Kuku huyu ananishangaza!

Kuku huyu ananishangaza!

MT255

JF-Expert Member
Joined
May 3, 2012
Posts
3,606
Reaction score
4,914
Habari wana jamvi....katika harakati za kujiongezea kipato nina biashara yangu ya kufuga kuku wa kienyeji shambani kwangu wapatao 120 hivi....tatizo linalonishangaza nimekuwa napata taarifa kwa kuwepo mayai madogo madogo kama ya ndege lakini yanafanana kabisa na mayai ya kuku....na sio mara mmoja hii hali inajirudia rudia pale bandani...baada ya kuuliza kwa baadhi ya watu niliambiwa ni ya kuku anataga sasa nauliza kwa yoyote anaefahamu tatizo nini mpaka kuku anataga mayai kama ya ndege?
Nawasilisha
 
Attachments

  • 1394863367281.jpg
    1394863367281.jpg
    31.5 KB · Views: 379
kuku anataga mayai kama ya ndege? kwani kuku ni mnyama?
. Japo na yy ni jamii ya ndege lakini shida yake imeeleweka. Au ulitaka aseme anataga mayai madogo kama ndege jamii ya njiwa?. Haya basi tusaidie hata mm nahitaji msaada wa jb hilo
 
Hata jogoo pia akikomaa hua anataga,mayai yake yanakua mdoogo tofaut na ya kuku jike
 
Pole Sanaa mjasiriliamali...sasa tafuata mwanamifugo yeyote alie karibu na wewee...upate ushaurii

Nimeamua kulileta hili hapa kwanza nikiamini JF ni uwanja mkubwa sana na naweza pata majibu katika hili
 
Hiyo inategemea na kuku mwenyewe labda anaweza kuwa na umbo dogo, sababu ni nyingi, vipi lishe yao nzuri kama calcium, Sio wote wanataga mayai madogo sana ni mmoja mmoja tu labda ni stress
 
MTOTO WA KUKU mbona nawe mjasiriamali vidole vyako vyaonekana si kama ya binadamu wa kawaida manake ni virefu si kawaida..tupe jibu kwanza katika hili!:mod:
 
Last edited by a moderator:
Best hebu jaribu kule JF doctor unaweza pata mwelekeo, hapa watu wanakuzingua tu, wanaishia kushangaa viganja vyako instead of subject matter.
 
Inawezekana kuna kuku wenye umbo dogo wale wenye miguu mifupi na ni mara ya kwanza kutaga,

Ili kuku watoe mayai ya wastani au makubwa jaribu kuwapa Mashudu utaona Mabadiliko.
 
tuma Pm kwa mamajoe au Kubota hao ndio wataalamu sisi tutakuzingua tu hapa
na kuna wengine kuku huwa anakutana naye kwenye sahani tu !!
 
Last edited by a moderator:
Pole ni chakula hasa virutubisho, kuna vile vimayai vidogo lakini gamba gumu ni chakula na kuna mayai ya kawaida lakini gamba dhaifu ni kukosa calcium. Hata kama ni kienyeji pure jitaidi kuwapa chakula chenye virutubisho vyote muhimu iwapo wanataga.
Habari wana jamvi....katika harakati za kujiongezea kipato nina biashara yangu ya kufuga kuku wa kienyeji shambani kwangu wapatao 120 hivi....tatizo linalonishangaza nimekuwa napata taarifa kwa kuwepo mayai madogo madogo kama ya ndege lakini yanafanana kabisa na mayai ya kuku....na sio mara mmoja hii hali inajirudia rudia pale bandani...baada ya kuuliza kwa baadhi ya watu niliambiwa ni ya kuku anataga sasa nauliza kwa yoyote anaefahamu tatizo nini mpaka kuku anataga mayai kama ya ndege?
Nawasilisha
 
Mama Joe hivyo virutubisho ni aina gani?
na ikiwa kuku wa kienyeji anafugwa tu kwenye banda inapaswa ale nini?
 
Last edited by a moderator:
Back
Top Bottom