Masomo, ilibidi nisafiri kwenda mbali kwaajili ya masomo halafu sikua na mtu wa kuwaangalia. Ikabidi niuze wote. Ila ukituliza kichwa hao kuku watakutoa kimaisha, utapiga hatua sana. Utakua haukosi 300,000/= au 200,000/= za haraka haraka.
Sema jitahidi uwe unawapa kinga kila baada ya miezi mitatu, magonjwa yanaosumbua kuku hua ni Sotoka, Gumboro na Mafua (Na yote yana kinga zinauzwa madukani) kuna magonjwa mengine kama minyoo sio hatari sanaaa hua wanapona. Ukiweza kuwapa kinga za hayo magonjwa matatu kila baada ya miezi mitatu basi mambo yatakua poa sana.