Kuku katotoa vifaranga 24, nifanye nini ili vyote vikue?

Chukua majani ya alovera 3-5 loweka kwenye maji Lita kumi kwa masaa sita hadi kumi na mbili!!wape kwa siku nzima yatakayo baki unamwaga....mfululizo kwa siku saba!itawajengea kinga hasa ya kideri
 
Huyo kuku aliyeatamia mayai 24 ni aina gani? Ana umbo kubwa mno au? Inaonekana ni mbegu nzuri mno
 
Kuku mwenyewe katotoa leo leo!
Kuna tiba/kinga ya kuwafanya vifaranga hao wote wakue?
yaani hata kama kifaranga akifa, afe kwa kuangukiwa na ndoo au jembe, ila sio afe kwa ugonjwa.

NB; Naishi porini, hakuna duka la dawa.
hivyo dawa naomba ziwe za asili, maana kuna kila aina ya mmea hapa
kwa kuanza usiruhusu mama yao azurule nao; kunguru kicheche watawafyeka wote. Wanunulie chakula chick starter walau kilo mbili ama tatu wape; pia siku ya saba wachanje newcastle ( kideri) siku ya 14 Gombolo; Siku ya 21 rudia Newcastle na siku ya 28 rudia Gombolo.

Wiki ya 7 wachanje ndui baada ya hapo rudia chanjo ya kideri kika baada ya miezi 3.

Ongeza vifaranga zaidi kwa kutumia njia ya kisasa ya kutotoresha hakuna haja ya kuku kulakia mayai siku 21; kwa nini? Tutafute kwa ufafanuzi zaidi.

Kuza hiyo iwe chanzo cha kipato pembeni na mshahara; why not?

Tutafute; 0682 231053
 
Write your reply... ^
 
umeuliza swali nyeti sana tena muhimu kweli kweli. Kuku wengi wanaototoa mwisho wa siku hukuza mmo ama wawili tu sijui nini tatizo
Kuhusu kukuza vifaranga wachache ni kwamba vifaranga bila ya wewe ku-control mazingira wataisha wote ni lzm wewe uweke mazingira rafiki kwa wao kukua na hayo mazingira ni dawa Newcastle na gombolo na pia waweke wakae kwenye banda wasiwe nje

Kwa case ya jamaa ya hupo polini hata cjui
 
Mkuu a45 ahsante sana kwa elimu yako.
 
  • Thanks
Reactions: a45
Kuhusu kukuza vifaranga wachache ni kwamba vifaranga bila ya wewe ku-control mazingira wataisha wote ni lzm wewe uweke mazingira rafiki kwa wao kukua na hayo mazingira ni dawa Newcastle na gombolo na pia waweke wakae kwenye banda wasiwe nje

Kwa case ya jamaa ya hupo polini hata cjui
kwa dawa za asili ni zipi?
 
siku 7 baaada ya kuku kutotoa vifaranga wape chanjo ya newcastle. kisha siku ya 14 wape chanjo ya gumboro. rudia tena hivyo siku ya 21 na 28 kisha siku ya 35 wape chanjo ya ndui na waache kwa siku mbili uwape dawa ya minyoo. mengine tuchekiane inbox.
 
Mkuu Nlkua Naomba Msaada wa Majina ya madawa yanayo tumika kuchanja ayo magonjwa apo juu
1.newcastle
2.gumboro
3.ndui
4.na iyo dawa ya minyoo
 
Tafuta chemli (kwa ajili ya joto)
Chakula bora na maji safi.
 
siku 7 baaada ya kuku kutotoa vifaranga wape chanjo ya newcastle. kisha siku ya 14 wape chanjo ya gumboro. rudia tena hivyo siku ya 21 na 28 kisha siku ya 35 wape chanjo ya ndui na waache kwa siku mbili uwape dawa ya minyoo. mengine tuchekiane inbox.
Kwa vifaranga 24 chanjo zote hizo unajua inafik elfu 40 kasoro,ulichotoa ni kizuri ila kwa mtu mwenye vifaranga vingi.
 
Kuku mwenyewe katotoa leo leo!
Kuna tiba/kinga ya kuwafanya vifaranga hao wote wakue?
yaani hata kama kifaranga akifa, afe kwa kuangukiwa na ndoo au jembe, ila sio afe kwa ugonjwa.

NB; Naishi porini, hakuna duka la dawa.
hivyo dawa naomba ziwe za asili, maana kuna kila aina ya mmea hapa
Mchinje jogoo ili kuku ajikite kwenye malezi!!!
 
Kwa vifaranga 24 chanjo zote hizo unajua inafik elfu 40 kasoro,ulichotoa ni kizuri ila kwa mtu mwenye vifaranga vingi.
Mkuu nimekuelewa ila huu ndo utaratibu kwahiyo hauepukiki kama unataka matokeo mazuri. tumezoea kufuga kwa imani bila ya kuzingatia chanjo na pale ugonjwa unapokuja utasikia mfugaji analalamika eti "kuna ugonjwa umepita umemaliza kuku". yatupasa kufanya hivyo haijalishi una vifaranga wawili au 100.
 
Mkuu Nlkua Naomba Msaada wa Majina ya madawa yanayo tumika kuchanja ayo magonjwa apo juu
1.newcastle: Newcastle ni chanjo. nenda duka la mifugo muone daktari wa mifugo akupatie tu mkuu. kifaranga hupewa baada ya siku 7 kuzaliwa na siku ya 21.
2.gumboro: Gumboro vilevile hupewa siku ya 14 na 28 baada ya kuzaliwa.
3.ndui: Chanjo inaitwa fowlpox
4.na iyo dawa ya minyoo: Piperazine

Mkuu angalia majibu yangu hapo in red.
 
Back
Top Bottom