Gorgeousmimi
JF-Expert Member
- Jun 21, 2010
- 9,296
- 7,683
Jinsi ya kumatayarisha kuku




Cc Revocatus Kashaga
- Mgawe kuku kwenye kifua,Mgeuze ili mgongo uwe juu na mchanechane kwenye mapaja na kifua,dhumuni la kufanya hivo ni ili viungo vikolee vizuri.

- Kama unavyoona pembeni kuna vitunguu swaumu,vitwange na umpake mkuku,fanya kama unamfanyia masaji,weka viungo kwenye sehemu zote ulizomkata mkata hakikisha vinainga ndani,kisha muweke All around spices,na mchanganyiko wa viungo vya kuku vyenye uzile,giligilani,pilipilimanga,Kari,pilipili ya unga red paprika,endelea kumfanyia masaji tumia vidole.Malizia na juisi ya limau.Ukiwa unamuweka viungo muweke pande zote.Baada ya hapo kuku atakuwa na muonekano huu

- Muache kuku akolee viungo masaa kadhaa.
- Washa oven na uweke moto 200-225 degrees
- Mchome kuku na katikati uwe unachukua ile sausi inayotoka kwa kuku na kumnyinyizia kwa juu.Akiiva juu mgeuze na upande wa pili ili apate rangi na upande huo.Mwishoni ukitaka crispy skinn weka grill juu kwa dakika tano.

- Kuku tayari kwa kuliwa,unaweza kumla na msosi wowote,wali,chipsi ugali n.k

Cc Revocatus Kashaga