Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Maelezo safiNadhan ufugaj ni asili tu..toka naanza maisha nilianza kufuga ila sikua nafuga wa kuuza..kwahiyo nilikua nafuga ilimrad nipate kuku wa kula...so hata chanjo sikua nawapa..kwahiyo kuku wemgi wakawa wanarest in peace .sikua najali as nikitaka kuku napata wa kuchinja..
Last yr nikakutana na mama anafuga kuku wengi balaa..tena ana eneo dogo tu huko kahama...nikajiona mie mjinga.maana nna eneo kubwa kila sk najaza maua tu..so jan nikaanza okota mayai siwawekei kuku walalie naenda kautotoresha napata vifaranga vingi zaidi
Nawapa chanjo zote..7 dys,14 dys,21dys na wakifikisha 3mths!
Nafuga kienyeji kwasababu its a SIDE HUSTLE....sio biashara nayotegemea kwamba iniweke mjini ..
Niliwah fuga broiler miaka hiyo wakafa wote nilianza kipindi kibaya nilikua [emoji1768] kwahyo usimamizi ukawa F,
Changamoto nnayopata kipinfi hiki cha mvua kuku zimekufa aisee ...lakini naambiwa ni kwasababu ya hali ya hewa,
Ulishaji nawapa chakula special wanadai ukiwapa pumba tu wanadumaa..kwahuo wakiwa wadogo had mwez 1 nawapa kile chao special starter wakimaliza hicho nawabadilishia..
Changamoto nnayokumbana nayo nimeambiwa banda ni dogo coz kila wk napokea kuku...kwahyo wanabanana...ndo nikaambiwa pia sababu ya kufariki ..kwahyo nimewakatia vizimba nikaweka singboad kutenganisha ukiwamix wakubwa na wadogi wanaonewa sana wanang'atwa sana .na wanamaliziwa msos na wakubwa .yaan usiwamix waliofikisha 2wks na wapya wa siku 1 ..ni headache kwakweli...so this wk ninastop kupeleka mayai nikomae nao hawa kwanza,
La mwisho nilinunua pia hawa machotara kama kuku 40[emoji119][emoji119][emoji119] chotara anakula usk mzima..kwahyo changamoto ni hiyo wanakula mno mno mno afu wanavurugu balaa ....hawa niliamua kumix ili nipate mbegu fulan maana nna kuchi pia...kwakweki wanakula sijapata kuona na kilo 1 nanunua 1300! Kuku kirnyrji 10 wadogo wanakula kilo 1 kwa siku 2 ..chotara masaa3 hakuna msosi!
Kuku wa kienyeji siyo wazuri kibiashara , kuku wa kibiashara ni wale wa mayai na wale wa nyama.Samahani kw nini asifuge wa kienyeji umeona nini mkuu
Kama wastani wa gharama unazotoa kuhudumia kuku ni ndogo kuliko mauzo unayopata hao ni WA biashara tafadhali zingatia Muda unapokokotoa faida!Hv ni kweli kuwa kuku wa kienyeji si kuku wa biashara?
Posho ndio nini? Unamuuza Broiler kwa 10,000 akiwa na umri gani?Kama unataka kufuga wa kienyeji nakushauri hivi nunua hata 100 wakiwa wamekua kua wapige posho then watoe .Kwa huku nilipo nilikuwa naletewa wasize yakati kwa buku 4 mi nawapa posho na dawa miezi 4 nawasukuma sokoni kwa 10 hakuna kuchagua we beba tu Kama una 10 lako.Hii kazi ilinishinda kutokana na ulevi na madeni.Ila si haba.
Posho=Chakula Cha kuku, broiler sina uzoefu nao nimezungumza wakienyeji.Posho ndio nini? Unamuuza Broiler kwa 10,000 akiwa na umri gani?
Ok hapo nimekupata mkuu. Posho mfuko wa 50kg unauzwa sh.ngapi?Posho=Chakula Cha kuku, broiler sina uzoefu nao nimezungumza wakienyeji.
Kwa wakienyeji unatengeneza mwenyewe tu.Ok hapo nimekupata mkuu. Posho mfuko wa 50kg unauzwa sh.ngapi?
Nikianza na 100 pure layers wale wekundu.Je itafaa?Kama una soko la uhakika fuga kuku wa nyama broiler.
Kama hauna uhakika wa soko la kuku wa nyama fuga kuku wa mayai layers.
Usithubutu wala kujaribu kufuga kibiashara kuku wa pure kienyeji.
Ila kama upo makini kiufugaji na unataka mafanikio na mtaji wa kutosha unao,eneo zuri la kufuga unalo basi fuga kuku wa mayai my friend,angalau wasipungue kuku wa mayai kuanzia 1000 hivi utakula mema ya nchi mpaka utakinai.
Wa SUA mbona wanafungua lodge na vibanda vya kuonyesha movie na kuuza series?Ukitaka kuwa precise, basi unatakiwa kuonana na watu wa Animal Science kama wale wa SUA! Utaeleweshwa kwa saa chache tu, na utaelewa!!
Sawa mkuu ila kumbuka soko lake linategemea huko mkoa gani..mfano Kagera,Shinyanga,Tabora bado watu wanapenda kuku wa kienyeji ata chotara kwa kiasi flani.Pesa ya haraka fuga hao wa nyamaView attachment 1793995View attachment 1793997
Siyo kila mhitimu wa sua kasomea kilimo au ufugaji.Wa SUA mbona wanafungua lodge na vibanda vya kuonyesha movie na kuuza series?
Yeah upo sahihi,Yani Hawa ukiwa nje ya mji mashambani huko wanajitaftia wenyewe chakula sio mpaka ununueBwana sikia ndugu yangu usitake mbwembwe usitake pesa za haraka,Ndio kila mtu anahitaji pesa ila ki ufupi mpaka sasa sijaona ufugaji ambao una pesa tena pesa kweli kweli kama ufugaji wa kuku wa kienyeji.
Kuku wa mayai kila mtu anafuga,mnakutana kwa Mangi kila mtu na mitrei yake kibao hamjui wakumuuzia,Kuku wa nyama kila mtu anafuga imefika hatua kuku mzima anauzwa 4000 (hiii ni nini eti) tusifate mkumbo kwenye ufugaji SOKO litakua gumu na hivi makuku yenyewe ya kisasa,mayai yenyewe ya kisasa (stress tupu).
Hela ya kweli wajuba wanakwambia REAL MONEY imejificha kwenye mabawa ya kuku wa kienyeji,kuku wa kienyeji ni pesa Ni gold inayotembea,Ujue namna ya kumfuga/kumlea hadi kupata product tamu.
Haya ni mawazo yangu na ushauri wangu,kama kweli unataka pesa isiyo na stress kwa kiasi kikubwa basi ufugaji pekee wa ki don wa ki pofa ni wa kuku wa kienyeji.
Tafuta mfanyabiashara/Mfugaji wakuku wa kienyeji alie karibu yako akumegee siri usizojua,usiende omba ushauri wa kufuga kuku wa kienyeji kwa mfuga broiler au kuku wa mayai.