Kuku wangu wa mayai wamegoma kutaga wanaelekea week ya 19

Kuku wangu wa mayai wamegoma kutaga wanaelekea week ya 19

Nina kuku wa mayai zaidi ya 1,000 wanakwenda wiki ya 19 lakini wamegoma kudondosha yai. Licha ya kununua chakula cha kiwandani kuanzia Wana siku ya kwanza mpaka leo.

Lakini pia uzito wao walionao ni uzito stahiki kulingana na umri wao.

Naanza kupata stress maana wanatetea tu tangu week ya 16, lakini kutaga hawataki.

Msaada tutani wakuu.Ufugaji si mwepesi.
Ikifika wiki ya 22 hujaona yai ndo uwe na wasiwasi kwa sasa bado mapema mkuu.
 
ongeza vyombo vya chakula alafu huo mfumoo unaoutumia utakuletea hasara sana wakianza kutaga
Vyombo vya chakula baadhi vilikuwa vimetolewa nje kwa ajili ya kufanyia usafi, na drinkers zisizopungua 80 na feeders zaidi ya 100.

Mkuu ndio napambana pia nguvu sina yakutosha, nilitaka Mwenyezimungu akijalia kuanzia January nianze nunua cage, sema uchumi mgumu Dokta, tunafuga kwa kutegemea mshahara.
 
Back
Top Bottom