adrenaline
JF-Expert Member
- Jun 17, 2015
- 3,152
- 4,843
Mifuko hiyo ya Jamii nafuu hata ya Makampuni ya Kubett
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Mpaka sasa Malipo ya mkupuo kwa wastaafu chini ya mfuko wa nssf ni asilimia 25 tu ya mafao yako. Kwa hiyo kusema upewe kwa sasa kiasi ambacho hata wastaafu hawapewi ni ndoto za mchana. Huko nssf ni kilio!! Kile kikokotoo kilichopigiwa kelele, huko nssf ndicho kinachotamba! Hata zoezi LA kuwahamishia PSSSF watumishi wa umma waliokuwa NSSF halijasaidia maana mtumishi huyo akistaafu bado nssf ndio wanaohusika kumlipa mafao yake kwa kikokotoo hicho hicho ambacho kililalamikiwa na rais akakisitisha! Eti wanasema nssf ndiko alikolipia michango yake mingi!!Kulingana na yanayotokea kwa watu kukosa mishahara mfano shule binafsi kama tusiime, st Anne Marie na zingine nyingi ilhali watumishi hao wanachangia vizuri tu nssf. Serikali aioni haja ya kuruhusu watu wachukue sehemu ya asilimia 30 tu ya mafao yao ili kujilinda kipindi hiki cha janga la covid19. Lengo kuu la mifuko hii in kuihifadhi jamii.
Na ni dhahiri kwa hali ilivyo wanahitaji hifadhi nyakati hizi kwani waajiriwa hawana fedha na waajiri hawana fedha za kuwalipa ni vyema wapewe walizokuwa wanatunza nssf ili nazo ziwatunze na ndio malengo. Au kama kuna watu wamezitafuna basi wanachama waambiwe. Kama kweli hii ni serikali ya wanyonge lazima italifanyia kazi suala hili tofauti na hapo itakuwa ni kuigiza tu kujali wanyonge.
Na fedha zitoke ndani ya wiki au sikutatu kulingana na hali ya dhalura iliyopo.
WABUNGE MKO WAPI? HIZI NDIO ZILIKUWA HOJA ZA DHARURA KUJADILIWA BUNGENI SIO UPINZANI KUWAZA KUPINGA TU KILA KITU NA WA CHAMA TAWALA KUSIFIA MPAKA UJINGA.
Fanyieni kazi haya
Kama unayoyaongea ni ya ukweli basi hii mifuko haina maana kabisa.. Yaani mstaafu anakosa pesa ya kulipwa anasubiri mpaka wanachama wachange ndio apewe? Kwani michango take aliyokuwa anachanga inakuwa imeenda wapi wakati huo mpaka asubiri ya wengine? Kufiria kwa makini hapo utaona eidha hueleweki au hujielewi ama kuelewa vizuri unachokiongeaHilo ni swala lingine, angalau bado wanachochote cha kuwalipa Wastaafu ambao wameshachangia kwa miaka mingi klk huyu ambaye hajachangia sana na bado hajastaafu kutaka kulipwa.
Kama unayoyaongea ni ya ukweli basi hii mifuko haina maana kabisa.. Yaani mstaafu anakosa pesa ya kulipwa anasubiri mpaka wanachama wachange ndio apewe? Kwani michango take aliyokuwa anachanga inakuwa imeenda wapi wakati huo mpaka asubiri ya wengine? Kufiria kwa makini hapo utaona eidha hueleweki au hujielewi ama kuelewa vizuri unachokiongea
Labda nieleweshe unaelewa inafanyaje kazi kiasi cha kukosa mafao ya kumlipa mstaafu na kutegemea michango wa wanachama wapya.? Ni michango ya mstaafu anayedai inakuwa imepotelea wp?Labda wewe ndio hauelewi jinsi hii mifuko inavyofanya kazi, siyo kwamba unachokiweka ndicho unachokipata hiyo siyo Benki kwanza hata Benki yenyewe ukiweka laki watakukata kiasi.
Jielimishe kwanza jinsi mifuko inavyofanya kazi ndio uongee.
Labda nieleweshe unaelewa inafanyaje kazi kiasi cha kukosa mafao ya kumlipa mstaafu na kutegemea michango wa wanachama wapya.? Ni michango ya mstaafu anayedai inakuwa imepotelea wp?
Kipi bora, upate 30 % now ikusaidie kununua barakoa, sanitizers na lishe bora kwa familia yako au ufe na hiyo pesa usikie ukiwa kaburini??Halafu ukistaafu umeshazeeka na kuchoka utakubali malipo ya uzeeni pungufu 30%?
Kipi bora, upate 30 % now ikusaidie kununua barakoa, sanitizers na lishe bora kwa familia yako au ufe na hiyo pesa usikie ukiwa kaburini??
Sent using Jamii Forums mobile app
Mifuko haiendeshwi kwa hisia na matakwa binafsi, bali kwa Mahesabu, kwamba ukipewa sasa hivi 30% ukistaafu kutakuwa hakuna hela ya kukupa kwa maana ulishaichukuwa nikimaanisha kama kila mtu akitaka apewe 30% sasa hivi, wanaostaafu watakosa