Kukosekana Utulivu wa Kisiasa na kupaa kwa bei za vyakula duniani

Kukosekana Utulivu wa Kisiasa na kupaa kwa bei za vyakula duniani

Lady Whistledown

JF-Expert Member
Joined
Aug 2, 2021
Posts
1,147
Reaction score
2,008
Bei za bidhaa za kilimo zimekuwa zikifuata mwelekeo wa kupanda kwa sababu ya mwitikio wa serikali duniani dhini ya Covid-19. Bei hizo zilipanda kutokana na vikwazo vya kuuza chakula nje kwa baadhi ya nchi.

Lakini mzozo wa sasa kati ya Urusi na Ukraine umepeleka bei kwenye viwango vipya na vya hatari, hata kuzidi vile vilivyojitokeza mwanzoni kabisa mwa vuguvugu katika nchi za Kiarabu (Arab Spring) na janga la upungufu na kuongezeka kwa gharama za chakula ulimwenguni ambazo zilisababisha madhara makubwa mwaka 2007-2008.

Utafiti wa Shirika la Umoja wa Mataifa la biashara na maendeleo (UNCTAD) ulisema kulikuwa na ongezeko la asilimia 83 la bei za vyakula duniani kati ya 2005 na 2008. Wakati bei ya mahindi ilipanda karibu mara tatu, bei ya ngano iliongezeka asilimia 127, na bei ya mchele iliongezeka kwa asilimia 170 kati ya Januari 2005 na Juni 2008.

Chapisho hilo pia linaeleza kuwa makadirio ya awali ya Chakula na Kilimo Shirika la Umoja wa Mataifa (FAO), ni kuwa bei ya juu ilisukuma watu milioni 40 kwenye baa la njaa mwaka 2008, na kuongeza idadi ya jumla ya wasio na lishe bora watu duniani hadi milioni 963, ikilinganishwa na 923 milioni mwaka 2007. FAO ilionya kwamba mgogoro wa kifedha na kiuchumi uliokuwa ukiendelea ugeweza kuongeza idadi ya watu wanaoishi katika njaa na umaskini.

Ongezeko jipya la bei ni matokeo ya vita vinavyoendelea, ambavyo vinaweza kuathiri utulivu wa kisiasa na usalama wa chakula popote duniani.

Vita vinavyoendelea Ukraine vimekuwa na athari za haraka kwenye soko la chakula duniani kwani Ukraine na Urusi ni wazalishaji wa bidhaa za kilimo ambazo ni muhimu kwa usalama wa chakula, kama vile ngano, shayiri, mahindi pamoja na mafuta ya alizeti na mbegu.

Global Food Price Indexes 2021_22.png

Kielelezo 1: Namna bei ya vyakula inavyopanda duniani tangu mwezi Juni, 2021. Bei zimeonekana kupaa zaidi katika kipindi cha tangu Februari 2022.

Mkurungenzi wa kitengo cha UNCTAD kuhusu mikakati ya utandawazi na maendeleo Richard Kozul-Wright, anasema vita vya Ukraine huenda vikaongeza mivutano ya kisiasa kwenye ngazi ya kimataifa, kuamua sera za kitaifa za fedha, kuongeza madhara ya mfumuko wa bei na kusababisha ongezeko la bei ya mafuta na bidhaa nyingine. Anasema maeneo yote ya uchumi wa dunia yataathiriwa vibaya na mzozo wa Ukraine, wengine zaidi ya wengine.

Ripoti iliyosahihishwa ya UNCTAD kuhusu biashara na maendeleo inakadiria kuwa uchumi wa dunia utapungua kwa asilimia 2.6 mwaka huu wa 2022 kutoka madakirio ya asilimia 3.6 hapo awali. Shirika hilo linasema sababu kuu ya kushusha kwa kiasi kikubwa makadirio ya ukuaji wa uchumi, ni sintofamu inayozunguuka vita nchini Ukraine.

Kiwango cha uharibifu wa kijeshi, muda wa vita na vikwazo dhidi ya Russia, kutaongeza kudorora kwa uchumi unaoendelea ulimwenguni na kudhoofisha afueni iliyoanza kupatikana baada ya janga la Covid 19.

Kwa kuzingatia kuwa nchi nyingi za Kiafrika zinategemea mataifa hayo mawili, Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB) iliweka bayana nia ya kuchangisha $1bn (£759m) katika muda wa wiki moja kusaidia uzalishaji wa kilimo barani Afrika na kulinda bara la Afrika kutokana na uhaba wa chakula unaotokana na uvamizi mgogoro huo.

Somalia, Benin, Misri na Sudan zinaongoza kwenye orodha ya nchi ambazo zinategemea pakubwa Urusi na Ukraine, huku zaidi ya 70% ya ngano yao ikitoka katika mataifa hayo mawili.

“AfDB inaona ongezeko hili la bei ya ngano, mahindi na maharagwe ya soya kama uwezekano wa kuzidisha uhaba wa chakula na kuongeza mfumuko wa bei,” Rais wa AfDB Akinwumi Adesina alisema.
 
Back
Top Bottom