Kuku wangu wa mayai wamegoma kutaga wanaelekea week ya 19

Kuku huanza kutaga kati ya week ya 20 -24. Kuwahi kutaga sio dalili nzuri, kwani ni lazima via vyake vya uzazi vikomar kumuwezesha kutaga. Ambapo umri sahihi ni wiki ya 20-24

Wakitaga mapema inaweza kusababisha yai kupasukia tumboni au kumfanya ashindee kutoa yai na kupelekea kufa.

Just maintain chakula na vitamins. Soon utapata matokeo.
Asante boss kwa kunitia moyo, maana nilikua najua inatakiwa waanze kutaga week ya 18 sasa hapa na stress maana nimefata miongozo yote.
 
Digestive cruide protein kwenye chakula Cha Silverland hawashauri uongezee wanasema ipo tayari, hata kuwakata midomo week ya 15/16 walinikatalia.
Tunawakata kuku midomo ili wasidonoane. Na kudonoana au kula mayai ni dalili ya upungufu wa baadhi nutrient kwenye chakula chao. Kama unawapa chakula bora, hakuna haja ya kuwakata midomo. Kuwakata midomo kuwa kuna wastress sana.
 
Na kuku wangu wa mayai zaidi ya 1000 wanaenda wiki ya 19 lakini wamegoma kudondosha yai. Licha ya kununua chakula cha kiwandani kuanzia Wana siku ya kwanza mpaka leo.

Lakini pia uzito wao walionao ni uzito stahiki kulingana na umri wao.

Naanza kupata stress maana wanatetea tu tangu week ya 16, lakini kutaga hawataki.

Msaada tutani wakuu.Ufugaji si mwepesi.
Mkuu umekaa nao mkazungumza kujua kiini cha tatizo?
 
Na kuku wangu wa mayai zaidi ya 1000 wanaenda wiki ya 19 lakini wamegoma kudondosha yai. Licha ya kununua chakula cha kiwandani kuanzia Wana siku ya kwanza mpaka leo.

Lakini pia uzito wao walionao ni uzito stahiki kulingana na umri wao.

Naanza kupata stress maana wanatetea tu tangu week ya 16, lakini kutaga hawataki.

Msaada tutani wakuu.Ufugaji si mwepesi.
Kuku wa mayai ni sensitive sana wakati wa mabadiliko ya hewa hasa joto.wakianza kuzoea joto huanza tena kutaga.Fanya subira wape chkula alfajiri kabla hawajanza kuhema kwa sababu ya joto
 
Tunawakata kuku midomo ili wasidonoane. Na kudonoana au kula mayai ni dalili ya upungufu wa baadhi nutrient kwenye chakula chao. Kama unawapa chakula bora, hakuna haja ya kuwakata midomo. Kuwakata midomo kuwa kuna wastress sana.
Yes mkuu nawao walisema hivyohivyo.
 
Kuku wa mayai ni sensitive sana wakati wa mabadiliko ya hewa hasa joto.wakianza kuzoea joto huanza tena kutaga.Fanya subira wape chkula alfajiri kabla hawajanza kuhema kwa sababu ya joto
Hili nimeanza kulifanya week iliyopita baada yakuona nikiwapa ratio wanayotakiwa kula hawaimalizi, ikalazimika niwape chakukula alfajir na jion jua likipoa. Mchana Huwa nawapa mchicha wadonoe donoe.
 
Vipi hali ya hewa, mazingira ya banda na uwezekano wa kuwa wamepata stress? Nakushauri ita Vet atembelee mradi akupe majibu kwa anayoyaona.
Kila baada ya week 2 kuna Vet Huwa anakuja kuwaangalia napia mtu wa Silverland Huwa nae anapita japo kwa mwez mara Moja.

Hali yahewa kwa sasa Kuna joto ingawa Banda liko vizuri linapitisha upepo wa kutosha.
 
Kaka hongera Kwa mapambano ya mradi,katika kipindi kama hiki naamini umeshaandaa meoneo ya kutagia,Sasa chukua mayai Yale ya plastiki fanya kuwawekea kwenye huto tuvyumba twa kutagia,wanadai inasaidia kuchochea Hali ya kutaga Kwa kuku anaelekea kuanza kutaga...pia chunguza kama wameanza Ile Hali ya kuchuchumaa ukitaka kuwashika mgongoni,kama ndivyo soon watataga..
 
Kila baada ya week 2 kuna Vet Huwa anakuja kuwaangalia napia mtu wa Silverland Huwa nae anapita japo kwa mwez mara Moja.

Hali yahewa kwa sasa Kuna joto ingawa Banda liko vizuri linapitisha upepo wa kutosha.
Sawa Mkuu, basi subiri hii wiki ipite ukianza wiki ya 21 utaona matokeo hadi zifike wiki 24 production itakuwa imeshachanganya. Jipe hizi wiki mbili za utulivu tu kiongozi utaona matokeo positive sana si unajua wiki kwa kuku ni siku nyingi sanaa.

All the best Mkuu.
 
Asantee mkuu. Ngoja niendelee kuwa na mvumilivu. Maana hawa washenz wanakula kama nini. Kwahio nataman waanze kutaga wanipe ahueni.
 
Mzee hapo usipanic niliwahi kuwafuga Kuna mbegi wanaenda mpaka miezi 6 ndo adondoshe Yai, kaza mkanda kamanda nakuelewa sana, hao kuku ni kama Wana laana, hawajui Cha mchana Wala usiku wao ni kupiga msosi tu
Ok mkuu ngoja niendelee kukomaa nione. Ingawa wananitoboa sana mifuko. Budget yao ilikua ya week 20, sasa ngoja niongezee week zingine 3 iwe mpaka week ya 23 tofauti na hapo wataniua.
 
Na kuku wangu wa mayai zaidi ya 1000 wanaenda wiki ya 19 lakini wamegoma kudondosha yai. Licha ya kununua chakula cha kiwandani kuanzia Wana siku ya kwanza mpaka leo.

Lakini pia uzito wao walionao ni uzito stahiki kulingana na umri wao.

Naanza kupata stress maana wanatetea tu tangu week ya 16, lakini kutaga hawataki.

Msaada tutani wakuu.Ufugaji si mwepesi.
Kama umefuga kisa maneno yamotivational speaker mkuu nikupe pole kwakwel
 
wanaenda wiki ya 19 lakini wamegoma kudondosha yai

Nafikiri hili joto linachangia sana, hapa nazungumzia kama uko maeneo ya ukanda wa Pwani. Nimetumia akili ya kuzaliwa tu.Ikizidi wiki ya 24 nafikiri uanze kuchukua hatua.

Imetumika kimalkia kirahisi sana,kama una nia ya kuelewa utaelewa tu!

Asantee mkuu. Ngoja niendelee kuwa na mvumilivu. Maana hawa washenz wanakula kama nini. Kwahio nataman waanze kutaga wanipe ahueni.
Kabisa hapo ukiangalia namna viroba vinapungua lazima uchanganyikiwe kuna time kama kuna wasaidizi unaweza ukahisi wanakupiga mifuko ya msosi kumbe ni hao ndege tu wanaimaliza wenyewe. 😂
 
Nafikiri hili joto linachangia sana, hapa nazungumzia kama uko maeneo ya ukanda wa Pwani. Nimetumia akili ya kuzaliwa tu.Ikizidi wiki ya 24 nafikiri uanze kuchukua hatua.

Imetumika kimalkia kirahisi sana,kama una nia ya kuelewa utaelewa tu!

Asantee mkuu, kimalikia kwangu sio shida. Ngoja nipitie pitie niongeze maarifa.
 
Back
Top Bottom