Kukosekana kwa intaneti: Kebo moja ya intaneti ilikatwa mapema Jumapili katika Mji wa bandari wa Afrika wa Durban, je ni hujuma?

Kukosekana kwa intaneti: Kebo moja ya intaneti ilikatwa mapema Jumapili katika Mji wa bandari wa Afrika wa Durban, je ni hujuma?

Watumiaji wa intaneti nchini Tanzania, Kenya, Rwanda na Uganda wamekuwa wakilalamikia ukosefu wa intaneti huku watoa huduma kote Afrika Mashariki wakikiri kumekuwa na tatizo.

View attachment 2989668

Wamesema wanajitahidi kurekebisha tatizo hilo.

Huduma hiyo ilikumbwa na hitilafu katika nyaya za chini ya bahari zinazounganisha eneo hilo na dunia nzima kupitia Afrika Kusini, mtaalam wa sekta hiyo Ben Roberts aliambia BBC.

Hali kama hiyo ilishuhudiwa katika sehemu za Magharibi na Kusini mwa Afrika mwezi Machi.

Cloudflare Radar, ambayo inafuatilia uunganishaji wa intaneti, imesema kuwa Tanzania ni miongoni mwa nchi zilizoathirika zaidi na trafiki kushuka hadi asilimia 30 ya viwango vinavyotarajiwa.

Gazeti la Citizen la Tanzania lilieleza kilichotokea kama "kuzimwa kwa mtandao ambao kumeathiri njia kuu za mtandao".

Safaricom, pia nchini Kenya, ilisema "inakabiliwa na changamoto". Airtel Uganda imesema inafahamu kuhusu "huduma ya mtandao ya mara kwa mara".

Na MTN Rwanda ilisema kulikuwa na "suala la uharibifu wa uhusiano wa kimataifa". Malawi, Msumbiji na Madagascar pia zimeathirika kulingana na Cloudflare Radar.

Bw Roberts, kutoka kampuni ya pan-Africa ya Liquid Intelligent Technologies, alisema kuwa amethibitisha kuwa kebo moja inayopitia kando ya pwani ya Afrika Mashariki, inayojulikana kama Eassy, ilikuwa imekatwa mapema Jumapili katika Mji wa bandari wa Afrika wa Durban.

Kebo nyingine pia ilikatwa. Alipuuzilia mbali uwezekano kwamba huenda ni hujuma na uongeza kuha hali kama hiyo wakati mwingine hutokea kwa bahati mbaya.

Kebo zingine zinazounganisha Afrika Mashariki na Ulaya pia zinapatikana na hatua kwa hatua huduma inapaswa kuboreshwa kwani data inapitishwa tena.

Lakini kwa vile makampuni mengi makubwa yana vituo vya data nchini Afrika Kusini uharibifu wa kiungo muhimu ambacho Eassy hutoa ulikuwa na athari kubwa.

Chanzo: BBC
SA kuna namna wanatumika na maraifa mrengo wa kulia
 
Hatari sana, muhimu kuwa na mbinu mbadala, mpaka Sasa mtandao ya kubeti upande wa kasino haufanyi kazi, mpaka Sasa nimeshindwa kucheza kasino online
Mkuu, siku hizi madubwi yapo mpaka masaki, ungetoka nje ukaweke mzigo.
 
Swali ni kwamba kwanini hatuna redundant connection ya kupita middle east? Haiwezekani zote mbili kukatika mara 1
 
Screenshot_2024-05-13-21-38-05-61_6012fa4d4ddec268fc5c7112cbb265e7.jpg
 
MtamaMchungu

...network has redundancy implemented through multiple submarine cables connecting the North towards Europe and South towards South Africa along the East coast of Africa.

In February 2024, a submarine fiber cut occurred between Djibouti and Jeddah, impacting some of our traffic capacity to Europe. This subsea fault is yet to be resolved due to security concerns along the Red Sea.

On May 12th, 2024, another subsea fault occurred off the coast of South Africa near Mtunzini impairing all subsea capacity between East Africa and South Africa. An undersea cable repair vessel has been mobilized, and restoration efforts may take several days.

These events have resulted in a higher demand for international capacity through Europe, and we are working on activating additional capacities through the available routes to alleviate the impact.
 
Kwanini watanzania huko kwenye masomo ya Sayansi huwa mnasoma nini ?

Lini bara la Afrika litakuwa na uwezo wa kuzalisha yenyewe huduma ya internet bila kutegemea huduma kutoka kwa mzungu ?
Mshamba huwezi kuelewa hapo ulipo ukiambiwa define internet hujui

INSHORT UNAWEZA TENGENEZA NETWORK ILI UPATAE INTERNET LAZIMA UCONNECT NA GLOBAL INTERCONNECTED COMPUTER NETWORKS (INTERNET) SASA HAPO UNAITENGENEZAJE?

KAA KIMYA SIKU NYINGINE
 
MtamaMchungu

...network has redundancy implemented through multiple submarine cables connecting the North towards Europe and South towards South Africa along the East coast of Africa.

In February 2024, a submarine fiber cut occurred between Djibouti and Jeddah, impacting some of our traffic capacity to Europe. This subsea fault is yet to be resolved due to security concerns along the Red Sea.

On May 12th, 2024, another subsea fault occurred off the coast of South Africa near Mtunzini impairing all subsea capacity between East Africa and South Africa. An undersea cable repair vessel has been mobilized, and restoration efforts may take several days.

These events have resulted in a higher demand for international capacity through Europe, and we are working on activating additional capacities through the available routes to alleviate the impact.
Interesting... this is the kind of information that needs to be shared. I could not understand why we didn't have redudant cable and if we had one, why we are not using it.

Thank you
 
Mshamba huwezi kuelewa hapo ulipo ukiambiwa define internet hujui

INSHORT UNAWEZA TENGENEZA NETWORK ILI UPATAE INTERNET LAZIMA UCONNECT NA GLOBAL INTERCONNECTED COMPUTER NETWORKS (INTERNET) SASA HAPO UNAITENGENEZAJE?

KAA KIMYA SIKU NYINGINE
Mueleweshe taratibu mkuu
Uelewa wake mdogo
 
Back
Top Bottom