Kuku wa kisasa hawatagi, sasa chanzo chao ni nini?

cumbamalema

JF-Expert Member
Joined
Sep 4, 2024
Posts
366
Reaction score
820
Jamani kwa wajuzi wa mambo naomba mnisaidie, nimezoea kuwaona kuku wa kisasa na huwa hawatagi, swali langu vifaranga vyake vinapatikana vipi?
 
Wapo kuku maalumu waliochaguliwa kitaalum na na kuboreshwa genetically wao kazi yao ni kutaga hao mayai ya broiler tu.

Mayai hayo yakianguliwa tunapata broiler walionyimwa sifa ya kuendeleza kizazi genetically.
 
Mayai hao yakianguliwa tunapata broiler walionyimwa sifa ya kuendeleza kizazi genetically.
Hao kuku umeshawahi kuwaona?Maana kuku wa mayai wakichoka kutaga huwa wanauzwa kwa ajili ya kuliwa, sasa hawa inakuwaje?
 
Wapo kuku maalumu waliochaguliwa kitaalum na na kuboreshwa genetically wao kazi yao ni kutaga hao mayai ya broiler tu.

Mayai hayo yakianguliwa tunapata broiler walionyimwa sifa ya kuendeleza kizazi genetically.
Me ninao broiler niliwafuga Hadi miezi 6 wakaanza kutaga ila utagaji wao ni hafifu, kwenye kuku 10 kwa siku wanaweza kutaga wawili au watatu au wakagoma kabisa
 
Hao kuku umeshawahi kuwaona?Maana kuku wa mayai wakichoka kutaga huwa wanauzwa kwa ajili ya kuliwa, sasa hawa inakuwaje?
Kuna mashamba maalum yana hawa wazazi wa broiler unaowaona kwa kikristo wanaitwa ( parental stock) hawa ndio hutoa mayai ya hawa broiler unaowaona ambao kiuhalisia wao hawawezi kuzaliana tena , na hao parental stock wakikomaa kabisa wanakua wakubwa sana anaweza kujaa kwenye ndoo ndogo
 
Me ninao broiler niliwafuga Hadi miezi 6 wakaanza kutaga ila utagaji wao ni hafifu, kwenye kuku 10 kwa siku wanaweza kutaga wawili au watatu au wakagoma kabisa
Mara nyingi Chakula kinapokosa virutubisho vinavyotakiwa husababisha kuku kutotaga inabyotakiwa
 
Kuku wa kisasa (sijajua kama ni wote,.mimi nimefuga hawa wa MALAWI)...wana uwezo wa kutaga mayai YALIYORUTUBISHWA na yanaweza kutotolewa, pia wanataga bila jogoo, hivyo kutoa mayai YASIYORUTUBISHWA na hayawezi totolewa,.....kuwafanya watage mayai YALIYORUTUBISHWA, unahitaji kuwachanganya na majogoo, pia uwe na eneo kubwa la wazi, na utaratibu mzuri na tofauti wa chakula kati majogoo na jike....
 
Kuna siku nilijaribu kununua mayai mawili ya kisasa na kuyahifadhi kwa siku 10, siku ya 10 kuyacheck yanatoa funza na harufu kali.
 
Kuna mashamba maalum yana hawa wazazi wa broiler unaowaona kwa kikristo wanaitwa ( parental stock) hawa ndio hutoa mayai ya hawa broiler unaowaona ambao kiuhalisia wao hawawezi kuzaliana tena , na hao parental stock wakikomaa kabisa wanakua wakubwa sana anaweza kujaa kwenye ndoo ndogo
Au ndio Yale wanapanga mezani kule mbagala mguu kama WA mbuzi
 
Back
Top Bottom