Kuku wangu wa mayai wamegoma kutaga wanaelekea week ya 19

wiki ya 19 mbona muda wao bado mkuu au?
 
Mkuu ulitumia mbinu gani katika kuwakuza vifaranga kuepukana na vifo kipindi wakiwa wadogo?
 
Mkuu ulitumia mbinu gani katika kuwakuza vifaranga kuepukana na vifo kipindi wakiwa wadogo?
Mara yakwanza nilifuga kuku 15 wakafa nikanunua vifaranga wa mwezi mmoja 30, wakawa wanakufa, wakabaki kama 13 nikawauza.nikasema ngoja ninunue wengine 300, kwenye 300 ilikua kama shamba darasa ingawa walikufa kama 60.

Baada ya hapo ndio nikafuga 1100 wa mayai. Kwahio nibaada ya kupata uzoefu at least wa mwaka mmoja kwa vitendo. Maana mwanzo nilitaka niwe nafuga sasso nakuwauza kwenye mabucha, lkn nikaja kugundua nyama ya kuku hasa sasso wanunuzi ni wachache kheri broiler au kuku wa mayai.
 
Shukrani mkuu, nami niko kwenye foleni nasubiri vifaranga 400.
 
Huu ni utajiri.
 
Mambo yamebadilika sasa. Sisi tuliosoma Agricultural Science Sekondari enzi hizo za Nyerere na Mwinyi ilikua mpaka wafikishe miezi 6
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…