakuwa waungwana duniani na mbinguni. Wataua mpaka ndugu na jamaa zao na hats wao pia. Hii kitu iachiwe no matter what.
 
Hata wao watawala wanatamani sana kufanya hivyo ila hizo hela zipo sasa mkuu?
Ziende wapi tena? Kama hazipo basi mwajiri mkuu atoke atufafanulie ziko wapi. Au atukopee sehemu kisha zetu zikirudi atarudisha. Hivyo tu
 
Sheria inasemaje? Ni wazo mzuri lakini ungeanza kwa kuwaomba wabunge wapeleke muswada bungeni wenye mapendekezo Haya,maana sheria ya mafao haitambui hili swala

Sent using Jamii Forums mobile app
Hii ni dharura mkuu kwa maslahi ya nchi. Sio kila kitu mpaka kijadiliwe. Kwani sharia na miongozo ya wizara ya elimu inasemaje kuhusu kufunga mashule na vyuo? Mbona masomo yalisitishwa? Kuna mswada ulieenda bungeni kwanza? Hii dharura mkuu kwa maslahi mapana ya nchi.
 
[emoji16][emoji16][emoji16][emoji16]shida ni kwamba hata hiyo 30% haipo.

Watu wamejengea mijumba ya gharama kuuzia watu, watu hawanunui,w ala hawapangi bei kubwa mno, matokeo yake mkwanja ni kana umezikwa ukaliwa na mchwa.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Barikiwa sana huku secta binafsi hali ni mbya wakat huo huo ndo wachangia wazuri wa mifuko hii
Nadhan muda huu ndo ilikuwa nyakati mwafaka kumjali mteja

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kama usipopewa sasa hivi utakufa na njaa hata huko uzeeni hufiki ili kupewa 100%. Ni vyema 30% ya sasa hivi ilikuokoa maisha kuliko 100% ambayo itakukuta ushavuta kamba... Kwa hili hakuna mwenye hoja

Mifuko haiendeshwi kwa hisia na matakwa binafsi, bali kwa Mahesabu, kwamba ukipewa sasa hivi 30% ukistaafu kutakuwa hakuna hela ya kukupa kwa maana ulishaichukuwa nikimaanisha kama kila mtu akitaka apewe 30% sasa hivi, wanaostaafu watakosa
 
Kwahiyo bora afe sasaiv? Akili mnamuachiaga nani? Rubbish


Mifuko haiendeshwi kwa hisia na matakwa binafsi bali ni Hisabati yaani wanakokotoa na ili Mahesabu yakubali na kila anayekatwa aweze kulipwa akistaafu ndio maana wanafanya hivyo, kuna sababu kwa nini inaitwa "akiba ya uzeeni” hawakuita akiba ya ukipata tatizo.
 
Back
Top Bottom