Kuku wangu wa mayai wamegoma kutaga wanaelekea week ya 19

Kuku wangu wa mayai wamegoma kutaga wanaelekea week ya 19

RUSTEM PASHA

JF-Expert Member
Joined
Jan 26, 2016
Posts
4,707
Reaction score
11,365
Nina kuku wa mayai zaidi ya 1,000 wanakwenda wiki ya 19 lakini wamegoma kudondosha yai. Licha ya kununua chakula cha kiwandani kuanzia Wana siku ya kwanza mpaka leo.

Lakini pia uzito wao walionao ni uzito stahiki kulingana na umri wao.

Naanza kupata stress maana wanatetea tu tangu week ya 16, lakini kutaga hawataki.

Msaada tutani wakuu.Ufugaji si mwepesi.
 
Mkuu uuze layers ambao washatumia zaidi ya mil 16, utawauzaje Ili upate faida kuku wa miezi minne na nusu?.
Kiukweli nilifikiri ni ule ufugaji wa 1M - 3M

16M ni uwekezaji mkubwa kwa kuku I think waliokuuzia vifaranga watakua na wataalamu wanaoweza kujibu haya maswali.

Pia zile mashine za kutotolesha hazifit kwenye bajeti ya 16M?
 
Wanakilo ngapi?
Wako wangapi?
Unalisha kilo ngapi kwa siku?
Mimi na muwakilisha wa Silverland tulichukua randomly sample ijumapili iliyopita tulikuta Wana 1.47kg,1.5Kg, 1.57kg, kwa ujumla tuliepata uzito mdogo ilikua 1.38kg, mwenye uzito mkubwa ilikua 1.6Kg.

Wako 1000, ingawa nilinunua elfu 1. Sawa na box 10, kwa Kila box wanasema walioongeza mmoja mpaka wawili, na walikufa 11. Napia walinichanganyia jogoo mmoja. Kwahio Huwa na assume wako buku tu.

Week hii ya 18, nawalisha kg 88 kwa siku.
 
Kiukweli nilifikiri ni ule ufugaji wa 1M - 3M

16M ni uwekezaji mkubwa kwa kuku I think waliokuuzia vifaranga watakua na wataalamu wanaoweza kujibu haya maswali.

Pia zile mashine za kutotolesha hazifit kwenye bajeti ya 16M?
Niliwachukua Silverland, tatizo Kuna kuku maalumu wazazi ndio wazurii kwa kutotolesha mayai yao. Na hawauzi madume wanauza majike tu.

Ingawa wanasema watataga lakini naanza kupata hofu, ilitakiwa week hii angalau nione yai hata Moja, lakini sijaona inakua hasara sasa.
 
Na kuku wangu wa mayai zaidi ya 1000 wanaenda wiki ya 19 lakini wamegoma kudondosha yai. Licha ya kununua chakula cha kiwandani kuanzia Wana siku ya kwanza mpaka leo.

Lakini pia uzito wao walionao ni uzito stahiki kulingana na umri wao.

Naanza kupata stress maana wanatetea tu tangu week ya 16, lakini kutaga hawataki.

Msaada tutani wakuu.Ufugaji si mwepesi.
Kuku huanza kutaga kati ya week ya 20 -24. Kuwahi kutaga sio dalili nzuri, kwani ni lazima via vyake vya uzazi vikomar kumuwezesha kutaga. Ambapo umri sahihi ni wiki ya 20-24

Wakitaga mapema inaweza kusababisha yai kupasukia tumboni au kumfanya ashindee kutoa yai na kupelekea kufa.

Just maintain chakula na vitamins. Soon utapata matokeo.
 
Back
Top Bottom