Habarini ndugu,
Nimekuwa nikifatilia mara nyingi sana mtu unaweza kuletewa hata kuku 10 kama zawadi na ukaamua kuwafuga katika banda la hovyo tu ajabu ni kwamba watazaliana ingali huwapi chakula cha maana zaidi ya mabaki ya ugali na maharage muda mwingine hawaingii hata bandani wanalala nje ila watazaliana vizuri na kutaga mayai ya kutosha(Wanaweza kufika hata 30),
Cha ajabu sasa kuku wale wale ukiamua kuwageuza kuwa Business Project salaleee hapo sasa ndo Vifo, mafua ya Ndege, Mdondo na kila aina ya ugonjwa utawaandama kuku wako bila kusahau kuku kuzila kutaga wengine hufika mbali zaidi kuanza kula mayai yao wenyewe....Paka nao hawabaki nyuma huja na kuanza kuwinda vifaranga yani kila aina ya majanga huanza kupata kuku wako.
Nimekuwa sielewi hili jambo hivi ni nini kipo nyuma ya haya masuala hebu wajuzi wa Ufugaji watuelezee. ANGALIZO: Imani za kishirikina haziruhusiwi kwenye mjadala.
View attachment 3149553