Kuku aina ya Bukini

Kuku aina ya Bukini

CHANG'OMBE

Member
Joined
Jul 22, 2012
Posts
19
Reaction score
6
Habari wanajamvi

Katika pita pita zangu kwenye mitandao nimeona aina ya kuku ambayo sikupata kuisikia - BUKINI. Najua kuwa kuna BATA BUKINI kumbe sasa hata KUKU BUKINI wapo? Kwa wale wanaowafahamu kuku hao ningependa kujuzwa mambo yafuatayo:-

Je, wanasifa gani? Umbile lao, uzazi wao (utagaji mayai), na sifa zake zingine

Je, wanapatikana kwa wingi sehemu gani hapa TZ

Je, kwa Dar es Salaam, Pwani na hata Moro kuna watu wamewafuga? Wako maeneo gani?

Je, bei zao zikoje?

Je, kuna mwenye mawasiliano na wafugaji wa kuku hao?

MSAADA TAFADHALI!!!!

NAWASILISHA
 
HELLO GREAT THINKERS!

Huu mfugo ni mpya kabisa yaani hakuna waliokwishafuga au kuona waliofuga? Tuelimishane jamani
 
mimi nina bata bukini tu
nauza laki mbili mmoja
 
Kuku Bukini,mmmmmhh! Ngoja wadau waje! Labda ni kizazi kipya!
 
Bata laki mbili Smile kwani amekuwa mbuzi katoliki
tena ni vile nimefulia mimi nilimnunua mama yao 2008 elfu tisini mkuu,ni wazuri sio mchezo ,vile tu sina mtu wa kukaa nao vizuri wala nisingeuza mbona!
 
Ahh! Kumbe bukini nilidhani ''bikini'' nikasema hii inakua version mpya!
 
1216330378_72f279df24.jpg
Cat+Duck+Photoshop+Animal+Hybrid+Funny+LOLcat+Picture.jpg

funny_crocodile_duck_photoshop.jpg
Amherstxgolden.jpg

Grouse_2-400x600.jpg
JR73057-big-chicken.jpg

Sijawahi kusikia kuhusu kuku bukini, sidhani kama yupo.
 
Kwa wadau wote mliochangia mada yangu, kama mnavyoona hata mimi nimeonyesha mshangaowa kuwepo kwa kuku hao. kuku BUKINI na KUCHi wametajwa katika Hotuba ya Bajeti ya Wizara ya Mifugo na Uvuvi ya mwaka 2011/2012 na sijawahi kuwa na mawasiliano na watu wa Wizara hiyo.

Pengine labda walimaanisha BATA BUKINI.
 
Hivi wale kuku wasio na mkia/Wasio na manyoya marefu ya mkiani huitwaje ?

Nadhani kule Dar es Salaam Zoo kuku hao wapo, wanaitwa VINYOYA, ila wale jamaa hawawauzi bali ni wamewafuga kwa ajili ya kitoweo chao wenyewe. Na wwalisema waliletewa na watu wa mikoani (bila kuitaja).
 
Nakumbuka nilipokuwa mdogo kijijini tulikua na hao kuku , lakini hawakuwa wengi.
unaweza kuta ni mmoja kati kuku 10 au 20, na tulikuwa tukiwaita Bukini.
 
bukini ni ni bata na hawa mm binafsi nina wafuga. wako kama bata wa kawaida ila tu sio wanene na wazembe kama bata wa kawaida. wao wako sharp sana na hutaga mayai mengi zaid.

sifa yao mbaya ni wakali sana sana huweza kula mtu usipokuwa makini ila wakikuzoea basi hawana shida na wewe.

kwa dar soko lao kuwa ni kwa wachina na hununua hadi sh 80000 mmoja. utamiaji wao ni kama bata wa kawaida tu na vifaranga vyao hukua bila hofu hawana magonjwa sana na wanastahimili hali ngumu ingawa wwanapenda zaid pumba na majani
 
Kwa wadau wote mliochangia mada yangu, kama mnavyoona hata mimi nimeonyesha mshangaowa kuwepo kwa kuku hao. kuku BUKINI na KUCHi wametajwa katika Hotuba ya Bajeti ya Wizara ya Mifugo na Uvuvi ya mwaka 2011/2012 na sijawahi kuwa na mawasiliano na watu wa Wizara hiyo.

Pengine labda walimaanisha BATA BUKINI.

kuku bukini ni wale kuku ambao ni kama hawana mkia kifupi manyoya ya mkiani ni mafupi mno ni wafupi na ni wanene haswa niliwaona mkurunga ila sijawahi kuwafuga
 
Habari wanajamvi

Katika pita pita zangu kwenye mitandao nimeona aina ya kuku ambayo sikupata kuisikia - BUKINI. Najua kuwa kuna BATA BUKINI kumbe sasa hata KUKU BUKINI wapo? Kwa wale wanaowafahamu kuku hao ningependa kujuzwa mambo yafuatayo:-

Je, wanasifa gani? Umbile lao, uzazi wao (utagaji mayai), na sifa zake zingine

Je, wanapatikana kwa wingi sehemu gani hapa TZ

Je, kwa Dar es Salaam, Pwani na hata Moro kuna watu wamewafuga? Wako maeneo gani?

Je, bei zao zikoje?

Je, kuna mwenye mawasiliano na wafugaji wa kuku hao?

MSAADA TAFADHALI!!!!
NAWASILISHA
kuku bukini wapo na ni kuku wa kienyeji.ni mwenye umbo fupi na nene.ana upanga mrefu.hana mkia na ana Miguu mifupi isiyo na manyoya.hupatikana kwa wingi Mikoa ya tanga,pwani,Kilimanjaro,na singida.
 
Mimi nimewahi kusikia CHANG'OMBE ila CHAKUKU sijawahi kusikia

Wajameni hili ni jukwaa la ujasiriamali, mtu anapouliza au kutaka kufahamishwa jambo fulani ana maana yake. Sasa ukiona huna cha kusema afadhali kusoma na kujiondokea tu kuliko kuandika mambo yasiyoeleweka. Tunaulizia habari hizi na zile ili tufanye Ujasiriamali. Kuna watu wameeleza kuwa hakuna Kuku Bukini lakini MAMA TIMMY amesema wapo na akaeleza sifa zao. Unadhani tunauliza kwa kukurupuka tu?
 
Back
Top Bottom