Kuku wa kuoka pamoja na mboga mboga

farkhina

Platinum Member
Joined
Mar 14, 2012
Posts
14,568
Reaction score
16,917
*****Mahitaji*****

1)Kuku 1
2)kitunguu maji 1 kikubwa
3)Pilipili boga (hoho) 1
4)Kitunguu saumu na tangawizi 1tsp
5)mbatata 5 (viazi) ndogo
6)Spices upendazo
7)nyanya zilosagwa 4-5
8)giligilani
9)chicken broth mix(sio lazima)
10)ndimu 1
11)chumvi.
12)bilinganya 3 ndogo

*****Namna ya kuandaa*****

1)katakata vegetable zote weka pembeni.
2)Weka kuku chumvi na spices unazopendelea.
3)weka kuku kwenye tray juu yake weka vegetables na katia giligilani kwa juu.
4)Mimina nyanya ulosaga
5)unaweza kuongezea chumvi kwa juu na pilipili manga (mtama).
6)Funika foil na bake kwa lisaa limoja au hadi iwe imewiva.


Maasalam [emoji8].



 

Attachments

  • IMG_1959.JPG
    172.1 KB · Views: 53
Giligilani ndio bilinganya, umenitamanisha msosi huo wakati nipo hapa napiga chai na maandazi, ngoja kesho nijipange
 
Asante Madam,nitaleta mrejesho
 
Giligilani ndio bilinganya, umenitamanisha msosi huo wakati nipo hapa napiga chai na maandazi, ngoja kesho nijipange

Giligilani ni kotmir wengine tunaita ivo.au coriander.

Alafu bilinganya nimelisahau kuweka kwenye mahitaji apo ahsante kwa kunikumbusha.

Kila la kheir tunasubir kesho,chai na maandazi yummy yummy
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…